bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 9
Luke 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 10 →
1
Akawaita wale kumi na wawili, wakusanyike, akawapa uwezo na nguvu za kufukuza pepo wote na za kuponya magonjwa.
2
Akawatuma, wautangaze ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.
3
Akawaambia: Msichukue kitu cha njiani, wala fimbo wala mkoba wala chakula wala shilingi, tena mtu asiwe na nguo mbili!
4
Nyumbani mo mote mtakamoingia, kaeni humo! Namo ndimo, mtakamotoka tena!
5
Nao wote wasiowapokea, basi, utokeni mji wao na kuyakung'uta mavumbi yaliyoishika miguu yenu, yaje yanishuhudie kwao!
6
Wakatoka, wakapita vijijini wakiipiga hiyo mbiu njema na kuponya wagonjwa po pote.
7
Mfalme Herode alipoyasikia mambo yote yaliyokuwapo, akahangaika, maana wengine walisema: Yohana amefufuka katika wafu,
8
wengine: Elia ametokea, wengine: Mmoja wao wafumbuaji wa kale amefufuka.
9
Lakini Herode akasema: Yohana mimi nimemkata kichwa. Lakini huyo ni nani, ninayemsikia mambo kama hayo? Akatafuta kumwona.
10
Mitume waliporudi, wakamsimulia mambo yote, waliyoyafanya. Kisha akawachukua, akaondoka kwenda nao peke yao, wakaingia mji, jina lake Beti-Saida.
11
Makundi ya watu walipovitambua wakamfuata, naye akawapokea, akasema nao mambo ya ufalme wa Mungu, akawaponya waliopaswa na kuponywa.
12
Jua lilipotaka kuchwa, wale kumi na wawili wakamjia, wakamwambia: Uliage kundi la watu, waende zao vijijini na mashambani huko pembenipembeni, waone ulalo na vyakula, kwani hapa tulipo ni nyika.
13
Akawaambia: Wapeni ninyi vyakula! Wakasema: Sisi hatuna kitu hapa kuliko mikate mitano na visamaki viwili; au twende sisi kuwanunulia watu hawa wote vyakula?
14
Kwani waume tu waliokuwako walipata 5000. Akawaambia wanafunzi wake: Mwaagize, wakae mafungumafungu kama hamsinihamsini!
15
Wakafanya hivyo, wakawakalisha wote.
16
Akaitwaa ile mikate mitano na vile visamaki viwili, akatazama juu mbinguni, akaviombea, akawamegeamegea, akawapa wanafuanzi, wawapangie hao watu wengi.
17
Wakala, wakashiba wote, pakaokotwa makombo yaliyowasalia vikapu kumi na viwili.
18
*Ikawa, alipokuwa akiomba peke yake, wakawapo pamoja naye wanafunzi wake, akawauliza akisema: Makundi ya watu hunisema kuwa ni nani?
19
Nao wakajibu wakisema: Wanakusema kuwa u Yohana Mbatizaji, wengine: Elia, wengine husema: Amefufuka mmoja wao wafumbuaji wa kale.
20
Kisha akawauliza: Lakini ninyi mnanisema kuwa ni nani? Petero akajibu akisema: Kristo wa Mungu.
21
Ndipo, alipowatisha na kuwakataza, wasimwambie mtu neno hilo.
22
Akawaambia: Imempasa Mwana wa mtu kutwa mengi na kukataliwa nao wazee na watambikaji wakuu na waandishi, mpaka auawe, kisha afufuliwe siku ya tatu.
23
Akawaambia wote: Mtu akitaka kunifuata mimi ajikataze mapenzi yake, ajitwishe kila siku nao msalaba wake, kisha anifuate!
24
Maana mtu anayetaka kuiokoa roho yake ataiangamiza. Lakini mtu atakayeiangamiza roho yake kwa ajili yangu mimi, huyo ataiokoa.
25
Kwani mtu vinamfaa nini, avichume vya ulimwengu wote, akijiangamiza mwenyewe, au akiponzwa navyo?
26
Kwani mtu atakayenionea soni mimi na maneno yangu, basi, naye Mwana wa mtu atamwonea soni huyo atakapokuja mwenye utukufu wake yeye na wa Baba yake na wa malaika watakatifu.*
27
Lakini nawaambiani lililo kweli: Miongoni mwao wanaosimama hapa wamo wengine, ambao hawatakuonja kufa, mpaka watakapouona ufalme wa Mungu.
28
Ikawa, walipokwisha kuyasema hayo, zikipita kama siku nane, akamchukua Petero na Yohana na Yakobo, wakapanda mlimani kuomba
29
Alipokuwa akiomba, sura ya uso wake ikawa nyingine, nazo nguo zake zikawa nyeupe na kumerimeta.
30
Walipotazama, wakawako waume wawili wakiongea naye, nao walikuwa Mose na Elia.
31
Wakawatokea wenye utukufu, wakasema naye, ndivyo aende kuyatimiza mambo ya kufa kwake kule Yerusalemu.
