bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 15
John 15
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 16 →
1
*Mimi ni mzabibu wa kweli naye Baba yangu ndiye mpalilizi.
2
Kila tawi langu lisilozaa huliondoa; lakini kila tawi lizaalo hulitakasa akilipogoa, lipate kuzaa mengi.
3
Ninyi mmekwisha kutakata mkilipokea lile Neno, nililowaambia.
4
Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu! Kama tawi lisivyoweza kuzaa likiwa peke yake, lisipokaa mzabibuni, vivyo hivyo nanyi hamna mwezacho, msipokaa ndani yangu.
5
Mimi ni mzabibu, ninyi m matawi. Anayekaa ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa mengi. Kwani pasipo mimi hamna mwezacho kukifanya.
6
Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi, likikauka; kisha watu huyakusanya pamoja na kuyatupa motoni yateketee.
7
Mtakapokaa ndani yangu, nayo maneno yangu yatakapokaa ndani yenu, mtaomba lo lote, mnalolitaka, kisha mtalipata.
8
Hapo ndipo, Baba yangu anapotukuzwa, mnapozaa mengi, mkawa wanafunzi wangu.*
9
*Kama Baba alivyonipenda, ndivyo, nami ninavyowapenda ninyi. Kaeni na kunipenda!
10
Mtakapoyashika maneno yangu mtakaa na kunipenda, kama mimi nilivyoyashika maagizo ya Baba yangu, nikakaa na kumpenda yeye.
11
Nimewaambia haya, furaha yangu iwakalie, nanyi furaha yenu itimie yote.
12
Hili ndilo agizo langu: Mpendane, kama nilivyowapenda!
13
Hakuna mwenye upendo kumpita mwenye kujitoa, awaokoe wapenzi wake.
14
Ninyi m wapenzi wangu mkiyafanya, ninayowaagiza.
15
Sitawaita tena watumwa, kwani mtumwa hayajui, bwana wake anayoyafanya. Nimewaita wapenzi, kwani yote, niliyoyasikia kwa Baba yangu, nimewatambulisha ninyi.
16
Sio ninyi mlionichagua, lakini ndiye mimi niliyewachagua ninyi, nikawaweka, mwende kuzaa matunda, nayo matunda yenu yakae; kwa hiyo Baba atawapa lo lote, mtakalomwomba katika Jina langu.*
17
Haya nawaagizani: Mpendane!
18
Ulimwengu ukiwachukia, tambueni, ya kuwa mimi ni mtangulizi wenu aliyeanza kuchukiwa nao!
19
Kama mngekuwa wa ulimwengu, wao wa ulimwengu wangewapenda, kwamba m wenzao. Lakini kwa sababu ham wa ulimwengu, kwani mimi naliwachagua na kuwatoa ulimwenguni, kwa hiyo wao wa ulimwengu huwachukia.
20
Likumbukeni lile neno, nililowaambia: Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake! Kama wamenifukuza mimi, watawafukuza nanyi.
21
Kama wamelishika Neno langu, hata lenu watalishika. Lakini hayo yote watawafanyia kwa ajili ya Jina langu, kwani hawamjui aliyenituma.
22
Kama singalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na kosa; lakini sasa hawana, watakalojikania makosa yao.
23
Mwenye kunichukia mimi humchukia naye Baba yangu.
24
Kama singalifanya kwao kazi, mwingine asizozifanya hata kale, wasingalikuwa na kosa. Lakini sasa wameziona, kisha wametuchukia, mimi na Baba yangu.
25
Lakini sharti litimie neno lililoandikwa katika Maonyo yao ya kwamba: Walinichukia bure.
26
*Lakini atakapokuja mtuliza mioyo, nitakayemtuma toka kwa Baba, yule Roho wa kweli atakayetoka kwa Baba, ndiye atakayenishuhudia.
27
Lakini nanyi m mashahidi, kwani tangu mwanzo mlikuwa pamoja nami.
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21