bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 6
John 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 7 →
1
*Kisha Yesu akaondoka kwenda ng'ambo ya bahari ya Galilea iitwayo ya Tiberia.
2
Kundi la watu wengi likamfuata, kwani waliviona vielekezo, alivyowafanyia wagonjwa.
3
Yesu akapanda mlimani, akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.
4
Lakini Pasaka ilikuwa karibu, ndiyo sikukuu ya Wayuda.
5
Yesu alipoyainua macho yake, akaona kundi la watu wengi wanaomjia, akamwambia Filipo: Tununue wapi mikate, hawa wapate kula?
6
Hivyo alivisema, amjaribu; kwani mwenyewe alijua, alichotaka kukifanya.
7
Filipo akamjibu: Mikate ya shilingi 200 haiwatoshi, kila mmoja apate kidogo tu.
8
Mmoja wao wanafunzi wake Anderea, nduguye Simoni Petero, akamwambia:
9
Hapa yupo mtoto mdogo, anayo mikate mitano ya mofa na visamaki viwili. Lakini hivyo vitawafaa nini watu walio wengi kama hawa?
10
Yesu akasema: Wakalisheni watu! maana mahali pale palikuwa na majani mengi; waliokaa waume tu walikuwa kama 5000.
11
Kisha Yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia waliokaa; vile vile navyo visamaki, kama walivyotaka.
12
Lakini waliposhiba, akawaambia wanafunzi wake: Yakusanyeni makombo yaliyosalia, pasipatikane kinachopotea!
13
Wakayakusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili makombo ya mikate ile mitano ya mofa yaliyowasalia waliokula.
14
Watu walipokiona kielekezo hicho, alichokifanya, wakasema: Kweli huyu ndiye mfumbuaji atakayekuja ulimwenguni.
15
Yesu alipowatambua, ya kuwa wanataka kuja, wamshike kwa nguvu, wamfanye mfalme, akaondoka tena akaja mlimani yeye peke yake tu.
16
Lakini jua lilipokwisha kuchwa, wanafunzi wake wakatelemka kwenda baharini,
17
wakaingia chomboni, wavuke kwenda Kapernaumu ng'ambo ya bahari. Giza ilipokwisha kuingia, Yesu alikuwa hajafika kwao bado.
18
Namo baharini mkainuka mawimbi kwa upepo uliovuma na nguvu.
19
Walipokwisha endelea mwendo wa nusu saa na kupita kidogo, wakamwona Yesu, anavyokwenda juu ya bahari na kukifikia chombo karibu, wakaogopa.
20
Ndipo, alipowaambia: Ni miye, msiogope!
21
Walipotaka kumwingiza chomboni, mara chombo kikawa ufukoni kwenye nchi, walikokwenda.
22
Kesho yake kundi la watu waliosimama ng'ambo ya bahari waliona, ya kuwa hakuwako chombo kingine huko, ni kile kimoja tu. Nao walikuwa wameona, ya kuwa Yesu hakuingia chomboni pamoja na wanafunzi wake; waliona, wanafunzi wake walivyoondoka peke yao.
23
Lakini vyombo vingine vilivyotoka Tiberia vikafika karibu ya mahali pale, walipokula mikate, Bwana akiiombea.
24
*Watu walipoona, ya kuwa Yesu hayuko, ya kuwa wanafunzi wake hawako nao, wakaingia katika vile vyombo, wakafika Kapernaumu, wamtafute Yesu.
25
Walipomwona ng'ambo ya bahari wakamwuliza: Mfunzi mkuu, umefika lini hapa?
26
Yesu akawajibu akisema: Kweli kweli nawaambiani: Hamnitafuti, kwa maana mmeona vielekezo, ila kwa maana mmeila ile mikate, mkashiba.
27
Sumbukieni vyakula! Lakini vile vinavyoangamia sivyo, ni vile vinavyokaa, viwafikishe penye uzima wa kale na kale, navyo ndivyo, Mwana wa mtu atakavyowapani ninyi. Kwani huyu ndiye, Baba Mungu aliyemwagiza hivyo na kumtia muhuri.
28
Walipomwuliza: Tufanyeje, tupate kuzisumbukia kazi za Mungu?
29
Yesu akajibu, akawaambia: Hii ndiyo kazi ya Mungu, mkimtegemea yeye, aliyemtuma.*
30
Wakamwambia tena: Wewe unafanya kielekezo gani, tukione, tukutegemee? Wewe unasumbukia nini?
31
Baba zetu walikula Mana jangwani, kama ilivyoandikwa: Aliwapa mikate iliyotoka mbinguni, waile.
32
Yesu akawaambia: Kweli kweli nawaambiani: Mose siye aliyewapa ninyi mikate iliyotoka mbinguni, ila Baba yangu ndiye anayewapa ninyi mkate wa kweli utokao mbinguni.
33
Kwani mkate wa Mungu ndio ule ushukao toka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.
34
Ndipo, walipomwambia: Bwana, tupe siku zote mkate huo!
