bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
1 Chronicles 2
1 Chronicles 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 3 →
1
Wana wa Isiraeli ndio hawa: Rubeni, Simeoni, Lawi na Yuda, Isakari na Zebuluni,
2
Dani, Yosefu na Benyamini, Nafutali, Gadi na Aseri.
3
Wana wa Yuda: Eri na Onani na Sela; hawa watatu alizaliwa na Mkanaani binti Sua. Naye Eri, mwanawe wa kwanza wa Yuda, akawa mbaya machoni pa Bwana, kwa hiyo akamwua.
4
Naye mkwewe Tamari akamzalia Peresi na Zera. Hivyo wana wote wa Yuda walikuwa watano.
5
Wana wa Peresi ni Hesironi na Hamuli.
6
Nao wana wa Zera ni Zimuri na Etani na Hemani na Kalkoli na Dara, wao wote ni watano.
7
Nao wana wa Karmi ni Akari aliyewaponza Waisiraeli kwa kuuvunja mwiko wa kuchukua mali.
8
Nao wana wa Etani ni Azaria.
9
Nao wana wa Hesironi, aliozaliwa, ni Yerameli na Ramu na Kelubai.
10
Naye Ramu akamzaa Aminadabu, naye Aminadabu akamzaa Nasoni aliyekuwa mkuu wa wana wa Yuda.
11
Naye Nasoni akamzaa Salma, naye Salma akamzaa Boazi,
12
naye Boazi akamzaa Obedi, naye Obedi akamzaa Isai,
13
naye Isai akamzaa mwanawe wa kwanza Eliabu na wa pili Abinadabu na wa tatu Simea,
14
wa nne Netaneli, wa tano Radai,
15
wa sita Osemu, wa saba Dawidi.
16
Nao maumbu zao ni Seruya na Abigaili. Nao wana wa Seruya ni Abisai na Yoabu na Asa-Eli, hawa watatu.
17
Naye Abigaili akamzaa Amasa, naye babake Amasa ni Mwisimaeli Yeteri.
18
Naye Kalebu, mwana wa Hesironi, akazaa wana naye mkewe Azuba naye Yerioti; nao wanawe huyo ni hawa: Yeseri na Sobabu na Ardoni.
19
Azuba alipokufa, Kalebu akamchukua Efurati, naye akamzalia Huri.
20
Naye Huri akamzaa Uri, naye Uri akamzaa Besaleli.
21
Halafu Hesironi akaingia kwa binti Makiri, babake Gileadi; naye akamchukua alipokuwa mwenye miaka 60, akamzalia Segubu.
22
Naye Segubu akamzaa Yairi; huyu Yairi akawa mwenye miji 23 katika nchi ya Gileadi.
23
Lakini Wagesuri na Washami wakavichukua vijiji vya Yairi kwao, Kenati na vijiji vyake, vyote pamoja ni miji 60. Hawa wote ni wana wa Makiri, babake Gileadi.
24
Hesironi alipokwisha kufa mle Kalebu-Efurata, ndipo, Abia, mkewe Hesironi, alipomzalia Ashuri, babake Tekoa.
25
Wana wa Yerameli, mwanawe wa kwanza wa Hesironi, walikuwa: wa kwanza Ramu, tena Buna na Oreni na Osemu wa Ahia.
26
Yerameli akawa na mke mwingine, jina lake Atara, naye ni mamake Onamu.
27
Nao wana wa Ramu, mwanawe wa kwanza wa Yerameli, walikuwa: Masi na Yamini na Ekeri.
28
Nao wana wa Onamu walikuwa Samai na Yada; nao wana wa Samai ni Nadabu na Abisuri.
29
Nalo jina la mkewe Abisuri ni Abihaili, naye akamzalia Abani na Molidi.
30
Nao wana wa Nadabu ni Seledi na Apaimu; naye Seledi alipokufa hakuwa na wana.
31
Nao wana wa Apaimu: Isi; nao wana wa Isi: Sesani; nao wana wa Sesani: Alai.
32
Nao wana wa Yada, nduguye Samai: Yeteri na Yonatani; naye Yeteri alipokufa hakuwa na wana.
33
Nao wana wa Yonatani: Peleti na Zaza. Hawa walikuwa wana wa Yerameli.
34
Sesani hakuwa na wana wa kiume, ila wa kike tu. Naye Sesani alikuwa na mtumwa wa Misri, jina lake Yariha.
35
Sesani akamwoza huyo mtumwa wake Yariha mwanawe wa kike, akamzalia Atai.
36
Naye Atai akamzaa Natani, naye Natani akamzaa Zabadi.
37
Naye Zabadi akamzaa Efulali, naye Efulali akamzaa Obedi.
38
Naye Obedi akamzaa Yehu, naye Yehu akamzaa Azaria.
39
Naye Azaria akamzaa Helesi, naye Helesi akamzaa Elasa.
40
Naye Elasa akamzaa Sisimai, naye Sisimai akamzaa salumu.
41
Naye Salumu akamzaa Yekamia, naye Yekamia akamzaa Elisama.
42
Nao wana wa Kalebu, nduguye Yarameli: Mwanawe wa kwanza Mesa aliye babake Zifu, tena wana wa Maresa aliye babake Heburoni.
43
Nao wana wa Heburoni: Kora na Tapua na Rekemu na Sema.
44
Naye Sema akamzaa Rahamu, babake Yorkamu. Naye Rekemu akamzaa Samai.
45
Naye mwana wa Samai ni Maoni; naye Maoni ni babake Beti-Suri.
46
Naye Efa, suria ya Kalebu, akamzaa Harani na Mosa na Gazezi; naye Harani akamzaa Gazezi.
47
Nao wana wa Yadai: Regemu na Yotamu na Gesani na Peleti na Efa na safu.
48
Maka, Suria ya Kalebu, akamzaa Seberi na Tirihana.
49
Tena akamzaa Safu, babake Madimana, na Sewa, babake Makibena, na babake Gibea; naye Akisa ni mwana wa kike wa Kalebu.
50
Hawa walikuwa wana wa Kalebu. Wana wa Huri aliyekuwa mwana wa kwanza wa Efurata ni Sobali, babake Kiriati-Yearimu,
51
na Salma, babake Beti-Lehemu, na Harefu, babake Beti-Gaderi.
52
Nao wana wa sobali, babake Kiriati-Yearimu, walikuwa Haroe, ndio nusu yao wa Menuhoti.
53
Nazo koo za Kiriati-Yearimu ndio Waitiri na Waputi na Wasumati na Wamisirai; kwao hao ndiko, walikotoka Wasorati na Waestauli.
54
Wana wa Salma: Beti-Lehemu na Wanetofati, Atiroti, Beti-Yoabu nayo nusu yao Wamanahati, ndio wasori;
55
nazo koo za waandishi waliokaa Yabesi ndio Watirati, Wasimati, Wasukati. Hawa ndio Wakini waliotoka kwa Hamati, baba yao mlango wa Rekabu.
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29