bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Chronicles 16
1 Chronicles 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 17 →
1
Walipokwisha kuliingiza Sanduku la Mungu wakaliweka katikati ya lile hema, Dawidi alilolipigia, wakamtolea Mungu ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na za kumshukuru.
2
Dawidi alipokwisha kuzitoa hizo ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na za shukrani akawabariki watu katika Jina la Bwana.
3
Kisha akawagawia watu wote wa Isiraeli, waume kwa wake, kila mtu mkate wa sikukuu na kipande cha nyama na andazi la zabibu.
4
Akaweka Walawi wengine, watumike hapo penye Sanduku la Bwana na kuwakumbusha watu, Bwana Mungu wa Isiraeli aliyoyafanya, wamshukuru na kumtukuza,
5
ndio mkuu Asafu na Zakaria aliyekuwa mkuu wa pili, tena Yieli na Semiramoti na Yehieli na Matitia na Eliabu na Benaya na Obedi-Edomu na Yieli, wavishike vyombo vya kuimbia, mapango na mazeze, naye Asafu ayapige matoazi.
6
Nao watambikaji Benaya na Yahazieli wapige matarumbeta siku zote mbele ya Sanduku la Agano la Mungu.
7
Siku hiyo ndipo, Dawidi alipoagiza kwanza kumshukuru Bwana kwa msaada wa Asafu na wa ndugu zake:
8
Mshukuruni Bwana, nalo Jina lake litambikieni! Yajulisheni makabila ya watu matendo yake!
9
Mpigieni shangwe za kumwimbia! Mataajabu yake yote yatungieni tenzi!
10
Lishangilieni Jina lake lililo takatifu! Mioyo yao wamtafutao Bwana na ifurahi!
11
Mchungulieni Bwana nazo nguvu zake! Utafuteni uso wake siku zote!
12
Yakumbukeni mataajabu yake, aliyoyafanya. nayo maamuzi yake yashangazayo yakisemwa na kinywa chake!
13
Ninyi mlio uzao wake Isiraeli aliyemtumikia, nanyi wana wa Yakobo, yeye aliyemchagua!
14
Yeye Bwana ni Mungu wetu, nchi zote anaziamua.
15
Likumbukeni Agano lake kale na kale! Aliowaagiza kulishika Neno lake ni vizazi elfu.
16
Agano ni lile, alilomwekea Aburahamu, nacho kiapo ni kile, alichomwapia Isaka.
17
Mbele yake Yakobo naye akalisimamisha kuwa maongozi, Agano la kale na kale liwe kwake Isiraeli
18
kwamba: Wewe ndiwe, nitakayekupa nchi ya Kanaani. iwe fungu lenu, nililowapimia.
19
Vilikuwa hapo, walipokuwa kikundi cha watu wanaohesabika, maana kule walikuwa wachache tu, tena wageni.
20
Wakawaendea watu wa huko, taifa kwa taifa, walipotoka kwa mfalme mmoja, wakawajia wenziwe.
21
Lakini hakuna mtu, aliyempa ruhusa kuwakorofisha, hata wafalme akawapatiliza kwa ajili yao kwamba:
22
Niliowapaka mafuta msiwaguse tu, wala wafumbuaji wangu msiwafanyizie mabaya!
23
Mwimbieni Bwana, nchi zote! Utangazeni wokovu wake siku kwa siku!
24
Wasimulieni wamizimu utukufu wake, nako kwenye makabila yote ya watu mataajabu yake!
25
Kwani mkuu ni Bwana, apaswa na kutukuzwa sana, naye anaogopesha kuliko miungu yote.
26
Kwani miungu yote ya makabila ya watu ni ya bure tu, lakini Bwana ndiye aliyezifanya mbingu.
27
Ukuu na urembo uko mbele yake, uwezo na uchangamko upo hapo, alipo.
28
Ninyi mlio wa ukoo wa watu, mpeni Bwana yaliyo yake! Kwa kuwa ni mtukufu na mnguvu, mpeni Bwana yaliyo yake!
29
Kwa kuwa Jina lake ni tukufu, mpeni Bwana yaliyo yake! Chukueni vipaji vya tambiko, mje kumtokea! Mtambikieni Bwana na kuvaa mapambo yapasayo Patakatifu!
30
Mkimtokea, mastuko na yawaguie, ninyi wa nchi zote! Yeye ndiye aliyeishikiza nchi, isije kuyumbayumba!
31
Kwa hiyo mbingu na zifurahi, nchi nayo na ipige shangwe! Nako kwa wamizimu na waseme: Bwana ni mfalme!
32
Hata bahari nayo yote yajaayo ndani yake na yavume! Mashamba nayo yote yaliyomo na yapige vigelegele!
33
Itakuwa, nayo miti yote ya mwituni imshangilie Bwana, kwani ndiye atakayekuja kuihukumu nchi.
34
Mshukuruni Bwana, ya kuwa ni mwema! Ya kuwa upole wake ni wa kale na kale!
35
Semeni: Tuokoe, Mungu uliye wokovu wetu! Tukusanye na kutuponya kwenye wamizimu, tupate kulishukuru Jina lako takatifu, tuzidishe kukusifu na kukushangilia!
36
Na atukuzwe Bwana Mungu wa Isiraeli, tangu kale hata kale! Watu wote wakaitika: Amin! Haleluya!
37
Huko kwenye Sanduku la Agano la Bwana Dawidi akamwacha Asafu na ndugu zake, watumikie mbele ya hilo Sanduku pasipo kukoma wakifanya kazi ipasayo kila siku moja.
38
Tena akamweka Obedi-Edomu pamoja na ndugu zake 68, huyu Obedi-Edomu, mwana wa Yedutuni, na Hosa wawe walinda malango.
39
Naye mtambikaji Sadoki na watambikaji ndugu zake akawaacha mbele ya Kao la Bwana kule kilimani kwenye Gibeoni,
40
wamtolee Bwana mezani pa kutambikia pasipo kukoma asubuhi na jioni ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na kuyafanya yote yaliyoandikwa katika Maonyo ya Bwana, aliyoyaagiza, Waisiraeli wayafanye.
41
Pamoja nao walikuwako Hemani na Yedutuni nao wengine wote waliochaguliwa na kuandikwa majina, waimbe: Mshukuruni Bwana, ya kuwa upole wake ni wakale na kale!
42
Akina Hemani na Yedutuni waliokuwa nao, wakapewa matarumbeta na matoazi ya kuwapa wenye kuyapiga na vyombo vyote vya kuimbia nyimbo za Mungu. Nao wana wa Yedutuni wakalinda langoni.
43
Kisha watu wote wakaenda kila mtu nyumbani kwake, naye Dawidi akazunguka kuubariki mlango wake.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29