bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 14
Luke 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 15 →
1
*Ikawa, alipoingia siku ya mapumziko nyumbani mwa mkuu wa Mafariseo, ale chakula, wakawa wakimtunduia.
2
Mbele yake mkawamo mtu mwenye ugonjwa wa safura.
3
Yesu akawauliza wajuzi wa Maonyo na Mafariseo akisema: Uko mwiko wa kuponya mtu siku ya mapumziko au hakuna?
4
Wao waliponyamaza, akamshika, akamponya, akamwaga.
5
Kisha akawaambia wale: Kwenu yuko mwenye punda au ng'ombe asiyemwopoa papo hapo, akitumbukia kisimani, hata ikiwa siku ya mapumziko?
6
Nao hawakuweza kumjibu haya.
7
Alipoona, walioalikwa walivyochagua viti vya mbele, akawatolea mfano akiwaambia:
8
Ukialikwa na mtu, uje arusini, usikae penye viti vya mbele! Labda miongoni mwao walioalikwa yumo mwenye ukuu kukupita.
9
Basi, anapokuja mwenye kuwaalika wewe na yeye atakuambia: Mpishe huyu! Ndipo, utakapoanza kupatwa na soni kwa kushika mahali palipo nyuma yao wote.
10
Ila ukialikwa uende, ukakae mahali pa nyuma! Maana mwenye kukualika atakapokuja akuambie: Mwenzangu, sogea mbele huku! Ndipo, utakapotukuzwa mbele yao wote, ambao mnakaa pamoja nao chakulani.
11
Kwani kila anayejikweza mwenyewe atanyenyekezwa, naye anayejinyenyekeza mwenyewe atakwezwa.*
12
Kisha akamwambia yule aliyemwalika: Unapofanya karamu ya mchana au ya jioni usiwaalike rafiki zako wala ndugu zako wala jamaa zako wala majirani walio wenye mali! Maana wasikualike tena, nawe ukapata kulipwa.
13
Ila unapofanya karamu uwaalike wakiwa na wavilema na viwete na vipofu!
14
Ndipo, utakapokuwa mwenye shangwe, kwani hawana cha kukulipa. Maana utalipwa, waongofu watakapofufuka.
15
Mmoja wao walikaa pamoja naye chakulani alipoyasikia haya akamwambia: Mwenye shangwe ndiye atakayekula chakula katika ufalme wa Mungu.
16
*Naye akamwambia: Kulikuwa na mtu aliyetengeneza karamu kubwa, akaalika wengi.
17
Saa ya karamu ilipotimia, akatuma mtumwa wake, aende, awaambie walioalikwa: Njoni! Kwani vyote viko tayari.
18
Wakaanza wote pamoja kuja kujipuzapuza. Wa kwanza akamwambia: Nimenunua shamba, sina budi kwenda, nilitazame; nakuomba, usiniwekee mfundo!
19
Mwingine akasema: Nimenunua ng'ombe kumi wa kuvuta magari, nami ninakwenda, niwajaribu; nakuomba, usiniwekee mfundo!
20
Mwingine akasema: Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.
21
Basi, mtumwa akarudi, akamsimulia bwana wake. Ndipo, yule mwenye nyumba alipochafuka, akamwambia mtumwa wake: Toka, uende upesi, ufike kwenye viwanja na njia za mjini, ulete wakiwa na wavilema na vipofu na viwete, uwaingize humu!
22
Kisha mtumwa akasema: Bwana, imekwisha fanyika, uliyoniagiza, lakini hamjajaa bado.
23
Naye bwana akamwambia mtumwa: Toka, ufike njiani na nyugoni, uwashurutishe kuingia, nyumba yangu ipate kujaa!
24
Kwani nawaambiani: Waume wale waliokuwa wamealikwa hakuna hata mmoja wao atakayevionja vyakula vyangu.*
25
Walipofuatana naye makundi mengi, akageuka, akawaambia:
26
Mtu akija kwangu asipomchukia baba yake na mama yake na mkewe na watoto wake na ndugu zake wa kiume na wa kike, hata asipoichukia roho yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
27
Naye asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
28
Maana kwenu yuko mtu anayetaka kujenga mnara, asiyekaa kwanza na kuzihesabu shilingi za jengo, kama anazo za kulitimiza?
29
Kwani akiisha kuweka msingi, asipoweza kumaliza, halafu wote wanaoviona wataanza kumfyoza
30
wakisema: Mtu huyu alianza kujenga, naye hakuweza kumaliza.
31
Au yuko mfalme anayekwenda vitani kushindana na mfalme mwenzake pasipo kukaa kwanza na kufikiri, kama ataweza kuwatuma askari wake elfu kumi, wakutane na yule anayemjia na askari elfu ishirini?
32
Kama haviwezi, atatuma wajumbe, yule mwingine akingali mbali bado, amwombe mapatano.
33
Vivyo hivyo hata kila mmoja wenu asiyeviacha vyote, alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
34
Chumvi ni nzuri, lakini chumvi ikiwa imepotewa na ukolezi itatiwa kiungo gani, ipate kukolea tena?
35
Haitafaa tena, wala kutupwa shambani wala penye mbolea, ile huitupa nje tu. Mwenye masikio yanayosikia na asikie!
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24