bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Chronicles 10
1 Chronicles 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 11 →
1
Wafilisti walipopigana nao Waisiraeli, watu wa Isiraeli wakawakimbia Wafilisti kwa madonda waliyopigwa, wakaanguka, wakafa kule mlimani kwa Gilboa.
2
Wafilisti wakawafuata na kuandamana na Sauli na wanawe, Wafilisti wakawaua wana wa Sauli: Yonatani na Abinadabu na Malkisua.
3
Mapigano yakawa makali hapo, Sauli alipokuwa; wapiga mishale walipomwona, akaumizwa nao wapiga mishale.
4
Ndipo, Sauli alipomwambia mchukua mata yake: Uchomoe upanga wako, unichome nao, hao wasiotahiriwa wasije kunichezea vibaya! Mchukua mata yake alipokataa kwa kuogopa sana, Sauli akausimika upanga, akauangukia.
5
Mchukua mata yake alipoona, ya kuwa Sauli amekufa, naye akauangukia upanga wake, akafa.
6
Ndivyo, Sauli alivyokufa na wanawe watatu, nao wa mlango wake wote wakafa pamoja naye.
7
Watu wote wa Isiraeli waliokaa kule katika mbuga ya bondeni walipoona, ya kuwa wamekimbizwa, ya kuwa Sauli na wanawe wamekufa, wakaiacha miji yao wakakimbia nao; kisha Wafilisti wakaja, wakakaa humo.
8
Ikawa kesho yake, Wafilisti walipokuja kuwapambua waliouawa, wakamwona Sauli na wanawe, jinsi walivyokufa mlimani kwa Gilboa.
9
Wakampambua, wakakichukua kichwa chake na mata yake, wakatuma wajumbe kwenda po pote katika nchi ya Wafilisti kuyatangaza penye vinyago vyao, hata kwa watu.
10
Mata yake wakayaweka nyumbani mwa mungu wao, nacho kichwa chake wakakiangika kwa misumari nyumbani mwa Dagoni.
11
Watu wote wa Yabesi wa Gileadi walipoyasikia yote, Wafilisti waliyomfanyizia Sauli,
12
wakaondoka watu wote walioweza kupiga vita, wakauchukua mzoga wa Sauli, nayo mizoga ya wanawe, wakaipeleka Yabesi, wakaizika mifupa yao chini ya mkwaju kwao Yabesi, wakafunga mfungo siku saba.
13
Ndivyo, Sauli alivyokufa kwa kumvunjia Bwana maagano, aliyoyafanya naye, kwa kuwa hakulishika Neno la Bwana, tena kwa kuwa alitafuta mwaguaji aliyejua kukweza mizimu.
14
Kwa kuwa hakutaka kuongozwa na Bwana, akamwua, nao ufalme akauondoa kwake, akampa Dawidi, mwana wa Isai.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29