bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Psalms 18
Psalms 18
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 67
Chapter 68
Chapter 69
Chapter 70
Chapter 71
Chapter 72
Chapter 73
Chapter 74
Chapter 75
Chapter 76
Chapter 77
Chapter 78
Chapter 79
Chapter 80
Chapter 81
Chapter 82
Chapter 83
Chapter 84
Chapter 85
Chapter 86
Chapter 87
Chapter 88
Chapter 89
Chapter 90
Chapter 91
Chapter 92
Chapter 93
Chapter 94
Chapter 95
Chapter 96
Chapter 97
Chapter 98
Chapter 99
Chapter 100
Chapter 101
Chapter 102
Chapter 103
Chapter 104
Chapter 105
Chapter 106
Chapter 107
Chapter 108
Chapter 109
Chapter 110
Chapter 111
Chapter 112
Chapter 113
Chapter 114
Chapter 115
Chapter 116
Chapter 117
Chapter 118
Chapter 119
Chapter 120
Chapter 121
Chapter 122
Chapter 123
Chapter 124
Chapter 125
Chapter 126
Chapter 127
Chapter 128
Chapter 129
Chapter 130
Chapter 131
Chapter 132
Chapter 133
Chapter 134
Chapter 135
Chapter 136
Chapter 137
Chapter 138
Chapter 139
Chapter 140
Chapter 141
Chapter 142
Chapter 143
Chapter 144
Chapter 145
Chapter 146
Chapter 147
Chapter 148
Chapter 149
Chapter 150
Chapter 19 →
1
Nakupenda kwa moyo, Bwana, uliye nguvu yangu.
2
Bwana ni ngome yangu na boma langu, tena ni mponya wangu, ni Mungu aliye mwamba wangu, kwa hiyo ninamjetea; ni ngao yangu na pembe ya kunipatia wokovu, tena ni kingo langu.
3
Bwana atukuzwaye ndiye, ninayemwitia; ndipo, ninapookolewa mikononi mwao walio adui zangu.
4
Kamba ziuazo zilikuwa zimeniasamia, nayo majito yaangamizayo yalinistusha;
5
kamba zivutiazo kuzimuni zilikuwa zimenizunguka, nayo mafungo yauayo yalikuwa mbele yangu.
6
Hapo niliposongeka nalimwita Bwana, yeye aliye Mungu wangu nikamlalamikia, akaisikia sauti yangu Jumbani mwake, malalamiko yangu ya usoni pake yakamwingia masikioni mwake.
7
Nchi ikatukutika na kutetemeka, nayo misingi ya milima ikatikisika kwa kutukuswa, kwani aliitolea makali yake yenye moto.
8
Moshi ukapanda puani mwake, moto ulao ukatoka, kinywani mwake, makaa ya moto yakamulikamulika mbele yake.
9
Akatanda mbingu ya kushukiapo, mawingu meusi yakawa chini ya miguu yake.
10
Akapanda gari, nalo likarushwa, likakimbizwa mbiombio mabawani mwa upepo.
11
Akatumia giza kuwa ficho lake, limfunike pande zote likiwa kao lake; ndio mawingu meusi yenye mvua kali.
12
Kwa nguvu ya kumulika mbele yake mawingu yakatutumka, mvua ya mawe ikanyesha pamoja na kupiga umeme.
13
Bwana akapiga ngurumo kule mbinguni, Alioko huko juu akaivumisha sauti yake, mvua ya mawe ikanyesha pamoja na kupiga umeme.
14
Alipoipiga mishale yake, akawatawanya, ngurumo zilipozidi kuwa nyingi, wakapigwa bumbuazi.
15
Ndipo, ilipoonekana mikondo ya maji, nayo misingi ya nchi ikafunuliwa kwa nguvu ya makaripio ya kwako, Bwana, na kwa ukali wa pumzi ya pua yako.
16
Akakunjua mkono toka juu, akanikamata, mle mlimo na maji mengi akanichopoa.
17
Akaniponya mikononi mwa adui yangu mwenye nguvu, namo mwao walionichukia kwa kuwa na uwezo kuliko mimi.
18
Walikuwa wamenijia mbele ile siku, nilipokuwa nimeshindwa, lakini Bwana akanijia kuwa shikizo.
19
Akanitoa kwao, akanikalisha palipo papana; ndivyo, alivyoniopoa kwa kupendezwa nami.
20
Yaupasayo wongofu wangu Bwana alinipa, akanipatia tena yaupasayo ung'avu wa mikono yangu.
21
Kwani naliziangalia njia zake Bwana, nisifanye kilicho kiovu mbele yake Mungu wangu.
22
Kwani maamuzi yake yote yako mbele yangu, nayo maongozi yake sikuyaacha, nisiyafuate.
23
Nikawa naye pasipo kuonywa, nikajiangalia, nisimkosee.
24
Bwana akanipatia tena yaupasayo wongofu wangu, kwa kuwa mikono yangu ilikuwa imeng'aa machoni pake.
25
Wewe humwia mpole aliye mpole, naye aliye mkweli wote nawe humwia mkweli wote.
