bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 10
John 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 11 →
1
Kweli kweli nawaambiani: Asiyepita mlangoni, apate kuingia zizini mwa kondoo, akipandia pengine, huyo ni mwizi na mnyang'anyi.
2
Lakini anayeingia mlangoni ndiye mchungaji wa kondoo.
3
Mlinda mlango anamfungulia huyo, nao kondoo humsikia sauti yake. Naye huwaita kondoo walio wake kwa majina yao, huwatoa nje.
4
Akiisha kuwatoa nje hutangulia mbele yao wote walio wake, nao kondoo humfuata, kwani wameijua sauti yake.
5
Lakini mgeni hawatamfuata, ila watamkimbia, kwani hawazijui sauti za wageni.
6
Fumbo hili Yesu aliwaambia, lakini wale hawakuitambua maana yao, aliyowaambia.
7
Yesu akasema tena: Kweli kweli nawaambiani: Mimi ndio mlango wa kondoo.
8
Wo wote waliokuja mbele yangu ndio wezi na wanyang'anyi; kwa hiyo kondoo hawakuwasikia.
9
Mimi ndio mlango. Mtu akiingilia kwangu mimi ataokoka, atakapoingia napo atakapotoka, apate malisho.
10
Mwizi haji, asipotaka kwiba na kuchinja na kuangamiza. Mimi nimekuja, wakae wenye uzima na wenye vingine vyote.
11
*Mimi ndiye mchungaji mwema; mchungaji mwema hujitoa kwa ajili ya kondoo.
12
Lakini mfanya kazi, asiye mchungaji wala mwenye kondoo, huwaacha kondoo na kukimbia anapomwona chui, akija. Naye chui huwakamata na kuwatawanya.
13
Kwani yeye ni mfanya kazi tu, hawasumbukii kondoo.
14
Mimi ndiye mchungaji mwema, ninawatambua walio wangu, nao walio wangu hunitambua mimi;
15
ndivyo, kama Baba anavyonitambua mimi, na kama mimi ninavyomtambua Baba. Nami mwenyewe ninajitoa, nife kwa ajili ya kondoo.
16
tena ninao kondoo wengine, wasio wa zizi hili; nao hao sharti niwalete, nao wataisikia sauti yangu; kisha watakuwa kundi moja na mchungaji mmoja.*
17
Kwa hiyo Baba ananipenda, kwa sababu najitoa mwenyewe, nife, nipate tena kuwapo.
18
Hakuna anayenishurutisha hivyo, ila mimi ninajitoa mwenyewe. Nina uwezo wa kujitoa, nife, tena nina uwezo wa kuwapo tena. Hivi ndivyo, alivyoniagiza Baba yangu.
19
Wayuda wakakosana tena kwa ajili ya maneno haya.
20
Wengine wao wakasema: Ana pepo, tena yuko na wazimu. Mwamsikilizaje?
21
Wengine wakasema: Maneno haya siyo ya mwenye wazimu. Yuko pepo awezaye kuwafumbua vipofu macho?
22
Kisha pakawa na sikukuu ya mweuo wa Patakatifu huko Yerusalemu; siku zake zilikuwa za kipupwe.
23
*Yesu alipokuwa anatembea hapo Patakatifu katika ukumbi wa Salomo,
24
Wayuda wakamzunguka, wakamwambia: Unatuhangisha roho zetu mpaka lini? Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie waziwazi!
25
Yesu akawajibu: Naliwaambia, nanyi hamnitegemei. Kazi, ninazozifanya katika Jina la Baba yangu, hizo zinanishuhudia.
26
Lakini ninyi hamnitegemei, kwani ninyi hammo katika kondoo wangu.
27
Kondoo wangu huisikia sauti yangu, nami nawajua, nao hunifuata.
28
Nami nawapa uzima wa kale na kale; hawataangamia kale na kale, wala hakuna mtu atakayewapoka mkononi mwangu.
29
Yeye Baba aliyenipa wale ni mkubwa kuliko wote; hakuna mtu anayeweza kuwapoka mkononi mwake Baba.
30
Mimi na Baba tu mmoja.*
31
Wayuda walipookota tena mawe, wamtupie,
32
Yesu akawajibu: Matendo mengi yaliyo mazuri nimewaonyesha kwa nguvu ya Baba; katika hayo ni lipi, mwatakalo kunipigia mawe?
33
Wayuda wakamjibu: Si kwa ajili ya tendo zuri, tukitaka kukupiga mawe, ila kwa ajili ya kumbeza Mungu, kwani wewe uliye mtu unajifanya kuwa Mungu.
34
Yesu akawajibu: Katika Maonyo yenu hamkuandikwa kwamba: Mimi nalisema: Ninyi m miungu? Nalo lililoandikwa haliwezi kutanguliwa.
35
Kama aliwaita wale miungu walioambiwa Neno la Mungu,
36
basi, mimi, ambaye Baba alinitakasa na kunituma ulimwenguni, mwanisemaje: Unambeza Mungu, kwa sababu nalisema: Mimi ni Mwana wake Mungu?
37
Nisipoyafanya matendo ya Baba yangu, msinitegemee!
38
Lakini ninapoyafanya, yategemeeni matendo hayo, msipotaka kunitegemea mimi! Nanyi mpate kujua na kutambua, ya kuwa Baba yumo mwangu, nami nimo mwake Baba.
39
Basi, wakatafuta tena kumkamata, lakini akatoka mikononi mwao.
40
Kisha akaondoka tena kwenda ng'ambo ya Yordani mahali pale, Yohana alipokuwa akibatiza hapo kwanza; akakaa pale.
41
Watu wengi wakamwendea hapo, wakasema: Yohana hakufanya kielekezo cho chote, lakini yote, Yohana aliyoyasema yake huyu, yalikuwa ya kweli.
42
Kwa hiyo wengi wakamtegemea pale.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21