bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Chronicles 5
1 Chronicles 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 6 →
1
Rubeni, mwana wa kwanza wa Isiraeli, alikuwa kweli mzaliwa wake wa kwanza; lakini kwa kuwa aliyachafua malalo ya baba yake, uzaliwa wake wa kwanza walipewa wana wa Yosefu, mwana wa Isiraeli, ingawa hawakuandikiwa uzaliwa wa kwanza katika kitabu cha udugu.
2
Kweli Yuda alikuwa mwenye nguvu katika ndugu zake, naye mtawalaji akatolewa kwake, lakini huo uzaliwa wa kwanza ulikuwa wake Yosefu.
3
Nao wana wa Rubeni, mwana wa kwanza wa Isiraeli, walikuwa: Henoki na Palu, Hesironi na Karmi.
4
Wana wa Yoeli: Mwanawe Semaya, mwanawe huyo Gogi, mwanawe huyo Simei,
5
mwanawe huyo Mika, mwanawe huyo Raya, mwanawe huyo Baali,
6
mwanawe huyo Bera, ambaye Tilgati-Pilneseri, mfalme wa Asuri, alimteka na kumhamisha, maana alikuwa mkuu wa Rubeni.
7
Ndugu zake walioandikwa katika kitabu cha udugu wa koo zao hivyo, walivyofuatana kuzaliwa, mkuu ni Yieli, akafuata Zakaria,
8
tena Bela, mwana wa Azazi, mwana wa Sema, mwana wa Yoeli. Huyu Bela alikaa Aroeri mpaka Nebo na Baali-Meoni.
9
Upande wa maawioni kwa jua alikaa mpaka kufika katika nyika iliyoko kwenye mto wa Furati, kwani makundi yalikuwa mengi katika nchi ya Gileadi.
10
Tena katika siku za Sauli walipiga vita na watu wa Hagri; hao walipokwisha kuuawa kwa mikono yao, wakakaa katika mahema yao upande wote mzima wa maawioni kwa jua wa Gileadi.
11
Nao wana wa Gadi walikaa ng'ambo yao katika nchi ya Basani mpaka Salka.
12
Mkuu alikuwa Yoeli, naye wa pili Safamu, tena Yanai na Safati wa huko Basani.
13
Ndugu zao wa milango ya baba zao: Mikaeli na Mesulamu na Seba na Yorai na Yakani na Zia na Eberi, watu saba.
14
Hawa ndio wana wa Abihaili, mwana wa Huri, mwana wa Yaroa, mwana wa Gileadi, mwana wa Mikaeli, mwana wa Yesisai, mwana wa Yado, mwana wa Buzi.
15
Ahi, mwana wa Abudieli, mwana wa Guni, alikuwa mkuu wa milango ya baba zao.
16
Walikaa Gileadi na Basani na katika vijiji vyao vidogo na katika malisho yote ya Saroni, hata kwenye mipaka yao.
17
Hawa wote waliandikwa katika vitabu vya udugu katika siku za Yotamu, mfalme wa Yuda, na katika siku za Yeroboamu, mfalme wa Isiraeli.
18
Wana wa Rubeni na wa Gadi nao wa nusu ya shina la Manase, wao waliokuwa wenye nguvu, walioweza kushika ngao na panga, waliojua kuvuta pindi, waliofundishwa vita, walikuwa watu 44760; ndio waliotoka kwenda vitani,
19
wakapigana nao Wahagri nao Wayeturi nao Wanafisi nao Wanodabu.
20
Wakasaidiwa kuwashinda, nao Wahagri pamoja nao wote waliokuwa pamoja nao wakatiwa mikononi mwao, kwani walimlilia Mungu katika mapigano, naye akayasikia maombo yao, kwa kuwa walimtegemea.
21
Wakayateka makundi yao: ngamia 50000, mbuzi na kondoo 250000 na punda 2000 na watu 100000.
22
Kwani walioumizwa walianguka wengi, kwa kuwa vita hivyo vilikuwa vimetoka kwake Mungu, wakakaa mahali pao, mpaka walipotekwa na kuhamishwa.
23
Nao wana wa nusu ya shina la Manase walikaa katika nchi hiyo toka Basani mpaka Baali-Hermoni, tena mpaka Seniri na milimani kwa Hermoni, nao walikuwa wengi.
24
Hawa ndio wakuu wa milango ya baba zao. Eferi na Isi na Elieli na Azirieli na Yeremia na Hodawia na Yadieli, nao walikuwa mafundi wa vita wenye nguvu, watu wenye majina makuu, kwa hiyo walikuwa wakuu wa kweli wa milango ya baba zao.
25
Lakini walipomvunjia Mungu wa baba zao maagano na kufanya ugoni kwa kuifuata miungu ya makabila ya ile nchi, Mungu aliyoyaangamiza mbele yao,
26
ndipo, Mungu wa Isiraeli alipoiamsha roho ya Puli, mfalme wa Asuri, nayo roho yake Tilgati-Pilneseri, mfalme wa Asuri, akawateka na kuwahamisha Warubeni nao Wagadi nao wa nusu ya shina la Manase, akawapeleka Hala na Habori na Hara na mtoni kwa Gozani; ndiko, waliko hata siku hii ya leo.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29