bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 8
John 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 9 →
1
Yesu akaenda zake mlimani pa michekele.
2
Asubuhi na mapema alipokuja tena Patakatifu, watu wote wakamwendea, naye akakaa akiwafundisha.
3
Ndipo, waandishi na Mafariseo walipoleta mwanamke aliyefumaniwa katika ugoni, wakamsimamisha katikati.
4
Kisha wakamwambia: Mfunzi, mwanamke huyu amefumaniwa papo hapo, alipofanya ugoni.
5
Lakini Mose alituagiza katika Maonyo kuwaua wanawake walio hivyo kwa kuwapiga mawe; basi, wewe unasemaje?
6
Lakini walisema hivyo kwa kumjaribu, wapate neno la kumsuta. Yesu akainama chini, akaandika mchangani kwa kidole.
7
Lakini walipokaza kumwuliza, akainua macho, akawaambia: Ninyi, asiye na kosa na aanze kumtupia jiwe!
8
Kisha akainama tena akiandika mchangani.
9
Nao walipoyasikia wakatoka mmojammoja, walioanza ndio wazee. Wakaachwa peke yao, yeye na yule mwanamke aliyekuwa hapo kati.
10
Yesu alipoinua macho, akamwambia: Mama, wako wapi wale waliokusuta? Hakuna aliyekupatiliza?
11
Aliposema: Hakuna, Bwana, Yesu akasema: Basi, hata mimi sikupatilizi; nenda zako! Lakini tangu sasa usikose tena!
12
Kisha Yesu akawaambia tena akisema: Mimi ndio mwanga wa ulimwengu; anifuataye mimi hataendelea kwenda gizani, ila atakuwa anao mwanga wa uzima.
13
Mafariseo wakamwambia: Wewe unajishuhudia mwenyewe; huu ushuhuda wako sio wa kweli.
14
Yesu akajibu, akawaambia: Hata nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ndio wa kweli; kwani ninajua, nilikotoka, tena ninakokwenda. Lakini ninyi hamjui, nitokako wala niendako.
15
Ninyi mwahukumu kimtu, mimi sihukumu mtu.
16
Lakini ijapo nihukumu mtu, hukumu yangu ni ya kweli kwani siko peke yangu, ila tuko mimi na yule aliyenituma.
17
Hata katika Maonyo yenu imeandikwa: Ushuhuda wa watu wawili ni wa kweli.
18
Mimi ndiye ninayejishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenituma hunishuhudia.
19
Wakamwambia: Baba yako yuko wapi? Yesu akajibu: Hamnijui mimi, wala hammjui Baba yangu. Kama mngenijua mimi mngemjua naye Baba yangu.
20
Maneno haya aliyasema penye sanduku ya vipaji alipofundishia Patakatifu. Lakini hata mmoja hakumkamata, kwani saa yake ilikuwa haijafika.
21
Akawaambia tena: Mimi nakwenda zangu, nanyi mtanitafuta, hata kufa mtakufa, mko katika ukosaji wenu. Niendako mimi, ninyi hamwezi kukufika.
22
Wayuda wakasema: Je? Atajiua mwenyewe akisema: Niendako mimi, ninyi hamwezi kukufika?
23
Akawaambia: Ninyi mmetoka huku nchini, mimi nimetoka huko juu. Ninyi mmetoka humu ulimwenguni, mimi sikutoka humu ulimwenguni.
24
Kwa hiyo naliwaambia: Kufa mtakufa, mko katika ukosaji wenu. Kwani msiponitegemea, ya kuwa mimi ndiye, mtakufa, mko katika ukosaji wenu.
25
Wakamwambia: Wewe ndiwe nani? Yesu akawaambia: Nimewaambia tangu mwanzo, kwa sababu gani niiseme tena?
26
Kama ningeyasema yale mengi, mliyoyafanya, ningewaumbua; lakini aliyenituma ni wa kweli, nami niliyoyasikia kwake, ndiyo, ninayoyasema ulimwenguni.
27
Hawakutambua, ya kuwa aliwaambia mambo ya Baba.
28
Kisha Yesu akasema: Hapo, mtakapomkweza Mwana wa mtu, ndipo, mtakapotambua, ya kuwa mimi ndiye. Hakuna ninayoyafanya kwa mapenzi yangu, ila Baba aliyonifundisha ndiyo, ninayoyasema.
29
Naye aliyenituma yuko pamoja nami; hakuniacha peke yangu, kwani mimi siku zote nayafanya, yanayompendeza.
30
Alipoyasema haya, wengi wakamtegemea.
