bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 1
Luke 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 2 →
1
Wengi walijaribu kuandika masimulio ya mambo yale yaliyotimilika kwetu.
2
Waliyafuatafuata yale waliyoambiwa na wenye kuyaona yote kwa macho yao, yalivyokuwa tangu mwanzo, kwani walikuwa wamelitumikia lile Neno.
3
Sasa nami nimeyafuata na kuyachungua yote mpaka hapo, yalipoanzia, nikaona, inafaa, nikuandikie sawasawa, kama yalivyofuatana, mwenzangu Teofilo,
4
upate kutambua, ya kuwa mambo yale uliyofundishwa ni ya kweli.
5
Siku zile, Herode alipokuwa mfalme wa Wayuda, palikuwa na mtambikaji wa chama cha Abia, jina lake Zakaria, naye mkewe alikuwa na wana wa Haroni, jina lake Elisabeti.
6
Wote wawili walikuwa waongofu machoni pa Mungu, wakaendelea na kuyashika maagizo na maongozi yote ya Bwana, watu wasione la kuwaonya.
7
Lakini walikuwa hawana mtoto, kwani Elisabeti alikuwa mgumba, nayo miaka yao wote wawili ilikuwa mingi.
8
Chama chake kilipofikiwa na zamu, akaenda kufanya kazi yake ya utambikaji mbele ya Mungu;
9
kwa desturi yao ya utambikaji yeye akapata kuvukiza, akaingia katika Jumba la Bwana.
10
Nalo kundi lote la watu wengi lilikuwa nje, wakiombea saa ileile ya kuvukiza.
11
Malaika wa Bwana akamtokea akisimama mezani pa kuvukizia kuumeni kwake.
12
Zakaria alipomwona akahangaika, woga ukamguia;
13
lakini malaika akamwambia: Usiogope, Zakaria! Kwani ombo lako limesikiwa: mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, nawe utamwita jina lake Yohana.
14
Wewe utafurahi na kushangilia, hata wengine wengi watakufurahia kuzaliwa kwake.
15
Kwani atakuwa mkubwa machoni pa Bwana; pombe na vileo vyo vyote hatakunywa, lakini atajazwa Roho takatifu papo hapo, atakapozaliwa na mama yake.
16
Atageuza wana wa Isiraeli wengi, warudi kwa Bwana Mungu wao.
17
Mwenyewe atamtangulia Bwana akiwa mwenye roho na nguvu za Elia, aigeuze mioyo ya baba, warudi kwa watoto, awageuze nao wabishi, waufuate ujuzi wa waongofu, amlinganyizie Bwana watu waliojitengeneza.
18
Zakaria akamwambia malaika: Haya nitayatambuaje? Maana mimi ni mzee, nayo miaka ya mke wangu imekuwa mingi.
19
Malaika akajibu, akamwambia: Mimi ni Gaburieli ninayesimama mbele ya Mungu; nimetumwa kusema na wewe, nikupigie mbiu hii njema.
20
Tazama, utakuwa bubu, usiweze kusema mpaka siku hiyo, hayo yatakapokuwapo, kwa sababu hukuyaitikia maneno yangu; nayo yatatimia, siku zao zitakapofika.
21
Wale watu waliokuwa wakimngoja Zakaria, wakastaajabu kukawia kwake katika Jumba la Mungu.
22
Alipotoka hakuweza kusema nao; ndipo, walipotambua, ya kuwa yako mambo, aliyoyaona katika Jumba la Mungu. Naye akawapungia kwa mkono, akakaa kuwa bubu.
23
Ikawa, siku za utambikaji wake zilipomalizika, akaondoka, akaenda nyumbani mwake.
24
Lakini baada ya siku zile mkewe Elisabeti akapata mimba, akajificha miezi mitano, akasema:
25
Ndivyo, alivyonitendea Bwana siku hizi akinitazama, aiondoe soni, niliyokuwa nayo kwa watu.
26
Mwezi wa sita malaika Gaburieli akatumwa na Mungu kwenda katika mji wa Galilea, jina lake Nasareti,
27
amfikie mwanamwali aliyeposwa na mume, jina lake Yosefu, wa mlango wa Dawidi; yule mwanamwali jina lake Maria.
28
Alipoingia mwake akasema: Salamu kwako, kwani yako uliyogawiwa! Bwana yuko pamoja na wewe uliye mwenye kipaji kinachovipita vya wanawake wengine.
29
Alipohangaika kwa neno hili akifikiri kwamba: Huyu ananiamkia kwa namna gani?
30
malaika akamwambia: Usiogope, Maria! Kwani umepata gawio jema kwa Mungu.
31
Tazama, utapata mimba, utazaa mtoto mwana mume, nalo jina lake utamwita YESU.
32
Ndiye atakayekuwa mkuu, ataitwa Mwana wake Alioko huko juu, naye Bwana Mungu atampa kiti cha kifalme cha baba yake Dawidi,
33
atautawala mlango wa Yakobo kale na kale, ufalme wake usiwe na mwisho.
34
Maria akamwambia malaika: Hili litakuwaje? kwani sijajua mume.
35
Malaika akajibu akimwambia: Roho Mtakatifu atakujia, nguvu zake Alioko huko juu zitakufunika kama wingu; kwa hiyo hata mtakatifu atakayezaliwa ataitwa Mwana wake Mungu.
