bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
John 17
John 17
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 18 →
1
Yesu alipokwisha kuyasema haya akayaelekeza macho yake mbinguni, akasema: Baba, saa imekwisha fika. Mtukuze Mwana wako, Mwana wako naye akutukuze!
2
Ni kama hivyo, ulivyompa kumtawala kila mwenye mwili, awape wote, uliompa, uzima wa kale na kale.
3
Nao huu ndio uzima wa kale na kale, wakutambue wewe, kwamba ndiwe peke yako Mungu wa kweli, tena wamtambue yule, uliyemtuma, kwamba ndiye Yesu Kristo.
4
Mimi nimekutukuza nchini na kuitimiza kazi, uliyonipa ya kuifanya.
5
Sasa, Baba, unitukuze kwako wewe na kunipa utukufu, niliokuwa nao nilipokuwa kwako, ulimwengu ulipokuwa haujawa bado.
6
Jina lako nimewafumbulia watu, ulionipa na kuwatoa ulimwenguni. Walikuwa wako, nawe umenipa mimi, nalo Neno lako wamelishika.
7
Sasa wametambua, ya kuwa yote, uliyonipa, yametoka kwako.
8
Kwani yale maneno, uliyonipa, nimewapa, wakayapokea, wakatambua kweli, ya kuwa nilitoka kwako, wakanitegemea, ya kuwa wewe ndiwe uliyenituma.
9
Mimi nawaombea hao, siuombei ulimwengu, ila nawaombea wale tu, ulionipa, kwani ni wako.
10
Nayo yote yaliyo yangu ni yako, nayo yaliyo yako ni yangu; namo mwao ndimo, nilimotukuzwa.
11
Nami simo tena ulimwenguni, lakini wao wamo ulimwenguni, kwani mimi nakuja kwako. Baba Mtakatifu, walinde, wakae na Jina lako, ulilonipa, wapate kuwa mmoja wote, kama sisi tulivyo mmoja!
12
Nilipokuwa pamoja nao naliwalinda, wakae na Jina lako, ulilonipa, nikawaangalia. Nao hawakuangamia hata mmoja wao, pasipo yule mwana wa mwangamizo, yaliyoandikwa yapate kutimia.
13
Lakini kwa kuwa sasa nakuja kwako, nayasema haya ulimwenguni, waipate furaha yangu, iwajie yote.
14
Mimi nimewapa Neno lako, ulimwengu ukawachukia, kwa sababu wao sio wa ulimwengu, kama mimi nisivyokuwa wa ulimwengu.
15
Siombi, uwaondoe ulimwenguni, ila naomba, uwalinde, yule Mbaya asiwajie.
16
Wao sio wa ulimwengu, kama mimi nisivyokuwa wa ulimwengu.
17
Watakase, wawe wa kweli! Neno lako ndilo la kweli.
18
Kama wewe ulivyonituma kwenda ulimwenguni, ndivyo nami nilivyowatuma kwenda ulimwenguni.
19
Nao ndio, ninaojitakasia mwenyewe, kwamba nao wawe watu waliotakaswa kweli.
20
Lakini si hawa tu, ninaowaombea, ila nawaombea hata wale watakaonitegemea wakilisikia neno lao.
21
Wote wapate kuwa mmoja, kama ulivyomo mwangu, wewe Baba, nami nilivyomo mwako! Wapate kuwamo mwetu nao hao, ulimwengu upate kunitegemea, ya kuwa wewe umenituma.
22
Nami nimewapa utukufu, ulionipa wewe, wapate kuwa mmoja, kama sisi tulivyo mmoja.
23
Mimi niwemo mwao, nawe wewe uwemo mwangu, wawe watu waliomaliza kuwa mmoja, nao ulimwengu utambue, ya kuwa wewe umenituma, kisha umewapenda, kama ulivyonipenda mimi.
24
Baba, nataka hata wale, ulionipa, wawe pamoja nami papo hapo, nitakapokuwapo mimi, wapate kuuona utukufu wangu, ulionipa, kwa sababu umenipenda, ulimwengu ulipokuwa haujaumbwa bado.
25
Baba mwongofu, ulimwengu haukukutambua, lakini mimi nimekutambua, nao hao wametambua, ya kuwa wewe umenituma.
26
Nami nimewatambulisha Jina lako, na tena nitalitambulisha, kwamba upendo, wewe ulionipenda, uwakalie, nami niwemo mwao.
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21