32
Lakini Petero na wenziwe walikuwa wamelemewa na usingizi. Walipoamka wakauona utukufu wake na wale waume wawili waliosimama naye.
33
Ikawa, walipotengwa naye, Petero akamwambia Yesu: Bwana, hapa ni pazuri kuwapo sisi, na tujenge vibanda vitatu, kimoja chako, na kimoja cha Mose, na kimoja cha Elia! kwani hakujua, alilolisema.
34
Angali akiyasema haya, pakawa na wingu, likawatia kivuli, wakashikwa na woga walipoingiwa na wingu lile.
35
Sauti ikatoka winguni, ikasema: Huyu ndiye mwanangu, niliyemchagua, msikilizeni yeye!
36
Sauti hiyo iliposikilika, Yesu akaonekana, yuko peke yake. Siku zile wakanyamaza, wasimsimulie mtu hata moja lao hayo waliyoyaona.
37
Ikawa siku ya kesho, waliposhuka mlimani wakakutana na kundi la watu wengi.
38
Mle kundini mkawamo mwanamume, akapaza sauti akisema: Mfunzi, nakuomba, umtazame huyu mwanangu, kwani ni wangu wa pekee!
39
Tazama, pepo humpagaa, naye mara moja hulia kwa kukumbwa, mpaka akitoka pofu; akiisha kumlegeza hukawia kumwondokea.
40
Nikawaomba wanafunzi wako, wamfukuze, lakini hawakuweza.
41
Yesu akajibu akisema: Enyi wa kizazi kisichomtegemea Mungu kwa kupotoka! Nitakuwapo nanyi na kuwavumilia mpaka lini? Umlete mwana wako, aje hapa!
42
Alipokuwa akija, pepo akamkamata kwa nguvu, akamkumba. Lakini Yesu akamkaripia huyo pepo mchafu, akamponya mtoto, akamrudishia baba yake.
43
Ndipo, wote walipoingiwa na kituko kwa ajili ya ukubwa wa nguvu yake Mungu. Wao wote walipoyastaajabu yote, aliyoyafanyiza, akawaambia wanafunzi wake:
44
Myaweke vema maneno haya masikioni mwenu! Maana Mwana wa mtu atatiwa mikononi mwa watu.
45
Lakini hawakulitambua neno hili, likawa limefichiwa wao, wasilione maana. Nao wakaogopa kumwuliza tena neno hilo.
46
Wakawa wakiwaza mioyoni mwao kwamba: Aliye mkuu kwetu ni nani?
47
Lakini Yesu akayajua, waliyoyawaza mioyoni mwao, akatwaa kitoto, akamsimamisha kando yake,
48
akawaambia: Mtu atakayempokea kitoto huyu kwa Jina langu hunipokea mimi. Tena akinipokea mimi humpokea yule aliyenituma mimi. Kwani aliye mdogo kwenu ninyi wote, huyo ndiye mkuu.
49
Yohana akajibu akisema: Bwana, tuliona mtu anayefukuza pepo kwa Jina lako; tukamzuia, kwani hafuatani nasi.
50
Yesu akamwambia: Msimzuie! Kwani asiyewakataa yuko upande wenu.
51
*Ikawa, zilipotimia siku zake za kuchukuliwa mbinguni, mwenyewe akauelekeza uso kwenda Yerusalemu,
52
akatanguliza wajumbe mbele yake. Hao walipokwenda, kuingia kijiji cha Wasamaria, wamtengenezee mahali,
53
hawakumpokea, kwani uso wake ulikuwa umeelekea kwenda Yerusalemu.
54
Wanafunzi akina Yakobo na Yohana walipoviona wakasema: Bwana, wataka, tuseme, moto ushuke toka mbinguni, uwamalize, kama Elia naye alivyofanya?
55
Lakini akapinduka, akawatisha akiwaambia: Hamjui, kama m wenye Roho gani?
56
Mwana wa mtu hakujia kuangamiza roho za watu, ila kuziokoa. Kisha wakaenda zao, wakafikia kijiji kingine.*
57
Walipokuwa wakienda njiani, palikuwapo aliyemwambia: Nitakufuata po pote, utakapokwenda.
58
Yesu akamwambia: Mbweha wanayo mapango, nao ndege wa angani wanavyo vituo, lakini Mwana wa mtu hana pa kukilazia kichwa chake.
59
Alipomwambia mtu mwingine akasema: Nifuate! huyo akasema: Nipe ruhusa, kwanza niende nimzike baba yangu!
60
Naye akamwambia: Waache wafu, wazike wao kwa wao! Lakini wewe nenda, uutangaze ufalme wa Mungu!
61
Mtu mwingine akasema: Nitakufuata, Bwana, lakini kwanza nipe ruhusa, niwaage waliomo nyumbani mwangu!
62
Yesu akamwambia: Mtu ashikaye jembe mkononi na kuvitazama vya nyumba, huyo hatauweza ufalme wa Mungu.*
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24