35
Yesu akawaambia: Mimi ndio mkate wa uzima; ajaye kwangu hataona njaa, naye anitegemeaye hataona kiu hata siku moja.
36
Lakini ndivyo, nilivyowaambia: Mmeniona, lakini hamnitegemei.
37
Wote, Baba anipao, ndio watakaokuja kwangu; naye ajaye kwangu sitamfukuza, ajiendee.
38
Kwani sikushukia toka mbinguni kuyafanya mapenzi yangu mimi, ila mapenzi yake yeye aliyenituma.
39
Nayo mapenzi yake yeye aliyenituma ndiyo haya: wote, alionipa, nisiwapoteze hata mmoja wao, ila niwafufue siku ya mwisho.
40
Kwani haya ndiyo mapenzi ya Baba yangu: kila anayemtazamia Mwana na kumtegemea apate uzima wa kale na kale, nami nitamfufua siku ya mwisho.
41
Wayuda wakamnung'unikia, kwa sababu alisema: Mimi ndio mkate ulioshuka toka mbinguni,
42
wakasema: Huyu siye Yesu, mwana wa Yosefu? Hatumjui baba yake na mama yake? Asemaje sasa: Nimeshuka toka mbinguni?
43
Yesu akajibu, akawaambia: Msinung'unike ninyi kwa ninyi!
44
Hakuna awezaye kuja kwangu, Baba aliyenituma asipomvuta, nami nitamfufua siku ya mwisho.
45
Katika Wafumbuaji yameandikwa ya kwamba: Wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Kila amsikiaye Baba na kujifunza kuja kwangu.
46
Sisemi: Yuko aliyemwona Baba, asipokuwa yule aliyetoka kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwona Baba.
47
*Kweli kweli nawaambiani: Anitegemeaye anao uzima wa kale na kale.
48
Mimi ndio mkate wa uzima.
49
Baba zenu walikula Mana jangwani, kisha wakafa.
50
Huu ndio mkate ushukao toka mbinguni, kwamba: Mwenye kuula asife!
51
Mimi ndio mkate wenye uzima ulioshuka toka mbinguni. Mtu atakayeula mkate huu atakuwa mzima pasipo mwisho. Nao mkate, nitakaowapa mimi, ndio mwili wangu utakaotolewa, ulimwengu upate uzima.
52
Wayuda wakabishana wao kwa wao wakisema: Huyu atawezaje kutupa mwili wake, tuule?
53
Yesu akawaambia: Kweli kweli nawaambiani: Msipoula mwili wa Mwana wa mtu, tena msipoinywa damu yake, hamna uzima mwenu.
54
Mwenye kuula mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa kale na kale, nami nitamfufua siku ya mwisho.
55
Kwani mwili wangu ni chakula cha kweli, nayo damu yangu ni kinywaji cha kweli.
56
Mwenye kuula mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa mwangu, nami mwake.
57
Kama Baba Mwenye uzima alivyonituma, tena kama mimi nilivyo mzima kwa nguvu ya Baba, vivyo hivyo naye mwenye kunila atakuwa mzima kwa nguvu yangu.*
58
Huo ndio mkate ulioshuka toka mbinguni, si kama ile, baba zenu waliyoila, wakafa. Mwenye kuula mkate huu atakuwa mzima pasipo mwisho.
59
Maneno haya aliyasema akifundisha nyumbani mwa kuombea huko Kapernaumu.
60
*Wengi waliokuwa wanafunzi wake walipoyasikia wakasema: Neno hili ni gumu. Yuko nani awezaye kulisikia?
61
Lakini Yesu kwa kujua moyoni mwake, ya kuwa wanafunzi wake wanalinung'unikia hilo, akawaambia: Hili linawakwaza?
62
Vitakuwaje, mkiona, Mwana wa mtu anavyopaa huko, alikokuwa kwanza?
63
Roho ndiyo inayotupatia uzima, mwili haufai kitu. Maneno, niliyowaambia, ndiyo ya Kiroho yenye uzima.
64
Lakini kwenu wako wasionitegemea. Kwani tangu mwanzo Yesu aliwajua wasiomtegemea, naye atakayemchongea alimjua vilevile.
65
Akasema: Kwa hiyo nimewaambia: Hakuna awezaye kuja kwangu, asipokuwa amepewa na Baba yangu.
66
Tokea hapo wengi waliokuwa wanafunzi wake wakarudi nyuma, wasifuatane tena naye.
67
Yesu alipowauliza wale kumi na wawili: Nanyi mwataka kujiendea?
68
ndipo, Simoni Petero alipomjibu: Bwana, tumwendee nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa kale na kale.
69
Nasi tumekutegemea, tukatambua, ya kuwa wewe ndiwe Kristo, Mwana wake Mungu Mwenye uzima.*
70
Yesu akawajibu: Mimi sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Tena mmoja wenu ni msengenyaji!
71
Hapo alimsema Yuda wa Simoni, yule Iskariota; kwani huyo ndiye aliyemchongea halafu. Naye alikuwa miongoni mwao wale kumi na wawili.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21