bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Chronicles 6
1 Chronicles 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 7 →
1
Wana wa Lawi: Gersoni, Kehati na Merari.
2
Nao wana wa Kehati: Amuramu, Isihari na Heburoni na Uzieli.
3
Nao wana wa Amuramu: Haroni na Mose na Miriamu; nao wana wa Haroni: Nadabu na Abihu, Elazari na Itamari.
4
Elazari akamzaa Pinehasi, Pinehasi akamzaa Abisua.
5
Naye Abisua akamzaa Buki, naye Buki akamzaa Uzi.
6
Naye Uzi akamzaa Zeraya, naye Zeraya akamzaa Merayoti.
7
Merayoti akamzaa Amaria, naye Amaria akamzaa Ahitubu.
8
Naye Ahitubu akamzaa Sadoki, naye Sadoki akamzaa Ahimasi.
9
Naye Ahimasi akamzaa Azaria, naye Azaria akamzaa Yohana.
10
Naye Yohana akamzaa Azaria; huyu ndiye aliyekuwa mtambikaji katika Nyumba hiyo, Salomo aliyoijenga Yerusalemu.
11
Azaria akamzaa Amaria, naye Amaria akamzaa Ahitubu.
12
Naye Ahitubu akamzaa Sadoki, naye Sadoki akamzaa Salumu.
13
Naye Salumu akamzaa Hilkia, naye Hilkia akamzaa Azaria.
14
Naye Azaria akamzaa Seraya, naye Seraya akamzaa Yosadaki.
15
Naye Yosadaki ndiye aliyekwenda nao Wayuda na Wayerusalemu, Bwana alipowahamisha kwa mkono wa Nebukadinesari.
16
Wana wa Lawi: Gersomu, Kehati na Merari.
17
Nayo haya ndiyo majina ya wana wa Gersomu: Libuni na Simei.
18
Nao wana wa Kehati: Amuramu na Isihari na Heburoni na Uzieli.
19
Wana wa Merari: Mahali na Musi; huu ndio ukoo wao Walawi kwa milango ya baba zao.
20
Wagersomu: Mwanawe Libuni, mwanawe huyo Yahati, mwanawe huyo Zima,
21
mwanawe huyo Yoa, mwanawe huyo Ido, mwanawe huyo Zera, mwanawe huyo Yatiri.
22
Wana wa Kehati: Mwanawe Aminadabu, mwanawe huyo Kora, mwanawe huyo Asiri,
23
mwanawe huyo Elkana, mwanawe huyo Ebiasafu, mwanawe huyo Asiri,
24
mwanawe huyo Tahati, mwanawe huyo Urieli, mwanawe huyo Uzia, mwanawe huyo Sauli.
25
Nao wana wa Elkana: Amasai na Ahimoti;
26
mwanawe huyo Elkana, wanawe yeye Elkana: mwanawe Sofai, naye mwanawe huyo Nahati,
27
mwanawe huyo Eliabu, mwanawe huyo Yerohamu, mwanawe huyo Elkana, (mwanawe huyo Samweli).
28
Nao wana wa Samweli: Mzaliwa wa kwanza (Yoeli), tena wa pili Abia.
29
Wana wa Merari: Mahali, mwanawe huyo Libuni, mwanawe huyo Simei, mwanawe huyo Uza,
30
mwanawe huyo Simea, mwanawe huyo Hagia, mwanawe huyo Asaya.
31
Hawa ndio, Dawidi aliowaweka kwa ajili ya kuimba Nyumbani mwa Bwana, lile Sanduku lilipokuwa limekwisha kutua.
32
Nao walikuwa wakitumika mbele ya Kao la Hema la Mkutano kwa kuimba, mpaka Salomo alipoijenga Nyumba ya Bwana mle Yerusalemu, wakasimama katika kazi zao na kupokeana zamu kama desturi yao.
33
Nao hao ndio waliosimama katika kazi zao nao wana wao miongoni mwa wana wa Kehati: Mwimbishaji Hemani, mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli,
34
mwana wa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elieli, mwana wa Toa,
35
mwana wa Sufu, mwana wa Elkana, mwana wa Mahati, mwana wa Amasai,
36
mwana wa Elkana, mwana wa Yoeli, mwana wa Azaria, mwana wa Sefania,
37
mwana wa Tahati, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora,
38
mwana wa Isihari, mwana wa Kehati, mwana wa Lawi, mwana wa Isiraeli.
39
Naye ndugu yake Asafu alisimama kuumeni kwake; Asafu alikuwa mwana wa Berekia, mwana wa Simea,
40
mwana wa Mikaeli, mwana wa Basea, mwana wa Malkia,
41
mwana wa Etini, mwana wa Zera, mwana wa Adaya,
42
mwana wa Etani, mwana wa Zima, mwana wa Simei,
43
mwana wa Yahati, mwana wa Gersomu, mwana wa Lawi.
44
Nako kushotoni walisimama ndugu zao wana wa Merari: Etani, mwana wa Kisi, mwana wa Abudi, mwana wa Maluki,
45
mwana wa Hasabia, mwana wa Amasia, mwana wa Hilkia,
46
mwana wa Amusi, mwana wa Bani, mwana wa Semeri,
47
mwana wa Mahali, mwana wa Musi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi.