31
*Hao Wayuda waliomtegemea Yesu akawaambia: Ninyi mkilikalia Neno langu, kweli m wanafunzi wangu,
32
mwitambue iliyo ya kweli, nayo iliyo ya kweli itawakomboa.
33
Wakamjibu: Sisi tu uzao wake Aburahamu, hatujawa bado watumwa wa mtu, nawe wasemaje: Mtakombolewa?
34
Yesu akawajibu: Kweli kweli nawaambiani: Kila afanyaye makosa ni mtumwa wa makosa.
35
Naye mtumwa hakai nyumbani kale na kale, lakini mwana ndiye akaaye kale na kale.
36
Basi, huyo Mwana atakapowakomboa, mtakuwa mmekombolewa kweli.*
37
Ninajua, ya kuwa ninyi m uzao wake Aburahamu. Lakini mnatafuta kuniua, kwani ndani yenu Neno langu halipati pa kukaa.
38
Mimi niliyoyaona kwa Baba, ndiyo, ninayoyasema. Nanyi yafanyeni, mliyoyasikia kwake Baba!
39
Ndipo, walipojibu na kumwambia: Baba yetu ni Aburahamu. Yesu akawaambia: Mkiwa watoto wake Aburahamu yafanyeni matendo yake Aburahamu!
40
Lakini sasa mnatafuta kuniua; nami nimewaambia iliyo ya kweli, niliyoisikia kwa Mungu; hivyo Aburahamu hakuvifanya.
41
Ninyi huyafanya matendo ya baba yenu. Wakamwambia: Sisi hatukuzaliwa kwa ugoni. Tunaye baba mmoja, ndiye Mungu.
42
Yesu akawaambia: Mungu kama angekuwa Baba yenu, mngenipenda mimi. Kwani mimi nimetoka kwa Mungu, nikaja huku, lakini sikujijia mwenyewe tu, ila yeye alinituma.
43
Mbona hamyatambui ninayoyasema? Ni kwa sababu hamwezi kulisikia Neno langu.
44
Ninyi mmetoka kwa baba yenu, ni yule Msengenyaji; kwa hiyo mnataka kuzifanya tamaa za baba yenu. Yeye alikuwa mwua watu tangu mwanzo, hakusimama penye kweli, kwani moyoni mwake hamna iliyo ya kweli. Anaposema uwongo anasema yaliyo yake yeye, kwani ni mwongo na baba yake uwongo.
45
Lakini mimi ninaposema iliyo ya kweli, hamnitegemei.
46
*Kwenu yuko nani anayeweza kuniumbua kuwa mwenye kosa lo lote? Nikisema iliyo ya kweli, mbona ninyi hamnitegemei?
47
Aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu. Kwa hiyo ninyi hamyasikii, kwani ninyi ham wa Mungu.
48
Wayuda wakajibu, wakamwambia: Sisi hatusemi kweli: Ndiwe Msamaria? Tena una pepo?
49
Yesu akajibu: Mimi sina pepo, ila ninamheshimu Baba yangu, nanyi mwanibeza.
50
Lakini mimi sitafuti, nitukuzwe. Yuko anayevitafuta na kuhukumu.
51
Kweli kweli nawaambiani: Mtu atakapolishika Neno langu hataona kufa kale na kale.
52
Ndipo, Wayuda walipomwambia: Sasa tumekutambua, ya kuwa una pepo. Aburahamu amekufa, nao wafumbuaji wamekufa, na wewe wasema: Mtu atakapolishika Neno langu hataona kufa kale na kale?
53
Je? Wewe u mkubwa kuliko baba yetu Aburahamu aliyekufa? Nao wafumbuaji wamekufa. Wajifanya kuwa nani?
54
Yesu akajibu: Nikijipa utukufu mwenyewe, utukufu wangu ni wa bure; lakini Baba yangu ndiye anayenipa utukufu, ni yeye, mnayemsema ninyi: Ni Mungu wetu.
55
Nanyi hamkumtambua yeye, lakini mimi nimemjua. Nami kama ningesema: Simjui, ningefanana nanyi kuwa mwongo. Lakini nimemjua, nalo Neno lake ninalishika.
56
Baba yenu Aburahamu alishangilia, kwamba aione siku yangu; akaiona, akafurahi.
57
Wayuda wakamwambia: Hujapata bado miaka 50, nawe umemwona Aburahamu?
58
Yesu akawaambia: Kweli kweli nawaambiani: Aburahamu alipokuwa hajakuwapo bado, mimi nilikuwa nipo.
59
Ndipo, walipookota mawe, wamtupie. Lakini Yesu akawa amefichika, akapatoka patakatifu.*
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21