26
Wewe humwia mng'avu aliye mng'avu, lakini aliye mpotovu nawe humpotokea.
27
Kwani walio wanyonge wewe huwaokoa, lakini macho yajivunayo huyanyenyekeza.
28
Kwani wewe ndiye anayeiwasha taa yangu, wewe Bwana, Mungu wangu, huliangaza nalo giza langu.
29
Kwani nitashambulia vikosi vizima kwa nguvu yako, kwa nguvu ya Mungu wangu narukia napo ukutani.
30
Njia yake Mungu haipindiki, Neno lake Bwana limeng'azwa. Yeye ni ngao yao wote wamkimbiliao.
31
Kwani yuko nani aliye Mungu, asipokuwa Bwana? Tena yuko nani aliye mwamba, asipokuwa Mungu wetu?
32
Ni yeye Mungu aliyenivika nguvu, njia yangu huitengeneza, iwe imenyoka kabisa.
33
Hunipatia miguu ikimbiayo kama ya kulungu, anisimamishe kwangu vilimani juu.
34
Huifundisha mikono yangu kupiga vita, mpaka mikono yangu iweze kupinda hata uta wa shaba.
35
Hunipa ngao ya kuniokoa, kuumeni kwako hunishikiza, napo hapo, unaponinyenyekeza, hunikuza.
36
Huipanulia miguu yangu, ipate pa kupitia, viwiko vyangu vya miguu visiteleze.
37
Nitawakimbiza adui zangu, mpaka niwakamate; sitarudi, nisipokwisha kuwamaliza.
38
Nitawaponda, wasiweze kuinuka tena. Sharti waanguke miguuni pangu.
39
Hunivika nguvu ya kupiga vita, huwalaza chini yangu wao waniinukiao.
40
Hunipa adui zangu, niwaone migongo, nipate kuwanyamazisha wachukivu wangu.
41
Hakuna mwokozi, wanapolalamika, wanapomwitia Bwana, hawaitikii.
42
Nitawaponda, mpaka wabunguke kama mavumbi upeponi, niwazoe kama mataka yaliyoko viwanjani.
43
Kwenye magomvi ya watu ulinitoa, ukanipa kuwa kichwa chao wao wamizimu, watu, ambao nilikuwa siwajui, wanitumikie.
44
Masikio yao yanaponisikia, hunitii, nao watokao mbali hunipongeza.
45
Hao watokao mbali walikuwa wamenyauka, walipotoka mabomani kwao na kutetemeka.
46
Bwana Mwenye uzima ni mwamba wangu upasao kusifiwa, yeye Mungu aliyeniokoa sharti atukuke!
47
Mungu ndiye aliyenipatia malipizi na kuteka makabila ya watu, wanitii.
48
Wewe ndiwe uliyeniokoa mikononi mwao walio adui zangu, kwao waniinukiao ukaniweka kuwa mkuu wao, kwao walionikorofisha ukaniponya.
49
Kwa hiyo nitakushukuru, Bwana, kwenye wamizimu, nalo Jina lako na niliimbie.
50
Mfalme wake alimpatia wokovu mwingi, aliyempaka mafuta humfanyizia yenye upole; huyo ni Dawidi naye aliye wa uzao wake kale na kale.
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 67
Chapter 68
Chapter 69
Chapter 70
Chapter 71
Chapter 72
Chapter 73
Chapter 74
Chapter 75
Chapter 76
Chapter 77
Chapter 78
Chapter 79
Chapter 80
Chapter 81
Chapter 82
Chapter 83
Chapter 84
Chapter 85
Chapter 86
Chapter 87
Chapter 88
Chapter 89
Chapter 90
Chapter 91
Chapter 92
Chapter 93
Chapter 94
Chapter 95
Chapter 96
Chapter 97
Chapter 98
Chapter 99
Chapter 100
Chapter 101
Chapter 102
Chapter 103
Chapter 104
Chapter 105
Chapter 106
Chapter 107
Chapter 108
Chapter 109
Chapter 110
Chapter 111
Chapter 112
Chapter 113
Chapter 114
Chapter 115
Chapter 116
Chapter 117
Chapter 118
Chapter 119
Chapter 120
Chapter 121
Chapter 122
Chapter 123
Chapter 124
Chapter 125
Chapter 126
Chapter 127
Chapter 128
Chapter 129
Chapter 130
Chapter 131
Chapter 132
Chapter 133
Chapter 134
Chapter 135
Chapter 136
Chapter 137
Chapter 138
Chapter 139
Chapter 140
Chapter 141
Chapter 142
Chapter 143
Chapter 144
Chapter 145
Chapter 146
Chapter 147
Chapter 148
Chapter 149
Chapter 150
Chapter 19 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66
67
68
69
70
71
72
73
74
75
76
77
78
79
80
81
82
83
84
85
86
87
88
89
90
91
92
93
94
95
96
97
98
99
100
101
102
103
104
105
106
107
108
109
110
111
112
113
114
115
116
117
118
119
120
121
122
123
124
125
126
127
128
129
130
131
132
133
134
135
136
137
138
139
140
141
142
143
144
145
146
147
148
149
150