bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Chronicles 17
1 Chronicles 17
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 18 →
1
Ikawa, Dawidi alipokaa nyumbani mwake, Dawidi akamwambia mfumbuaji Natani: Tazama, mimi ninakaa katika nyumba iliyojengwa kwa miangati, lakini Sanduku la Agano la Bwana linakaa chini ya mapazia tu.
2
Natani akamwambia Dawidi: Yote yaliyomo moyoni mwako yafanye! Kwani Mungu yuko pamoja na wewe.
3
Lakini usiku uleule neno la Mungu likamjia Natani kwamba:
4
Nenda, umwambie mtumishi wangu Dawidi: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Wewe hutanijengea nyumba ya kukaa.
5
Kwani sikukaa nyumbani tangu siku ile, nilipowaleta Waisiraeli huku milimani, mpaka siku hii ya leo, ila nilikuwa hemani huku, tena hamani huko, Kao langu likawa huku na huko.
6
Je? Hapo pote, nilipokwenda pamoja na Waisiraeli wote, nilimwambia hata mmoja wao waamuzi wa Waisiraeli, niliowaagiza kuwachunga walio ukoo wangu, na kumwuliza neno la kwamba: Mbona hamnijengei nyumba ya miangati?
7
kwa hiyo umwambie sasa mtumishi wangu Dawidi: Hivi ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema: Mimi nilikuchukua malishoni, ulipowafuata kondoo, uwe nwenye kuwatawala walio ukoo wangu wa Waisiraeli.
8
Nikawa pamoja na wewe po pote, ulipokwenda, nikawaangamiza adui zako wote mbele yako; nitakupatia jina lililo sawa na majina ya wakubwa walioko huku nchini.
9
Nao walio ukoo wangu wa Waisiraeli nitawapatia mahali, nitakapowapanda, wapate kukaa hapo pasipo kuhangaika tena, wala watu waovu wasiwakorofishe tena kama huko kwanza
10
tangu siku zile nilipowaagiza waamuzi, wawatawale walio ukoo wangu wa Waisiraeli; nitawanyenyekeza adui zako wote, tena ninakuambia sasa: Bwana atakujengea nyumba.
11
Itakuwa hapo, siku zako zitakapotimia, uende kulala pamoja na baba zako; ndipo, nitakapoinua nyuma yako mzao wako atakayetoka kwa wanao, niusimike ufalme wake.
12
Yeye ndiye atakayenijengea nyumba, nami nitakisimamisha kiti chake cha kifalme, kipate kuwapo kale na kale.
13
Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu, nao upole wangu sitauondoa kwake, kama nilivyouondoa kwao waliokuwa mbele yako.
14
Nitamsimamisha, awe nyumbani mwangu namo katika ufalme wangu kale na kale, nacho kiti chake cha kifalme kitakuwa kimesimamishwa kale na kale.
15
Natani akamwambia Dawidi haya maneno yote sawasawa, kama alivyoyaona yote alipoyachunguza.
16
Kisha mfalme Dawidi akaingia pake Bwana, akakaa hapo akisema: Bwana Mungu, mimi ni nani? Nao mlango wangu ni nini ukinileta, nifike hapa?
17
Lakini haya yakawa madogo machoni pako, Mungu, kwa hiyo umeyasema yatakayoujia mlango wa mtumishi wako katika siku zilizo mbali bado, ukanitazama kimtu na kunikweza, Bwana Mungu.
18
Dawidi akuambie nini tena kwa hivyo, unavyomheshimu mtumishi wako? Wewe unamjua mtumishi wako.
19
Bwana, kwa ajili ya mtumishi wako na kwa mapenzi ya moyo wako umeyafanya haya makubwa yote, uyajulishe haya matendo makubwa yote.
20
Bwana, hakuna anayefanana na wewe, hakuna Mungu, asipokuwa wewe, kwa hayo yote, tuliyoyasikia kwa masikio yetu.
21
Tena liko taifa moja tu huku nchini linalofanana na ukoo wako wa Waisiraeli? Hao ndio, Mungu aliokwenda kuwakomboa, wawe ukoo wake. Hapo ulijipatia Jina kwa matendo makubwa yaliyoogopesha, ulipowafukuza wamizimu mbele yao walio ukoo wako, uliowakomboa na kuwatoa Misri.
22
Ukaupa ukoo wako wa Waisiraeli kuwa ukoo wako kale na kale, wewe Bwana ukawa Mungu wao.
23
Sasa Bwana, neno hili, ulilolisema la mtumishi wako na la mlango wake, liwe limeshupaa kale na kale, ukifanya, kama ulivyosema.
24
Ndivyo, Jina lako litakavyokuwa limeshupaa kwa kuwa kubwa kale na kale kwamba: Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, ni Mungu wa Isiraeli kweli, tena ndivyo, mlango wa mtumishi wako Dawidi utakavyokuwa wenye nguvu mbele yako.
25
Kwani wewe, Mungu wangu, umelifunua sikio la mtumishi wako, asikie, ya kuwa utamjengea nyumba, kwa hiyo mtumishi wako ameiona njia hii ya kukutolea maombo haya.
26
Sasa Bwana, wewe ndiwe Mungu; hayo mema, uliyomwambia mtumishi wako, na yapate kuwa. Sasa na ikupendeze kuubariki mlango wa mtumishi wako, uwepo kale na kale usoni pako! Kwani unayoyabariki wewe, Bwana, huwa yamebarikiwa kale na kale.
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29