bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Chronicles 7
1 Chronicles 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 8 →
1
Nao wana wa Isakari: Tola na Pua na Yasubu na Simuroni, ni watu wanne.
2
Nao wana wa Tola: Uzi na Refaya na Yerieli na Yamai na Ibusamu na Samweli, hawa walikuwa vichwa vyao vya milango ya baba zao; wao wa Tola walikuwa mafundi wa vita wenye nguvu katika vizazi vyao, hesabu yao katika siku za Dawidi ilikuwa watu 22600.
3
Nao wana wa Uzi: Iziraya, nao wana wa Iziraya: Mikaeli na Obadia na Yoeli na Isia, wote pamoja ni wakuu watano.
4
Tena vizazi vya kwao vya milango ya baba zao vilikuwa vyenye vikosi vikubwa vya wapiga vita, watu 36000, kwani walikuwa wenye wanawake na watoto wengi.
5
Nao ndugu zao wa koo zote za Isakari walikuwa mafundi wa vita wenye nguvu, walioandikwa katika kitabu cha udugu, wote pamoja walikuwa watu 87000.
6
Wa Benyamini: Bela na Bekeri na Yediaeli, watu watatu.
7
Nao wana wa Bela: Esiboni na Uzi na Uzieli na Yerimoti na Iri, vichwa vitano vya milango ya baba zao, nao walikuwa mafundi wa vita wenye nguvu nyingi; walioandikwa katika kitabu cha udugu walikuwa watu 22034.
8
Wana wa Bekeri: Zemira na Yoasi na Eliezeri na Eliyoenai na Omuri na Yeremoti na Abia na Anatoti na Alemeti; hawa wote walikuwa wana wa Bekeri.
9
Nao vichwa vya milango ya baba zao walioandikwa katika kitabu cha udugu hivyo, walivyofuatana kuzaliwa, walikuwa mafundi wa vita wenye nguvu, watu 20200.
10
Nao wana wa Yediaeli: Bilihani, nao wana wa Bilihani: Yeusi na Benyamini na Ehudi na Kanaana na Zetani na Tarsisi na Ahisahari.
11
Hawa wote walikuwa wana wa Yediaeli, nao walikuwa vichwa vya milango ya baba zao na mafundi wa vita wenye nguvu nyingi, watu 17200 walioweza kutoka kwenda vitani kupigana.
12
Naye Supimu na Hupimu walikuwa wana wa Iri; tena Husimu na wana wa Aheri.
13
Wana wa Nafutali: Yasieli na Guni na Yeseri na Salumu, ndio wana wa Biliha.
14
Wana wa Manase: Asirieli, aliyemzaa suria yake wa Kishami, ndiye aliyemzaa naye Makiri, babake Gileadi.
15
Naye Makiri akawaoza Hupimu na Supimu, nalo jina la umbu lake ni Maka, nalo jina la mwanawe wa pili ni Selofuhadi, naye Selofuhadi alikuwa na wana wa kike tu.
16
Naye Maka, mkewe Makiri, akazaa mwana wa kiume, akamwita jina lake Peresi, nalo jina la ndugu yake lilikuwa Seresi, nao wanawe ni Ulamu na Rekemu.
17
Nao wana wa Ulamu: Bedani. Hawa ndio wana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase.
18
Umbu lake Hamoleketi akazaa Ishodi na Abiezeri na Mala.
19
Nao wana wa Semida: Ayani na Sekemu na Likihi na Aniamu.
20
Wana wa Efuraimu: Sutela, na mwanawe huyo Beredi, na mwanawe huyo Tahati, na mwanawe huyo Elada, na mwanawe huyo Tahati,
21
na mwanawe huyo Zabadi, na mwanawe huyo Sutela, tena Ezeri na Eladi. Lakini wana wa Gati waliozaliwa katika nchi ile wakawaua, kwa kuwa walishuka kuyachukua makundi yao.
22
Baba yao Efuraimu akawasikitikia siku nyingi, nao ndugu zake wakaja kumtuliza moyo.
23
Kisha akaingia kwake mkewe, akapata mimba, akazaa mwana wa kiume, akamwita jina lake Beria, kwa kuwa mambo mabaya yalikuwa nyumbani mwake.
24
Mwanawe wa kike ni Sera, ndiye aliyejenga Beti-Horoni wa chini na wa juu, tena Uzeni-Sera.
25
Mwanawe ni Refa na Resefu, na mwanawe huyo Tela, na mwanawe huyo Tahani,
26
na mwanawe huyo Ladani, na mwanawe huyo Amihudi, na mwanawe huyo Elisama,
27
na mwanawe huyo Nuni, na mwanawe huyo Yosua.
28
Nchi, waliyoichukua, iwe yao, walikokaa, ni Beteli na vijiji vyake, tena upande wa maawioni kwa jua Narani, na upande wa machweoni kwa jua Gezeri na vijiji vyake na Sekemu na vijiji vyake mpaka Gaza na vijiji vyake.
29
Kando ya mipaka ya wana wa Manase: Beti-Seani na vijiji vyake, Taanaki na vijiji vyake, Megido na vijiji vyake, Dori na vijiji vyake. Humo ndimo, wana wa Yosefu, mwana wa Isiraeli, walimokaa.
30
Wana wa Aseri: Imuna na Isiwa na Iswi na Beria, naye Sera aliyekuwa umbu lao.
31
Nao wana wa Beria: Heberi na Malkieli, huyu ndiye baba yao wa Birzaiti.
32
Heberi akamzaa Yafuleti na Someri na Hotamu, naye umbu lao Sua.
33
Nao wana wa Yafuleti: Pasaki na Bimuhali na Asiwati. Hawa ndio wana wa Yafuleti.
34
Nao wana wa Semeri: Ahi na Roga na Huba na Aramu.
35
Nao wana wa ndugu yake Helemu: Sofa na Imuna na Selesi na Amali.
36
Wana wa Sofa: Sua na Harneferi na Suali na Beri na Imura,
37
Beseri na Hodi na Sama na Silisa na Itirani na Bera.
38
Nao wana wa Yeteri: Yefune na Pisipa na Ara.
39
Nao wana wa Ula: Ara na Hanieli na Risia.
40
Hawa wote walikuwa wana wa Aseri, vichwa vya milango ya baba zao, mafundi wa vita wenye nguvu nyingi waliochaguliwa, wawe vichwa vya wakuu; wao walioandikwa katika kitabu cha udugu kuwa katika vikosi vya wapiga vita hesabu yao ilikuwa watu 26000.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29