bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 16
John 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 17 →
1
Haya nimewaambia, maana msije kukwazwa.
2
Watawakataza kuziingia nyumba za kuombea; kweli saa inakuja, kila mwenye kuwaua ninyi atakapodhani, ya kuwa anamtumikia Mungu.
3
Hivyo watavifanya, kwa sababu hawakumtambua Baba wala mimi.
4
Lakini nimewaambia haya, kwamba saa yao itakapokuja, myakumbuke, ya kuwa mimi nimewaambia ninyi. Lakini tangu mwanzo sikuwaambia haya kwa hivyo, nilivyokuwa pamoja nanyi.*
5
*Lakini sasa nakwenda kwake yeye aliyenituma, tena kwenu hakuna anayeniuliza: Unakwenda wapi?
6
Ila kwa sababu nimewaambia haya, mioyo yenu imejaa masikitiko.
7
Lakini mimi nawaambiani lililo la kweli: Inawafalia, mimi niende zangu. Kwani nisipokwenda zangu, mtuliza mioyo hatawajia. Lakini nitakapokwenda, nitamtuma kwenu.
8
Naye atakapokuja atawaumbua wao wa ulimwengu kuwa wenye makosa wasio nalo la kujikania, wanaopaswa na kuhukumiwa.
9
Ndio wenye makosa, kwa kuwa hawanitegemei mimi;
10
hawana la kujikania, kwa kuwa nakwenda kwa Baba, nanyi hamnioni tena;
11
wapaswa na kuhukumiwa, kwa kuwa mtawala ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.
12
Yako maneno mengi bado, ninayotaka kuwaambia; lakini sasa mngeyaona kuwa mzigo usiochukulika.
13
Lakini yule atakapokuja, yule Roho wa kweli, yeye atawaongoza, awapeleke penye yote yaliyo ya kweli. Kwani hatayasema maneno yake mwenyewe, ila atayasema, atakayoyasikia, awatangazie nayo yatakayokuja.
14
Yeye ndiye atakayenitukuza, kwani katika yale yaliyo yangu ndimo, atakamoyatwaa, atakayowatangazia ninyi.
15
Yote, Baba aliyo nayo, ni yangu; kwa hiyo nilisema: Katika yale yaliyo yangu ndimo, atakamoyatwaa, atakayowatangazia ninyi.*
16
*Bado kidogo hamtaniona; tena patakapopita kitambo kidogo, mtaniona tena, kwa sababu ninakwenda kwa Baba.
17
Basi, kulikuwako wanafunzi wake waliosemezana wao kwa wao: Neno hili, analotuambia, ni neno gani la kwamba: Bado kidogo hamtaniona, tena patakapopita kidogo, mtaniona? Na tena: Ninakwenda kwa Baba?
18
Wakasema: Lile bado kidogo, alisemalo, ni kusemaje? Hatujui, analosema.
19
Kwa kuwatambua, ya kuwa walitaka kumwuliza, Yesu akawaambia: Mnaulizana kwa hilo, nililolisema: Bado kidogo hamtaniona; tena patakapopita kidogo, mtaniona?
20
Kweli kweli nawaambiani: Ninyi mtalia na kuomboleza, lakini wao wa ulimwengu watafurahi. Ninyi mtasikitika, lakini sikitiko lenu litageuka kuwa furaha.
21
Mwanamke anapozaa husikitika, kwani saa yake imekuja; lakini akiisha kumzaa mwana hayakumbuki tena maumivu, ila hufurahi kwa ajili ya mtu aliyezaliwa kukaa ulimwenguni.
22
Basi, nanyi sasa mnasikitika, lakini tutaonana tena, ndipo, mioyo yenu itakapofurahi; hiyo furaha yenu hakuna atakayeiondoa kwenu.
23
Siku ile hamtaniuliza neno.* *Kweli kweli nawaambiani: Lo lote, mtakalomwomba Baba, atawapa katika Jina langu.
24
Mpaka leo hakuna, mliloliomba katika Jina langu. Ombeni! Ndipo, mtakapopewa, furaha yenu iwe imetimizwa yote!
25
Haya nimewaambia kwa mifano. Lakini saa inakuja, itakapokuwa, nisiseme nanyi tena kwa mifano, ila nitawatolea waziwazi mambo ya Baba.
26
Siku ile mtaomba katika Jina langu, nani siwaambii: Mimi nitawaombea ninyi kwake Baba.
27
Kwani Baba mwenyewe anawapenda, kwa sababu ninyi mmenipenda mimi na kunitegemea kwamba: Mimi nimetoka kwa Baba.
28
Nimetoka kwa Baba, nikaingia ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu, niende kwa Baba.
29
Ndipo, wanafunzi wake waliposema: Tazama, sasa unasema waziwazi, usiseme mfano wo wote.
30
Sasa tunajua, ya kuwa unayajua yote, ya kuwa huulizwi na mtu. Kwa hiyo tunakutegemea, ya kuwa umetoka kwa Mungu.
31
Yesu akawajibu: Sasa mnanitegemea?
32
Tazameni, saa inakuja, tena imekwisha fika, mtawanyike kila mtu na kwao kwenyewe, mniache mimi, niwe peke yangu. Lakini mimi sipo peke yangu, kwani Baba yupo pamoja nami.
33
Haya nimewaambia, mpate kutengemana mwangu. Ulimwenguni mnayo maumivu; lakini tulieni mioyo! Mimi nimeushinda ulimwengu.*
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21