bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Psalms 68
Psalms 68
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 67
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 67
Chapter 68
Chapter 69
Chapter 70
Chapter 71
Chapter 72
Chapter 73
Chapter 74
Chapter 75
Chapter 76
Chapter 77
Chapter 78
Chapter 79
Chapter 80
Chapter 81
Chapter 82
Chapter 83
Chapter 84
Chapter 85
Chapter 86
Chapter 87
Chapter 88
Chapter 89
Chapter 90
Chapter 91
Chapter 92
Chapter 93
Chapter 94
Chapter 95
Chapter 96
Chapter 97
Chapter 98
Chapter 99
Chapter 100
Chapter 101
Chapter 102
Chapter 103
Chapter 104
Chapter 105
Chapter 106
Chapter 107
Chapter 108
Chapter 109
Chapter 110
Chapter 111
Chapter 112
Chapter 113
Chapter 114
Chapter 115
Chapter 116
Chapter 117
Chapter 118
Chapter 119
Chapter 120
Chapter 121
Chapter 122
Chapter 123
Chapter 124
Chapter 125
Chapter 126
Chapter 127
Chapter 128
Chapter 129
Chapter 130
Chapter 131
Chapter 132
Chapter 133
Chapter 134
Chapter 135
Chapter 136
Chapter 137
Chapter 138
Chapter 139
Chapter 140
Chapter 141
Chapter 142
Chapter 143
Chapter 144
Chapter 145
Chapter 146
Chapter 147
Chapter 148
Chapter 149
Chapter 150
Chapter 69 →
1
Mungu akiinuka, hutawanyika walio adui zake, nao wamchukiao hukimbia machoni pake!
2
Kama moshi unavyopeperuka, ndivyo, wanavyopeperuka; kama nta inavyoyeyuka motoni, ndivyo, wanavyoangamia usoni pake Mungu wao wasiomcha.
3
Lakini waongofu hufurahi na kushangilia kwa kuchangamka na kuona furaha mbele ya Mungu.
4
Mwimbieni Mungu, nalo Jina lake lishangilieni! Mtengenezeeni njia apitaye nyikani! Bwana ni Jina lake, mpigieni vigelegele!
5
Ni baba yao wafiwao na wazazi, nao wajane huwaamulia, ni Mungu akaaye pake, napo ni patakatifu.
6
Ni Mungu apaye wakiwa nyumba za kukaa, hutoa wafungwa kifungoni, nao wafanikiwe, lakini kwao wabishi, watakakokaa, ndiko kukavu.
7
Mungu, hapo, ulipotoka kuwatangulia wao walio ukoo wako, napo hapo, ulipokwenda kukanyaga kwenye jangwa,
8
ndipo, nchi ilipotetemeka, nazo mbingu zikanyesha maji, Mungu huyu alipotokea kule Sinai, alipotokea yeye Mungu aliye Mungu wao Waisiraeli.
9
Mvua ifurikayo ukiinyesha, Mungu, ilikuwa kila mara, fungu lako lilipotaka kuzimia; ndivyo, wewe ulivyolishikiza.
10
Walio kundi lako wakapata pa kukaa, nao wanyonge ukawashikiza, Mungu, kwa wema wako.
11
Wenye kulitangaza neno, alilolitoa bwana, ni kikosi kikubwa.
12
Wafalme wa vikosi watakimbia, watakimbia kweli, nao wanawake wenye nyumba watagawanya mateka.
13
Hapo, mnapolala kambini, yapo yanayomerimeta, yanafanana na mabawa ya kwenzi yang'aayo kama fedha, nayo manyoya yake humetuka kama dhahabu.
14
Mwenyezi alipowatawanya wafalme wale, mara kuling'aa kama theluji kulikokuwa na giza kuu.
15
Mlima wake Mungu ni mlima wa Basani, ule mlima wa Basani ulio wenye vilima huko kileleni.
16
Ninyi milima yenye vilima kileleni juu, sababu gani mnautazama kwa kijicho mlima ule Mungu alioupenda, akae pale? Kweli Bwana atakaa pale kale na kale
17
Magari yake Mungu ni maelfu na maelfu, hayahesabiki, Bwana anayo kule Sinai kwenye Patakatifu pake.
18
Ulipopaa juu, uliteka mateka, nako kwa watu ukayapokea waliyokupa; hata wabishi hawana budi kukaa kwake Bwana Mungu.
19
Bwana na atukuzwe siku kwa siku! Mungu hututwika mzigo, lakini hutusaidia kuuchukua.
20
Mungu, tuliye naye, ndiye Mungu aokoaye, mwenye njia za kutoka nako kufani ni Mungu Bwana.
21
Lakini vichwa vyao wachukivu wake Mungu ataviponda, nazo tosi zao wafulizao kukora manza zitachujuka.
