bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 13
John 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 14 →
1
*Sikukuu ya Pasaka ilipokuwa haijatimia, Yesu alikuwa amejua, ya kuwa saa yake imefika, autoke ulimwengu huu, aende kwa Baba; kwa kuwa aliwapenda watu wake waliomo ulimwenguni, akawapenda mpaka mwisho.
2
Walipokula chakula cha jioni, Msengenyaji alikuwa amekwisha kutia moyoni mwa Yuda wa Simoni Iskariota mawazo ya kumchongea.
3
Kwa hivyo, Yesu alivyojua, ya kuwa Baba alimpa yote mikononi mwake, ya kuwa alitoka kwa Mungu, tena anarudi kwa Mungu,
4
akainuka penye chakula, akaivua kanzu yake, akatwaa kitambaa cha ukonge, akajifunga kiunoni.
5
Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwaosha wanafunzi miguu na kuisugua kwa kile kitambaa, alichojifunga kiunoni.
6
Alipomfikia Simoni Petero, akamwambia; Bwana, wewe unioshe miguu?
7
Yesu akajibu, akamwambia: Ninachokifanya mimi, wewe hukijui sasa, lakini utakitambua halafu.
8
Petero alipomwambia: Hutaniosha miguu kale na kale, Yesu akamjibu: Nisipokuosha, hakuna fungu lako tena lililoko kwangu.
9
Ndipo, Simoni Petero alipomwambia: Bwana, usinioshe miguu tu, nioshe hata mikono na kichwa!
10
Yesu akamwambia: Aliyekwisha koga harudi tena kunawa, isipokuwa miguu, kwani ametakata wote. Nanyi mmetakata, lakini sio wote.
11
Kwani alimjua mwenye kumchongea; kwa hiyo alisema: Hamtakati nyote.
12
Alipokwisha kuwaosha miguu akayatwaa mavazi yake, akakaa tena chakulani, akawaambia; Mwakitambua, nilichowafanyia?
13
Ninyi mnaniita Mfunzi na Bwana, mnasema vema hivyo, kwani ndimi.
14
Basi, mimi niliye Bwana na Mfunzi wenu nikiwaosha ninyi miguu, imewapasa nanyi kuoshana miguu.
15
Kwani nimewapani la kujifunziamo, mfanyiane ninyi kwa ninyi, kama nilivyowafanyia mimi.*
16
Kweli kweli nawaambiani: Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake, wala mjumbe si mkubwa kuliko yule aliyemtuma.
17
Mkiyajua haya m wenye shangwe mkiyafanya.
18
Siyasemi ya ninyi nyote; mimi nawajua, niliowachagua. Lakini sharti andiko litimizwe la kwamba: Anayeula mkate wangu hunipiga mateke.
19
Nawaambia haya sasa, yanapokuwa hayajafanyika bado, kusudi hapo, yatakapofanyika, mpate kuyategemea, ya kuwa mimi ndiye.
20
Kweli kweli nawaambiani: Atakayempokea ye yote, nitakayemtuma, hunipokea mimi; naye mwenye kunipokea mimi humpokea aliyenituma.
21
Yesu alipokwisha kuyasema haya akazizimka jrohoni, akawashuhudia akisema: Kweli kweli nawaambiani: Mwenzenu mmoja atanichongea.
22
Wanafunzi wakatazamana, maana hawakumjua, aliyemsema.
23
Palikuwapo mwanafunzi wake mmoja aliyeegamia kifuani pa Yesu, ndiye, Yesu aliyempenda.
24
Simoni Petero akamkonyeza huyo, amwulize, kama ni nani, anayemsema.
25
Kisha yule aliyemwegamia Yesu kifuani akamwuliza: Bwana, ni nani?
26
Yesu akajibu: Ni yule, mimi nitakayemtowelea kitonge na kumpa. Basi, akatowelea kitonge, akakitwaa, akampa Yuda wa Simoni Iskariota.
27
Alipokwisha kukila kile kitonge, ndipo, Satani alipomwingia. Yesu akamwambia: Utakachokifanya, kifanye upesi!
28
Lakini wale waliokaa chakulani hakuna aliyeitambua sababu ya kumwambia hivyo;
29
wengine wakawaza: kwa sababu Yuda aliushika mfuko wa senti, Yesu alimwambia: Nunua chakula cha siku za sikukuu! au agawie maskini kidogo.
30
Basi, yeye alipokwisha kukipokea kile kitonge akatoka nje papo hapo, lakini ulikuwa usiku.
31
*Yule alipokwisha toka, Yesu akasema: Sasa Mwana wa mtu ametukuzwa, naye Mungu ndiye aliyetukuzwa kwake.
32
Kama Mungu alitukuzwa kwake, yeye Mungu atamtukuza kwake mwenyewe, tena atamtukuza upesi.
33
Vitoto, nipo pamoja nanyi bado kidogo; kisha mtanitafuta, lakini kama nilivyowaambia Wayuda: Ninyi hamwezi kupafika pale, ninapokwenda mimi, ndivyo, ninavyowaambia hata ninyi sasa.
34
Nawapa agizo jipya: Mpendane! Kama nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo!
35
Kwa hiyo wote watatambua, ya kama m wanafunzi wangu mimi, mtakapopendana ninyi kwa ninyi.*
36
Simoni Petero akamwambia: Bwana, unakwenda wapi? Yesu akajibu: Pale ninapokwenda, huwezi kunifuata sasa, lakini utanifuata halafu.
37
Petero akamwambia: Bwana, kwa nini siwezi sasa kufuatana na wewe?
38
Hata roho yangu nitaitoa kwa ajili yako wewe.
39
Yesu akajibu: Uitoe roho yako kwa ajili yangu mimi? Kweli kweli nakuambia: Jogoo hatawika, usipokuwa umekwisha kunikana mara tatu.
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21