bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 19
Luke 19
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 20 →
1
*Alipoingia Yeriko akapita kati ya mji.
2
Mle akaona mtu aliyeitwa jina lake Zakeo, alikuwa mkubwa wa watoza kodi, tena mwenye mali.
3
Alitaka kumwona Yesu, alivyo, lakini hakuweza, kwa sababu watu walikuwa wengi, naye alikuwa mfupi kwa umbo lake.
4
Akapiga mbio, aje mbele, akapanda mtamba, apate kumwona, kwani njia yake ilipitia papo hapo.
5
Yesu alipofika hapo akatazama juu, akamwambia: Zakeo, shuka upesi! Kwani leo sharti nikae nyumbani mwako!
6
Ndipo, aliposhuka upesi, akampokea na kufurahi.
7
Lakini walioviona wakamnung'unikia wote wakisema: Ameingia nyumbani mwake mkosaji na kutua humo.
8
Zakeo akainuka, akamwambia Bwana: Tazama, Bwana, nusu yao vyote, nilivyo navyo, nawapa maskini, tena kama nimepunja mtu, namrudishia mara nne.
9
Lakini Yesu akamwambia: Leo nyumbani humu mmeonekana wokovu, kwani mwenyewe naye ni mwana wa Aburahamu.
10
Kwani Mwana wa mtu amejia kutafuta na kuokoa kilichopotea.*
11
*Watu walipoyasikia hayo, akaongeza kusema na kutoa mfano. Kwa sababu alikuwa karibu ya Yerusalemu, watu wakawaza kwamba: Ufalme wa Mungu sharti utokee sasa hivi.
12
Kwa hiyo akasema: Mtu wa kifalme alikwenda kufika katika nchi ya mbali, ajipatie ufalme, kisha arudi.
13
Akawaita watumwa wake kumi, akawapa mia kumi za shilingi, akawaambia: Zichuuzieni, mpaka nitakaporudi!
14
Lakini wenyeji wake walimchukia, wakatuma wajumbe nyuma yake wakisema: Hatumtaki huyu, atutawale sisi.
15
Ikawa, alipokwisha kuupata ule ufalme, akarudi akaagiza, waitwe wale watumwa, aliowapa fedha, waje kwake, apate kujua, kila mtu alivyojipatia kwa kuzichuuzia.
16
Alipokuja wa kwanza, akasema: Bwana, shilingi zako mia zimeleta mia kumi nyingine.
17
Naye akamwambia: Vema, wewe mtumwa mwema, ulikuwa mwelekevu wa machache, utatwaa miji kumi, uitawale!
18
Alipokuja wa pili, akasema: Bwana, shilingi zako mia zimeleta mia tano.
19
Huyu naye akamwambia: Wewe nawe twaa miji mitano, uitawale!
20
Alipokuja mwingine wao akasema: Bwana, tazama hapa shilingi zako mia! Nimekuwa nimeziweka katika mharuma.
21
Kwani nilikuogopa, kwa kuwa wewe u mkorofi, hutwaa usiyoyaweka, huvuna usioyoyapanda.
22
Akamwambia: Kwa maneno yako wewe ninakuumbua, wewe mtumwa mbaya! Ulinijua, ya kuwa mimi ni mkorofi, hutwaa nisiyoyaweka, huvuna nisiyoyapanda?
23
Basi, kwa nini hukumpa mwenye duka fedha zangu? Nami nilipokuja ningalizichukua pamoja na faida?
24
Akawaambia walioko: Zichukueni shilingi zake mia, mmpe yule mwenye mia kumi!
25
Wakamwambia: Bwana, anazo mia kumi!
26
(Akajibu:) Nawaambiani: Kila mwenye mali atapewa; lakini asiye na kitu, atachukuliwa hata kile, alicho nacho.
27
Lakini wale wachukivu wangu wasionitaka, niwatawale, mwalete hapa, mwachinje mbele yangu!*
28
Alipokwisha kuyasema hayo akaendelea kusafiri, akapanda kwenda Yerusalemu.
29
Ikawa, alipokaribia Beti-Fage na Betania penye mlima unaoitwa Wa Michekele, akatuma wanafunzi wawili
30
akisem: Nendeni katika kijiji kinachowaelekea! Mtakapoingia mle mtaona, pamefungwa mwana punda, ambaye mtu hajampanda bado; mfungueni, mmlete!
31
Kama mtu atawauliza: Mbona mnamfungua? semeni hivi: Bwana wetu anamtakia kazi!
32
Wao waliotumwa walipoondoka kwenda wakaviona, kama alivyowaambia.
33
Walipomfungua mwana punda, wenyewe wakawauliza: Kwa sababu gani mnamfungua mwana punda?
34
Nao wakasema: Bwana anamtakia kazi.
35
Kisha wakampeleka kwa Yesu, wakatandika nguo zao upesiupesi juu ya mwana punda, wakampandisha Yesu.
36
Alipokwenda, wakatandika nguo zao njiani.
37
Alipofika kwenye mtelemko wa mlima wa michekele, wingi wote wa wanafunzi ukaanza kushangilia na kumsifu Mungu wakipaza sauti kwa ajili ya matendo yote ya nguvu, waliyoyaona.
38
Wakasema: Na atukuzwe ajaye kuwa mfalme kwa Jina la Bwana! Mbinguni uko utengemano, nao utukufu uko juu mbinguni!
39
Hapo palikuwa na Mafariseo mle kundini mwa watu, wakamwambia: Mfunzi, wakaripie wanafunzi wako!
40
Akajibu akisema: Nawaambiani: Hawa watakaponyamaza, mawe yatapiga makelele.
41
*Alipofika karibu, akautazama ule mji, akaulilia akisema:
42
Ungaliyatambua na wewe siku hii ya leo yanayokupa utengemano! Lakini sasa yamefichika, macho yako yasiyaone!
43
Kwani siku zitakujia, adui zako watakapokujengea boma, likuzinge, wapate kukuhangisha po pote.
44
Nao watakubomolea wewe na watoto wako waliomo mwako, wasiache mwako jiwe, lishikane na jiwe lenziwe, kwa sababu hukuzitambua siku, ulipokaguliwa.
45
Akapaingia Patakatifu, akaanza kuwafukuza wenye kuchuuzia pale,
46
akawaambia: Imeandikwa: Nyumba yangu sharti iwe nyumba ya kuombea, lakini ninyi mmeigeuza kuwa pango la wanyang'anyi.
47
Kisha akawa akifundishia Patakatifu kila siku. Lakini watambikaji wakuu na waandishi na wakubwa wa watu wakatafuta kumwangamiza,
48
wasione njia ya kuyafanya; kwani watu wote pia walishikamana naye na kumsikiliza.*
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 20 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24