bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Chronicles 21
1 Chronicles 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 22 →
1
Satani akawainukia Waisiraeli akimponza Dawidi, awahesabu Waisiraeli.
2
Dawidi akamwambia Yoabu na wakuu wa watu: Nendeni, mwahesabu Waisiraeli toka Beri-Seba hata Dani! Kisha nileteeni habari, nipate kuzijua hesabu zao.
3
Yoabu akamjibu: Bwana na aendelee kuwaongeza watu wake vivyo hivyo mara mia! Bwana wangu mfalme, kumbe wao wote sio watumishi wa bwana wangu? Hayo bwana wangu anayatakia nini? Kuwakosesha Waisiraeli hivyo ni kwa nini?
4
Lakini neno la mfalme likapata nguvu, asimsikie Yoabu; ndipo, Yoabu alipotoka, akaenda po pote kwao Waisiraeli, kisha akaja Yerusalemu.
5
Hapo Yoabu akampasha Dawidi habari za jumla ya watu waliohesabiwa, wakawa Waisiraeli wote watu milioni moja na 100000 wenye kushika panga, nao Wayuda walikuwa watu 470000 wenye kushika panga.
6
Walawi na Wabenyamini hakuwahesabu, kwani hilo neno la mfalme lilikuwa limemchukiza Yoabu.
7
Neno hili likawa baya machoni pake Mungu, kwa hiyo akawapiga Waisiraeli.
8
Ndipo, Dawidi alipomwambia Mungu: Nimekosa sana kwa kulifanya neno hilo; sasa umwondolee mtumishi wako hizo manza, alizozikora! Kwani nimefanya kisichopasa kabisa.
9
Lakini Bwana akamwambia Gadi aliyekuwa mchunguzaji wake Dawidi kwamba:
10
Nenda kumwambia Dawidi kwamba: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Mimi ninakuwekea mambo matatu, ndimo uchague moja lao, nikufanyizie.
11
Gadi akaja kwa Dawidi, akamwambia: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Jipatie ulitakalo!
12
Unataka miaka mitatu ya njaa? au unataka kukimbizwa miezi mitatu machoni pao wakusongao, panga za adui zako zikikupata? au unataka, upanga wa Bwana na ugonjwa mbaya uuao upite katika nchi hii, malaika wa Bwana akifanya maovu katika mipaka yote ya Waisiraeli? Sasa tafuta, uone nitakayomjibu aliyenituma!
13
Dawidi akamwambia Gadi: Nimesongeka sana, lakini na nijitupe mkononi mwake Bwana, kwani huruma zake ni nyingi mno nisijitupe mikononi mwa watu.
14
Ndipo, Bwana alipowauguza Waisiraeli ugonjwa mbaya uuao, wakafa kwa Waisiraeli watu 70000.
15
Mungu akamtuma malaika wake namo Yerusalemu, afanye humo namo maovu yake; lakini Bwana alipoyaona hayo maovu, aliyoyafanya, akageuza moyo kwa ajili ya huo ubaya, akamwambia yule malaika aliyeangamiza: Sasa inatosha, ulegeze mkono wako! Naye yule malaika wa Bwana alikuwa akisimama penye kupuria ngano pa Myebusi Ornani.
16
Dawidi alipoyainua macho yake, akamwona malaika wa Bwana, akisimama kati ya nchi na ya mbingu, nao upanga uliochomolewa ulikuwa mkononi mwake kuuelekea Yerusalemu; ndipo, Dawidi na wazee waliokuwa wamevaa magunia walipoanguka kifudifudi,
17
Dawidi akamwambia Mungu: Kumbe si mimi niliyeagiza kuwahesabu watu? Mimi ndiye niliyekosa na kufanya mabaya sana. Lakini hawa kondoo wamefanya nini? Bwana Mungu wangu, mkono wako na unipige mimi na mlango wa baba yangu! Lakini hawa walio ukoo wako usiwaue!
18
Ndipo, malaika wa Bwana alipomwambia Gadi, amwambie Dawidi, Dawidi apande kutengeneza pa kumtambikia Bwana papo hapo penye kupuria ngano pa Myebusi Ornani.
19
Kwa hilo neno, Gadi alilolisema katika Jina la Bwana, Dawidi akapanda.
20
Ornani alipogeuka akamwona malaika; nao wanawe wanne waliokuwa naye walikuwa wamejificha, naye Ornani mwenyewe alikuwa akipura ngano.
21
Dawidi alipokuja kwake Ornani, huyu Ornani alikuwa akitazama; alipomwona Dawidi, akatoka hapo pa kupuria ngano, akamwangukia Dawidi usoni hapo chini.
22
Dawidi akamwambia Ornani: Nipe mahali hapa pa kupuria ngano, nipajenge pa kumtambikia Bwana! Nitakulipa fedha zote zipapasazo, nipe tu mahali hapa, huku kuuawa kwa watu kukomeshwe!
23
Ornani akamwambia Dawidi: Jichukulie tu! Bwana wangu mfalme na afanye, anayoyaona kuwa mema. Tazama, nakupa hawa ng'ombe kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, nayo haya magari nakupa kuwa kuni, nazo hizi ngano zote nakupa kuwa vilaji vya tambiko.
24
Mfalme Dawidi akamwambia ornani: Sivyo, kwani nitanunua kabisa na kulipa fedha zote zipapasazo, kwani sitazichukua mali zako za kumtolea Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, nisizozilipa.
25
Dawidi akampa Ornani kwa kupanunua mahali pale vipande vya dhahabu 600 vilivyokuwa kama shilingi 45000.
26
Kisha Dawidi akamjengea Bwana hapo mahali pa kumtambikia, akamtolea ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na vipaji vya tambiko vya kumshukuru, akamwita Bwana na kumwomba, naye akamwitikia akitoa moto mbinguni, upaangukie hapo pa kumtambikia kwa kumtolea ng'ombe za kuteketezwa nzima.
27
Ndipo, Bwana aliposema na yule malaika, naye akaurudisha upanga wake alani mwake.
28
Kwa kuwa Dawidi aliona wakati huo, ya kuwa Bwana amemwitikia hapo pa kupuria ngano pa Myebusi Ornani, huja kutambikia hapo.
29
Nalo kao la Bwana, Mose alilolitengeneza nyikani, pamoja na meza ya kumteketezea Bwana ng'ombe za tambiko siku zile lilikuwa kilimani kwa Gibeoni.
30
Lakini Dawidi hakuweza kwenda huko kumtafuta Mungu, kwa kuwa alikuwa ametishwa na upanga wa yule malaika wa Bwana.
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29