bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 18
John 18
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 19 →
1
Yesu alipokwisha kuyasema haya akatoka pamoja na wanafunzi wake kwenda ng'ambo ya kijito cha Kidoroni, kulikokuwa na kiunga. Humo wakaingia yeye na wanafunzi wake.
2
Lakini naye Yuda aliyemchongea alipajua hapo, kwani Yesu na wanafunzi wake walikusanyika mara nyingi hapo.
3
Basi, Yuda alipokwisha kupata kikosi cha askari na watumishi wa watambikaji wakuu na wa Mafariseo, akaenda kulekule, wakishika taa na mienge na selaha.
4
Yesu alipoyajua yote yatakayomjia akawatokea, akawauliza: Mwamtafuta nani?
5
Walipomjibu: Yesu wa Nasareti, akawaambia: Ni mimi. Lakini naye Yuda mwenye kumchongea alikuwa amesimama pamoja nao.
6
Alipowaambia: Ni mimi, wakarudi nyuma, wakaanguka chini.
7
Alipowauliza tena: Mwamtafuta nani? wakasema: Yesu wa Nasareti.
8
Yesu akajibu: Nimekwisha waambia: Ni mimi; mkinitafuta mimi, waacheni hawa, waende zao!
9
Imekuwa hivyo, litimie lile neno, alilolisema: Wale, ulionipa, sikuwaangamiza hata mmoja.
10
Simoni Petero alikuwa na upanga, akauchomoa, akampiga mtumwa wa mtambikaji mkuu, akamkata sikio la kuume; jina lake yule mtumwa ndiye Malko.
11
Lakini Yesu akamwambia Petero: Uchomeke upanga alani mwake! Kinyweo, Baba alichonipa, nisikinywe?
12
Kisha kikosi cha askari na mkubwa wao na watumishi wa Wayuda wakamkamata Yesu, wakamfunga.
13
Wakampeleka kwanza kwa Ana; kwani alikuwa mkwewe Kayafa aliyekuwa mtambikaji mkuu wa mwaka ule.
14
Kayafa ndiye yule aliyekula njama na Wayuda kwamba: Inafaa, mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.
15
Lakini Simoni Petero na mwanafunzi mwingine wakamfuata Yesu; yule mwanafunzi mwingine alikuwa amejuana na mtambikaji mkuu, akaingia pamoja na Yesu uani kwa mtambikaji mkuu,
16
Petero akasimama nje mlangoni. Yule mwanafunzi mwingine aliyejuana na mtambikaji mkuu akatoka, akasema na mlinda mlango, akamwingiza Petero.
17
Kisha kijakazi aliyekuwa mlinda mlango alipomwambia Petero: Wewe nawe humo miongoni mwao wanafunzi wa mtu huyo? akasema: Simo.
18
Lakini watumwa na watumishi walikuwa wamewasha moto wa makaa, kwani palikuwa na baridi, wakasimama, wakaota moto; naye Petero alisimama pamoja nao, akiota moto.
19
Mtambikaji mkuu alipomwuliza Yesu kwa ajili ya wanafunzi wake na kwa ajili ya mafundisho yake,
20
Yesu akamjibu: Mimi nimesema waziwazi ulimwenguni. Mimi siku zote nimefundisha nyumbani mwa kuombea napo Patakatifu, Wayuda wote wanapokusanyika; hakuna, nililolisema na kufichaficha,
21
Unaniulizaje? Uwaulize walionisikia, niliyowaambia! Tazama, hao wanayajua, niliyoyasema mimi.
22
Aliposema hivyo, mtumishi mmoja aliyesimama hapo akampiga Yesu kofi akisema: Mtambikaji mkuu unamjibu hivyo?
23
Yesu akamjibu: Kama nimesema maovu, ujulishe huo uovu! Lakini kama nimesema vema, unanipigia nini?
24
Basi, Ana akampeleka kwa mtambikaji mkuu Kayafa hivyo, alivyokuwa amefungwa.
25
Lakini Simoni Petero alikuwa amesimama akiota moto. Walipomwuliza: Wewe nawe humo miongoni mwao wanafunzi wake? akakana akisema: Simo.
26
Miongoni mwao watumwa wa mtambikaji mkuu mlikuwamo mmoja aliyekuwa ndugu yake yule, Petero aliyemkata sikio, akasema: Mimi sikukuona kule kiungani pamoja naye?
27
Petero akakana tena; mara hiyo jogoo akawika.
28
Wakamtoa Yesu kwa Kayafa, wakampeleka bomani kulipokucha. Wao wenyewe hawakuingia bomani kwa mwiko wao, wasijitie uchafu, wapate kula Pasaka.
29
Kwa hiyo Pilato akawatokea nje, akauliza: Mwaleta mashtaka gani ya mtu huyu?
30
Walipojibu wakimwambia: Huyu kama asingekuwa mwenye kufanya maovu, tusingemleta kwako,
31
Pilato akawaambia: Mchukueni ninyi, mmhukumu kwa Maonyo yenu! Wale Wayuda wakamwambia: Sisi hatuna ruhusa ya kuua mtu.
32
Ilikuwa hivyo, litimie lile neno, Yesu alilolisema na kuonyesha kufa kulikomngoja.
33
Pilato akaingia tena bomani, akamwita Yesu, akamwuliza: Wewe ndiwe mfalme wa Wayuda?
34
Yesu akajibu: Wasema hivi kwa mawazo yako mwenyewe, au wako wengine waliokusimulia mambo yangu?
35
Pilato akajibu: Je? Mimi Myuda? Wao wa taifa lako na watambikaji wakuu wamekuleta kwangu. Umefanya nini?
36
Yesu akajibu: Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangeupigania, nisitiwe mikononi mwa Wayuda. Lakini sasa ufalme wangu sio wa hapa.
37
Pilato akamwuliza: Basi, wewe u mfalme gani? Yesu akajibu: Wewe unavyosema, ndivyo: mimi ni mfalme. Niliyozaliwa, tena niliyojia ulimwenguni, ndiyo hii: niishuhudie iliyo ya kweli! Kila aliye na kweli huisikia sauti yangu.
38
Pilato akamwambia: Iliyo ya kweli ndiyo nini? Alipokwisha kuyasema haya akawatokea tena Wayuda, akawaambia: Mimi sioni kwake neno la kumhukumu.
39
Lakini iko desturi kwenu, niwafungulie mmoja siku ya Pasaka; basi, mwataka, niwafungulie mfalme wa Wayuda?
40
Ndipo, walipopiga makelele tena wakisema: Huyu hatumtaki, twamtaka Baraba; naye Baraba alikuwa mnyang'anyi.
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 19 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21