bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 16
Luke 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 17 →
1
*Akawaambia wanafunzi wake: Kulikuwako mtu mwenye mali aliyekuwa na mtunza mali. Huyu aliposengenywa kwake, ya kuwa anatapanya mali zake,
2
akamwita, akamwambia: Hayo nayasikiaje kwako? Toa hesabu ya utunzaji wako wa mali zangu! Kwani huwezi tena kuzitunza mali zangu.
3
Mtunza mali akasema moyoni mwake: Nifanyeje? Kwani bwana wangu ananiondoa katika utunzaji wa mali. Kulima siwezi; nako kuomba, naona soni.
4
Nimetambua, nitakavyofanya, kusudi wanipokee nyumbani mwao, nitakapoondolewa katika utunzaji wa mali.
5
Akawaita wadeni wa bwana wake kila mmoja, akamwambia wa kwanza: Una deni gani kwa bwana wangu?
6
Aliposema: Matanaki 100 ya mafuta, akamwambia: Kichukue cheti chako, ukae, uandike 50!
7
Kisha akamwambia mwingine: Na wewe una deni gani? Naye aliposema: Makanda 100 ya mchele, akamwambia: Kichukue cheti chako, uandike 80!
8
Naye bwana akamsifu yule mtunza mali mpotovu, ya kuwa alifanya werevu. Kwani wana wa dunia hii huwaendea wa kizazi chao wenye werevu kuliko wana wa mwanga.
9
Nami nawaambiani: Jipatieni rafiki na kutoa mali za nchini zilizo za upotovu, kusudi wawapokee kwenye makao ya kale na kale, mali zitakapokoseka!
10
Aliye mwelekevu wa vitu vilivyo vichache huwa mwelekevu hata wa vile vilivyo vingi. Naye aliye mpotovu wa vitu vilivyo vichache huwa mpotovu hata wa vile vilivyo vingi.
11
Basi, msipokuwa waelekevu wa mali za nchini zilizo za upotovu, yuko nani atakayewapa yaliyo ya kweli?*
12
Nanyi msipokuwa waelekevu wa mali zilizo za wengine, yuko nani atakayewapa zilizo zenu?
13
Hakuna mtumishi anayeweza kutumikia mabwana wawili. Kwani itakuwa hivi: atamchukia wa kwanza na kumpenda wa pili, au atashikamana naye wa kwanza na kumbeza wa pili. Hamwezi kuwatumikia wote wawili, Mungu na Mali za Nchini (Mamona).
14
Mafariseo waliopenda fedha walipoyasikia hayo yote, wakamfyoza.
15
Akawaambia: Ninyi hujipa wongofu wenyewe mbele ya watu, lakini Mungu anaitambua mioyo yenu. Kwani yanayokwezwa na watu huwa chukizo mbele yake Mungu.
16
Mambo ya Maonyo na ya Wafumbuaji yametangazwa mpaka kuja kwake Yohana; toka hapo hutangazwa Utume mwema wa ufalme wa Mungu, tena kila mtu huingizwa kwa nguvu.
17
Kukoma kwao mbingu na nchi ni kwepesi kuliko kupotea kwa kichoro kimoja tu cha Maonyo.
18
Kila mtu anayemwacha mkewe na kuoa mwingine anazini; naye anayeoa mke aliyeachwa na mumewe anazini.
19
*Kulikuwa na mtu mwenye mali aliyevaa nguo za kifalme na za hariri, tena kila siku hula vya urembo vilivyo vizuri sana.
20
Kulikuwako hata maskini, jina lake Lazaro, alikuwa amewekwa mlangoni pake kwa kuwa mwenye vidonda.
21
Akataka sana kushibishwa na makombo yaliyoanguka mezani pake mwenye mali; mbwa nao huja kumlamba vidonda vyake.
22
Ikawa, maskini alipokufa akachukuliwa na malaika, akapelekwa kifuani pa Aburahamu. Kisha mwenye mali akafa naye, akazikwa.
23
Alipokuwa kuzimuni katika maumivu akayainua macho yake, akamwona Aburahamu, yuko mbali, naye Lazaro alikuwa amekaa kifuani pake.
24
Akaita akisema: Baba Aburahamu, nihurumie! Umtume Lazaro, achovye ncha ya kidole chake majini, aje, aupoze ulimi wangu! kwani naumia humu motoni.
25
Aburahamu akasema: Mwanangu, kumbuka, ya kuwa uliyapokea mema yako katika maisha yako! Lakini Lazaro huko alipata maovu tu. Lakini sasa yeye anatulizwa moyo hapa, nawe wewe unaumia.
26
Tena si kwa ajili hii tu, ila kati yetu sisi nanyi pameatuka ufa mkubwa, kusudi wanaotaka kupita toka hapa, wafike kwenu, wasiweze, wala toka huko wasiweze kupapita, wafike kwetu.
27
Ndipo, alipojibu: Nakuomba, baba, umtume, aende nyumbani kwa baba yangu.
28
Kwani ninao ndugu watano; aje, awashuhudie mambo ya hapa, nao wasije hapa penye maumivu.
29
Aburahamu aliposema: Wanao Mose na Wafumbuaji, na wawasikilize wao!
30
akasema: Sivyo, baba Aburahamu, lakini mtu aliyetoka kwa wafu atakapowaendea, ndipo, watakapojuta.
31
Lakini akamwambia: Wasipomsikia Mose na Wafumbuaji hawataonyeka, hata mtu akifufuka katika wafu.*
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24