bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Chronicles 4
1 Chronicles 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 5 →
1
Wana wa Yuda: Peresi, Hesironi na Karmi na Huri na sobali.
2
Naye Raya, mwana wa Sobali, akamzaa Yahati; naye Yahati akamzaa Ahumai na Lahadi. Huu ndio ukoo wao Wasorati.
3
Hawa ndio wana wa babake Etamu: Izireeli na Isima na Idibasi, nalo jina la umbu lao ni Hasilelponi.
4
Tena Penueli, babake Gedori, na Ezeri, babake Husa; hawa ndio wana wa Huri, mwana wa kwanza wa Efurata, babake Beti-Lehemu.
5
Naye Ashuri, babake Tekoa, alikuwa na wanawake wawili: Hela na Nara.
6
Nara akamzalia Ahuzamu na Heferi na Temuni na Ahastari. Hawa ndio wana wa Nara.
7
Nao wana wa Hela: Sereti, Isihari na Etinani.
8
Kosi akamzaa Anubu na Sobeba nao ukoo wa Ahariheli, mwana wa Harumu:
9
Yabesi alikuwa mwenye macheo kuliko ndugu zake, naye mama yake akamwita jina lake Yabesi kwamba: Nimemzaa kwa maumivu.
10
Naye Yabesi akamwomba Mungu wa Isiraeli kwamba: Laiti ungenibariki sana na kuipanua mipaka yangu, mkono wako ukawa pamoja nami, ukanizuilia mabaya, maumivu yasinipate! Mungu akayatimiza aliyoyaomba.
11
Naye Kelubu, ndugu yake Suha, akamzaa Mehiri, ndiye babake Estoni.
12
Naye Estoni akamzaa Beti-Rafa na Pasea na Tehina, babake Iri-Nahasi. Hawa ndio wana waume wa Reka.
13
Nao wana wa Kenazi: otinieli na Seraya; nao wana wa Otinieli: Hatati.
14
Naye Meonotai akamzaa Ofura. Naye Seraya akamzaa Yoabu, babake Ge-Harasimu (Bonde la Wahunzi), kwani walikuwa wahunzi.
15
Nao wana wa Kalebu, mwana wa Yefune: Iru, Ela na Namu; nao wana wa Ela: Kenazi.
16
Nao wana wa Yehaleleli: Zifu na Zifa, Tiria na Asareli.
17
Nao wana wa Ezera: Yeteri na Meredi na Eferi na Yaloni. (Bitia) akachukua mimba ya Miriamu na ya Samai na ya Isiba, babake Estemoa.
18
Naye mkewe wa Kiyuda wa Meredi akamzaa Yeredi, babake Gedori, na Heberi, babake Soko, na Yekutieli, babake Zanoa; lakini wale walikuwa wana wa Bitia, binti Farao, Meredi aliyemchukua, awe mkewe.
19
Nao wana wa mkewe Hodia, umbu lake Nahamu, babake Keila: Mgarmi na Estemoa wa Maka.
20
Nao wana wa Simoni: Amunoni na Rina, Beni-Hanani na Tiloni. Nao wana wa Isi: zoheti na Beni-Zoheti.
21
Wana wa Sela, mwana wa Yuda: Eri, babake Leka, na Lada, babake Maresa, nao ukoo wao waliojua kufuma bafta wa mlango wa Asibea;
22
tena Yokimu na wana waume wa Kozeba na Yoasi na Sarafu waliotawala Moabu, na Yasubi-Lehemu. Lakini maneno haya ni ya kale.
23
Hawa ndio wafinyanzi na wenyeji wa Netaimu na wa Gedera; walikaa huko kwa mfalme na kumfanyia kazi.
24
Wana wa Simeoni: Nemueli na Yamini, Yaribu, Zera, Sauli.
25
Mwanawe alikuwa Salumu, mwanaswe alikuwa Mibusamu, mwanawe alikuwa Misima.
26
Nao wana wa Misima: Mwanawe alikuwa Hamueli, mwanawe alikuwa Zakuri, mwanawe alikuwa Simei.
27
Naye Simei alikuwa mwenye wana wa kiume kumi na sita na wana wa kike sita, lakini ndugu zake hawakuwa na wana wengi, nao ukoo wao wote haukupata watu wengi kama wana wa Yuda.
28
Nao walikaa Beri-Seba na Molada na Hasari-Suali,
29
na Biliha na Esemu na Toladi,
30
na Betueli na Horma na Siklagi,
31
na Beti-Markaboti na Hasari-Susimu na Beti-Biri na Saraimu. Hii ndiyo miji yao, mpaka Dawidi aliposhika ufalme.
32
Navyo vijiji vyao vilikuwa Etamu na Aini, Rimoni na Tokeni na Asani, ni miji mitano.
33
Navyo vijiji vyao vyote vilivyoizunguka miji hii mpaka Baali vilikuwa makao yao, navyo vilikuwa na vitabu vyao vya udugu.
34
Tena: Mesobabu na Yamuleki na Yosa, mwana wa Amasiya,
35
na Yoeli na Yehu, mwana wa Yosibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli;
36
na Eliyoenai na Yakoba na Yesohaya na Asaya na Adieli na Yesimieli na Benaya,
37
na Ziza, mwana wa Sifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya, mwana wa Simuri, mwana wa Semaya.
38
Hawa waliotajwa kwa majina walikuwa wakuu katika ukoo wao, milango ya baba zao ilipokwisha kusambaa kwa wingi.
39
Wakaenda, hata waingie Gedori upande wa maawioni kwa jua wa huko bondeni kuwatafutia mbuzi na kondoo wao malisho.
40
Wakaona malisho mema ya kuwanonesha, nayo ile nchi ilikuwa pana pande zote, tena ilikuwa yenye utulivu na utengemano, kwani kale watu wa Hamu walikuwa wakikaa huko.
41
Wao walioandikwa majina hapo waliingia huko siku zake Hizikia, mfalme wa Yuda, wakayapiga mahema yao pamoja na Wameuni walioonekana huko, wakawatia mwiko wa kuwapo mpaka siku hii ya leo, wakakaa mahali pao, kwani malisho ya mbuzi na kondoo wao yalikuwapo.
42
Nao wengine wao waliokuwa wana wa Simeoni walikwenda milimani kwa Seiri, watu 500, nao wakuu wao walikuwa Pelatia na Naria na Refaya na Uzieli, wana wa Isi.
43
Wakayapiga masao ya Waamaleki walioponea huko, wakakaa huko mpaka siku hii ya leo.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29