48
Ndugu zao Walawi wengine walikuwa wamepewa kazi zote za utumishi wa Kao la Nyumba ya Mungu.
49
Naye Haroni na wanawe walikuwa wakivukiza hapo pa kuteketezea ng'ombe za tambiko napo hapo pa kuvukizia, tena walizifanya kazi zote za hapo Patakatifu Penyewe, wawapatie Waisiraeli upozi wakifanya yote, kama Mose, mtumishi wa Mungu, alivyowaagiza.
50
Nao hawa ndio wana wa Aroni: Mwanawe Elazari, mwanawe huyo Pinehasi, mwanawe huyo Abisua,
51
mwanawe huyo Buki, mwanawe huyo Uzi, mwanawe huyo Zeraya,
52
mwanawe huyo Merayoti, mwanawe huyo Amaria, mwanawe huyo Ahitubu,
53
mwanawe huyo Sadoki, mwanawe huyo Ahimasi.
54
Nayo haya ndiyo makao yao, walikotua katika mipaka yao: miongoni mwao wana wa Haroni ukoo wao Wakehati walipatwa na kura ya kwanza,
55
kwa hiyo wakawapa Heburoni katika nchi ya Yuda pamoja na malisho yake yaliyouzunguka.
56
Lakini mashamba ya huo mji na vijiji vyake wakampa Kalebu, mwana wa Yefune.
57
Tena wakawapa wana wa Haroni miji ya kukimbilia ya Heburoni, tena Libuna pamoja na malisho yake na Yatiri na Estemoa pamoja na malisho yake
58
na Hileni pamoja na malisho yake na Debiri pamoja na malisho yake
59
na Asani pamoja na malisho yake na Beti-Semesi pamoja na malisho yake.
60
Tena katika shina la Benyamini Geba pamoja na malisho yake na Alemeti pamoja na malisho yake na Anatoti pamoja na malisho yake. Miji yao yote ilikuwa 13 kwa hesabu ya koo zao.
61
Nao wana wa Kehati waliosalia walipewa miji 10 kwa kupigiwa kura katika ukoo wa hilo shina (Efuraimu), tena katika nusu ya shina la nusu ya Manase.
62
Nao wana wa Gersomu walipewa miji 13, iwe ya ukoo wao katika shina la Isakari na katika shina la Aseri na katika shina la Nafutali na katika shina la Manase huko Basani.
63
Nao wana wa Merari walipewa kwa kupigiwa kura miji 12, iwe ya ukoo wao katika shina la Rubeni na katika shina la Gadi na katika shina la Zebuluni.
64
Ndivyo, wana wa Isiraeli walivyowapa Walawi hiyo miji pamoja na malisho yao.
65
Wakawapa kwa kuipigia kura ile miji, iliyotajwa majina yao katika shina la wana wa Yuda na katika shina la wana wa Simeoni na katika shina la wana wa Benyamini.
66
Nao wengine waliokuwa wa ukoo wa wana wa Kehati walipata miji katika shina la Efuraimu, iwe yao.
67
Wakawapa miji ya kukimbilia ya Sikemu pamoja na malisho yake milimani kwa Efuraimu, tena Gezeri pamoja na malisho yake
68
na Yokimamu pamoja na malisho yake na Beti-Horoni pamoja na malisho yake
69
na Ayaloni pamoja na malisho yake na Gati-Rimoni pamoja na malisho yake.
70
Tena katika nusu ya shina la Manase Aneri pamoja na malisho yake na Bileamu pamoja na malisho yake. Hii ilikuwa yao wengine wa ukoo wa wana wa Kehati waliosalia.
71
Wana wa Gersomu walipata katika ukoo wao wa nusu ya shina la Manase Golani ulioko Basani pamoja na malisho yake na Astaroti pamoja na malisho yake.
72
Tena katika shina la Isakari: Kedesi pamoja na malisho yake na Daberati pamoja na malisho yake
73
na Ramoti pamoja na malisho yake na Anemu pamoja na malisho yake.
74
Tena katika shina la Aseri: Masali pamoja na malisho yake na Abudoni pamoja na malisho yake
75
na Hukoki pamoja na malisho yake na Rehobu pamoja na malisho yake.
76
Tena katika shina la Nafutali: Kedesi wa Galili pamoja na malisho yake na Hamoni pamoja na malisho yake na Kiriataimu pamoja na malisho yake.
77
Wana wa Merari waliosalia walipata katika shina la Zebuluni: Rimoni pamoja na malisho yake na Tabori pamoja na malisho yake;
78
tena ng'ambo ya pili ya Yordani kuelekea Yeriko upande wa Yordani wa maawioni kwa jua katika shina la Rubeni: Beseri wa nyikani pamoja na malisho yake na Yasa pamoja na malisho yake
79
na Kedemoti pamoja na malisho yake na Mefati pamoja na malisho yake.
80
Tena katika shina la Gadi: Ramoti wa Gileadi pamoja na malisho yake na Mahanaimu pamoja na malisho yake
81
na Hesiboni pamoja na malisho yake na Yazeri pamoja na malisho yake.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29