22
Bwana alisema: Nitawatoa kule Basani, niwarudishe, nitawatoa namo vilindini mwa bahari, niwarudishe.
23
Ndipo, utakapoiogesha miguu yako katika damu, nazo ndimi za mbwa wako zitapata mafungu yao kwa adui zako.
24
Watu huwatazama wanaokuendea, Mungu, wakimwendea patakatifu aliye Mungu wangu hata mfalme wangu.
25
Waimbaji wanakwenda mbele, wapiga mazeze huwafuata, katikati ni wanawali wapigao patu.
26
Mnapokusanyika mtukuzeni Mungu Bwana, ninyi mnywao maji kisimani kwao Waisiraeli!
27
Wako wa Benyamini aliye mdogo, tena huwatawala, wako wakuu wa Yuda walio vikosi vizima, wako wakuu wa Zebuluni, nao wa Nafutali!
28
Mungu wako ameviagiza vitakavyokupa nguvu; Mungu, ufulize kuyatia nguvu uliyotufanyizia!
29
Kwa ajili ya Nyumba yako iliyo ya kutambika sharti wafalme wakupelekee matunzo huko Yerusalemu.
30
karipia nyama wakaao bwawani! ndio wakorofi wote, huwa ng'ombe wakali wanaowakanyaga ndama, kwani ni fedha tu, wanazozitamani. Nayo makabila ya watu wapendao vita yatapanye kabisa!
31
Ndipo, wakuu wa Misri watakapotokea, nao watu weusi, ndio watakaoviinua mikono yao kumwelekea Mungu.
32
Mwimbieni Mungu, ninyi wafalme wa nchi, pamoja wa watu! Mshangilieni aliye Bwana!
33
Ni yeye akaliaye mbingu zilizoko kule juu, nazo ni za kale, ni yeye avumishaye sauti yake, ikinguruma na nguvu.
34
Mkuzeni Mungu kuwa mwenye nguvu! Waisiraeli ndio, uliowatokea utukufu wake, nguvu zake ziko juu mawinguni.
35
Mungu, unaogopesha toka Patakatifu pako, Mungu wa Isiraeli; yeye ndiye atakayeupa ukoo wake nguvu za kushupaa. Na atukuzwe yeye Mungu!
← Chapter 67
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 41
Chapter 42
Chapter 43
Chapter 44
Chapter 45
Chapter 46
Chapter 47
Chapter 48
Chapter 49
Chapter 50
Chapter 51
Chapter 52
Chapter 53
Chapter 54
Chapter 55
Chapter 56
Chapter 57
Chapter 58
Chapter 59
Chapter 60
Chapter 61
Chapter 62
Chapter 63
Chapter 64
Chapter 65
Chapter 66
Chapter 67
Chapter 68
Chapter 69
Chapter 70
Chapter 71
Chapter 72
Chapter 73
Chapter 74
Chapter 75
Chapter 76
Chapter 77
Chapter 78
Chapter 79
Chapter 80
Chapter 81
Chapter 82
Chapter 83
Chapter 84
Chapter 85
Chapter 86
Chapter 87
Chapter 88
Chapter 89
Chapter 90
Chapter 91
Chapter 92
Chapter 93
Chapter 94
Chapter 95
Chapter 96
Chapter 97
Chapter 98
Chapter 99
Chapter 100
Chapter 101
Chapter 102
Chapter 103
Chapter 104
Chapter 105
Chapter 106
Chapter 107
Chapter 108
Chapter 109
Chapter 110
Chapter 111
Chapter 112
Chapter 113
Chapter 114
Chapter 115
Chapter 116
Chapter 117
Chapter 118
Chapter 119
Chapter 120
Chapter 121
Chapter 122
Chapter 123
Chapter 124
Chapter 125
Chapter 126
Chapter 127
Chapter 128
Chapter 129
Chapter 130
Chapter 131
Chapter 132
Chapter 133
Chapter 134
Chapter 135
Chapter 136
Chapter 137
Chapter 138
Chapter 139
Chapter 140
Chapter 141
Chapter 142
Chapter 143
Chapter 144
Chapter 145
Chapter 146
Chapter 147
Chapter 148
Chapter 149
Chapter 150
Chapter 69 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40
41
42
43
44
45
46
47
48
49
50
51
52
53
54
55
56
57
58
59
60
61
62
63
64
65
66
67
68
69
70
71
72
73
74
75
76
77
78
79
80
81
82
83
84
85
86
87
88
89
90
91
92
93
94
95
96
97
98
99
100
101
102
103
104
105
106
107
108
109
110
111
112
113
114
115
116
117
118
119
120
121
122
123
124
125
126
127
128
129
130
131
132
133
134
135
136
137
138
139
140
141
142
143
144
145
146
147
148
149
150