36
Tazama, naye ndugu yako Elisabeti ana mimba ya mtoto mume katika uzee wake, mwezi huu ni wake wa sita, tena alikuwa ameitwa mgumba;
37
kwani hakuna jambo lisilowezekana kwa Mungu.
38
Maria akasema: Tazama, mimi ni kijakazi wa Bwana! Yaniwie, kama ulivyosema! Kisha malaika akaondoka kwake.
39
Siku hizo Maria akainuka, akaenda upesi milimani kufika katika mji wa Yuda.
40
Akaingia nyumbani mwa Zakaria, akamwamkia Elisabeti.
41
Ikawa, Elisabeti aliposikia, Maria anavyomwamkia, kitoto kikarukaruka tumboni mwake, kisha Elisabeti akajazwa Roho takatifu,
42
akapaza sauti kwa nguvu akisema: Wewe umebarikiwa kuliko wanawake wengine, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
43
Tena ni kwa sababu gani, mama yake Bwana wangu akinijia?
44
Kwani sauti yako ya kuniamkia iliponiingia masikioni, mara kitoto tumboni mwangu kilirukaruka kwa kushangilia.
45
Wewe uliyemtegemea Mungu utakuwa mwenye shangwe, kwani yatatimizwa hayo, uliyoambiwa na Bwana.
46
Maria akasema: Bwana ndiye, moyo wangu unayemkuza,
47
roho yangu humshangilia Mungu, mwokozi wangu.
48
Maana ameutazama unyenyekevu wa kijakazi wake; kwani tokea sasa itakuwa, wao wa vizazi vyote wanishangilie.
49
Amenifanyia makuu kwa kuwa mnguvu, Jina lake ni takatifu.
50
Huruma yake huwajia vizazi kwa vizazi wamwogopao.
51
Hufanya ya nguvu kwa mkono wake akiwatawanya waliojikweza katika mawazo ya mioyo yao.
52
Huangusha wenye nguvu katika viti vya kifalme, lakini wao walio wanyenyekevu huwapandisha.
53
Walio wenye njaa huwashibisha mema, lakini wenye mali huwaacha, wajiendee mikono mitupu.
54
Alipokumbuka huruma, akamsaidia mtoto wake Isiraeli,
55
kama alivyowaambia baba zetu, akina Aburahamu nao walio uzao wake kwamba: Wawe wa kale na kale!
56
Maria akakaa kwake, yapata miezi mitatu, kisha akarudi nyumbani kwake.
57
Elisabeti siku zake za kuzaa zilipotimia, akazaa mtoto mume.
58
Majirani zake na ndugu zake waliposikia, ya kuwa Bwana amemwonea huruma nyingi, wakafurahi pamoja naye.
59
Ilipokuwa siku ya nane, wakaja kumtahiri mtoto, wakamwita jina la baba yake: Zakaria.
60
Lakini mama yake akakataa akisema: Sivyo, sharti aitwe Yohana!
61
Wakamwambia: Hakuna mtu katika ndugu zako aitwaye jina hili.
62
Walipompungia baba yake na kumwuliza jina, alilolitaka, mtoto aitwe,
63
akataka kibao, akaandika na kusema: Yohana ndilo jina lake. Wakastaajabu wote.
64
Mara hiyo akafunguka kinywa chake na ulimi wake, akasema na kumtukuza Mungu.
65
Ndipo, woga ulipowashika wote waliokaa kando kando yao; mambo hayo yote yakasimuliwa milimani po pote pa Yudea.
66
Wote walioyasikia wakayaweka mioyoni mwao, wakasema: Basi, huyu mtoto atakuwa wa namna gani? Kwani mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.
67
Baba yake Zakaria akajazwa Roho takatifu, akafumbua yatakayokuwa akisema:
68
*Atukuzwe Bwana Mungu wa Isiraeli! kwani amewakagua wao wa ukoo wake na kuwapatia ukombozi.
69
Ametusimikia pembe ya wokovu katika mlango wa mtoto wake Dawidi,
70
kama alivyosema kale kwa vinywa vya wafumbuaji wake watakatifu.
71
Akatupatia wokovu kwao walio adui zetu namo mikononi mwao wote wanaotuchukia.
72
Aliwahurumia baba zetu, akalikumbuka Agano lake takatifu
73
nacho kiapo chake, alichomwapia baba yetu Aburahamu kwamba:
74
Tupate kukombolewa mikononi mwa adui zetu, tukae pasipo woga na kumtumikia siku zetu zote
75
tukiwa mbele yake wenye utakaso na wongofu.
76
Nawe kitoto, utaitwa mfumbuaji wake Alioko huko juu, utatangulia mbele ya Bwana, uzitengeneze njia zake
77
na kuwatambulisha wao wa ukoo wake wokovu wao, ya kuwa uko katika kuondolewa makosa yao.
78
Tukivipata hivi, ni kwa huruma zilizomo moyoni mwake Mungu wetu; kwa hiyo umetukagua mwanga unaotoka juu,
79
uwaangaze wanaokaa gizani kwenye kivuli kuuacho, uelekeze miguu yetu, ishike njia ya utengemano.
80
Yule mtoto alipokua akapata nguvu Rohoni, akakaa nyikani mpaka siku, alipowatokea Waisiraeli.*
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24