bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Chronicles 27
1 Chronicles 27
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 28 →
1
Hii ndiyo hesabu yao wana wa Isiraeli wakuu wa milango na wakuu wa maelfu na wa mamia nao wenye amri waliomtumikia mfalme katika mambo yote yayapasayo hayo mafungu, wakiingia, tena wakitoka mwezi kwa mwezi miezi yote ya mwaka, nalo fungu moja lilikuwa watu 24000.
2
Mkuu wa fungu la kwanza la mwezi wa kwanza alikuwa Yasobamu, mwana wa zabudieli; nalo fungu lake lilikuwa lenye watu 24000.
3
Alikuwa mmoja wao wana wa Peresi, akawa kichwa chao wakuu wote wa vikosi vya mwezi wa kwanza.
4
Naye mkuu wa fungu la mwezi wa pili alikuwa Mwahohi Dodai, naye mkubwa wa fungu lake alikuwa Mikloti; hata fungu lake lilikuwa lenye watu 24000.
5
Mkuu wa kikosi cha tatu cha mwezi wa tatu alikuwa Benaya, mwana wa mtambikaji Yoyada, yeye alikuwa kichwa, nalo fungu lake lilikuwa lenye watu 24000.
6
Huyu Benaya alikuwa fundi wa vita kwao wale thelathini, naye alikuwa mkuu wao wale thelathini. Aliyeliongoza fungu lake alikuwa mwanawe Amizabadi.
7
Mkuu wa nne wa mwezi wa nne alikuwa Asaheli, ndugu yake Yoabu, naye mwanawe Zebadia alimfuata. Fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.
8
Mkuu wa tano wa mwezi wa tano alikuwa mkuu Mwizirahi Samuhuti, fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.
9
Mkuu wa sita wa mwezi wa sita alikuwa Ira, mwana wa Ikesi wa Tekoa, fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.
10
Mkuu wa saba wa mwezi wa saba alikuwa Mpuloni Helesi aliyekuwa mmoja wao wana wa Efuraimu. Fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.
11
Mkuu wa nane wa mwezi wa nane alikuwa Sibekai wa Husa aliyekuwa mmoja wao Wazera. Fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.
12
Mkuu wa tisa wa mwezi wa tisa alikuwa Abiezeri wa Anatoti aliyekuwa mmoja wao Wabenyamini. Fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.
13
Mkuu wa kumi wa mwezi wa kumi alikuwa Maharai wa Netofa aliyekuwa mmoja wao Wazera. Fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.
14
Mkuu wa kumi na moja wa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaya wa Piratoni aliyekuwa mmoja wao wana wa Efuraimu. Fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.
15
Mkuu wa kumi na mbili wa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Heldai wa Netofa aliyekuwa wa mlango wa Otinieli. Fungu lake nalo lilikuwa lenye watu 24000.
16
Wakuu wa mashina ya Isiraeli walikuwa hawa: kwa Warubeni alikuwa mkubwa Eliezeri, mwana wa zikiri; kwa Wasimeoni Sefatia, mwana wa Maka;
17
kwa Lawi Hasabia, mwana wa Kemueli; kwa Haroni Sadoki;
18
kwa Yuda Elihu aliyekuwa mmoja wao ndugu zake Dawidi; kwa Isakari Omuri, mwana wa Mikaeli;
19
kwa Zebuluni Isimaya, mwana wa Obadia; kwa Nafutali Yerimoti, mwana wa Azirieli;
20
kwa wana wa Efuraimu Hosea, mwana wa Azazia; kwa nusu ya shina la Manase Yoeli, mwana wa Pedaya;
21
kwa nusu ya Manase kule Gileadi Ido, mwana wa Zakaria, tena kwa Benyamini Yasieli, mwana wa Abineri;
22
kwa Dani Azareli, mwana wa Yerohamu. Hawa walikuwa wakuu wa mashina ya Isiraeli.
23
Lakini wao waliokuwa wa miaka ishirini nao wasioipata bado Dawidi hakuwahesabu, kwani Bwana alisema, ya kuwa atawaongeza Waisiraeli, wawe wengi kama nyota za mbinguni.
24
Yoabu, mwana wa Seruya, alianza kuwahesabu, lakini hakumaliza, maana kwa ajili hii mapatilizo makali yaliwapata Waisiraeli. Kwa hiyo hesabu hiyo haikutiwa katika hesabu ya Mambo ya siku za mfalme Dawidi.
25
Mtunza vilimbiko vya mfalme alikuwa Azimaweti, mwana wa Adieli; naye mtunza vilimbiko vilivyokuwa mashambani na mijini na mizabibuni na ngomeni alikuwa Yonatani, mwana wa Uzia.
26
Msimamizi wa wafanya kazi za kulima mashambani alikuwa Eziri, mwana wa Kelubu.
27
Msimamizi wa mizabibu alikuwa Simei wa Rama, naye mtunza mvinyo zilizolimbikwa mizabibuni alikuwa Msifumi Zabudi.
28
Msimamizi wa michekele na wa mikuyu iliyokuwako katika nchi ya tambarare alikuwa Baali-Hanani wa Gaderi, naye mtunza mafuta yaliyolimbikwa alikuwa Yoasi.
29
Msimamizi wa ng'ombe waliolisha Saroni alikuwa Sitirai wa Saroni, naye msimamizi wa ng'ombe walioko mabondeni alikuwa Safati, mwana wa Adilai.
30
Msimamizi wa ngamia alikuwa Mwisimaeli Obili, naye msimamizi wa punda wake alikuwa Yehedia wa Meronoti.
31
Msimamizi wa mbuzi na kondoo alikuwa Mhagri Yazizi. Hawa wote walikuwa watunza mali za mfalme Dawidi.
32
Yonatani, mjomba wake Dawidi, alikuwa mwenye kula njama na mfalme, naye alikuwa mwenye utambuzi na mjuzi wa vitabu. Naye Yehieli, mwana wa Hakemoni, alikuwa mkuza wana wa mfalme.
33
Naye Ahitofeli alikuwa mwenye kula njama na mfalme, naye Mwarki Husai alikuwa rafiki yake mfalme.
34
Waliomfuata Ahitofeli walikuwa Yoyada, mwana wa Benaya, na Abiatari. Mkuu wa vikosi vya mfalme alikuwa Yoabu.
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 28 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29