bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Chronicles 22
1 Chronicles 22
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 23 →
1
Dawidi akasema: Hapa ndipo mahali pa nyumba ya Bwana Mungu, ndipo napo, Waisiraeli watakapoteketezea ng'ombe za tambiko.
2
Dawidi akaagiza, wageni walioko katika nchi ya Waisiraeli wakusanyike, akaweka mafundi wa kuchonga, wachonge mawe ya jengo ya kuijenga nyumba ya Mungu.
3
Tena Dawidi akaweka vyuma vingi vya misumari ya kutilia milango malangoni na vya mapapi na shaba nyingi zisizopimika.
4
Tena miti mingi ya miangati isiyohesabika, kwani Wasidoni na Watiro wakamletea Dawidi miti mingi ya miangati.
5
Maana Dawidi aliwaza moyoni kwamba: Mwanangu Salomo ujana wake ungali mchanga bado, nayo nyumba, Bwana atakayojengewa sharti iwe kubwa zaidi, ipate jina lenye utukufu katika nchi hizi zote, kwa hiyo nitamwandalia yaipasayo. Kwa sababu hii Dawidi akaandaa mengi, kabla hajafa.
6
Kisha akamwita mwanawe Salomo, akamwagiza kumjengea Bwana Mungu wa Isiraeli nyumba.
7
Hapo Dawidi akamwambia Salomo: Mwanangu, mimi nalitaka kwa moyo kulijengea Jina la Bwana Mungu wangu nyumba.
8
Lakini neno la Bwana likanijia la kwamba: Umemwaga damu nyingi kwa kupiga vita vikubwa, hutalijengea Jina langu nyumba, kwa kuwa umemwaga damu nyingi chini mbele yangu.
9
Tazama, kwako atazaliwa mwana, yeye atakuwa mtu wa kutulia, nami nitamtulizia adui zake wote pande zote, kwani jina lake ataitwa Salomo (Mtulivu), nami nitampatia utengemano na utulivu kwao Waisiraeli katika siku zake.
10
Yeye atalijengea Jina langu nyumba, naye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa baba yake, nami nitakishupaza kiti cha ufalme wake, kisimame kwao Waisiraeli kale na kale.
11
Sasa mwanangu, Bwana awe na wewe, ufanikiwe ukimjengea Bwana Mungu wako nyumba, kama alivyosema kwa ajili yako wewe.
12
Tena Bwana na akupe akili na utambuzi, atakapokuagiza kuwa mkuu wao Waisiraeli, uyaangalie Maonyo ya Bwana Mungu wako!
13
Ndivyo, utakavyofanikiwa ukiyaangalia maongozi na maamuzi, Bwana aliyamwagiza Mose ya kutumia kwao Waisiraeli. Jipe moyo, upate nguvu, usiogope, wala usiingiwe na vituko!
14
Tazama, ingawa nimekuwa mwenye masumbuko, nyumba ya Bwana nimeiwekea vipande vya dhahabu elfu mia, ndio shilingi kama milioni 22000 na vipande vya fedha milioni moja, ndio shilingi kama milioni 12000, tena shaba na vyuma visivyopimika kwa kuwa vingi; hata miti na mawe nimeweka, lakini haya utayaongeza.
15
Hata mafundi unao wengi, wachonga mawe na waashi na maseremala, tena kwa kila kazi wako wanaoijua vema.
16
Dhahabu na fedha na shaba na vyuma havihesabiki; haya! Inuka, kazifanye kazi hizo! Naye Bwana na awe na wewe!
17
Kisha Dawidi akawaagiza wakuu wote wa Waisiraeli kumsaidia mwanawe Salomo, akisema:
18
Je? Bwana Mungu wenu hakuwa nanyi akiwapatia kutulia pande zote? Kwani wote waliokaa katika nchi hii amewatia mkononi mwangu, nchi hii yote ikashurutishwa kumtii Bwana nao walio ukoo wake.
19
Sasa jipeni mioyo na kuzikaza roho zenu, mmtafute Bwana Mungu wenu! Inukeni, pajengeni Patakatifu pa Bwana Mungu, mlipeleke Sanduku la Agano la Bwana na vyombo vitakatifu vya Mungu katika nyumba hiyo itakayojengewa Jina la Bwana!
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 23 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29