bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 4
Luke 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 5 →
1
Yesu akajaa Roho takatifu, akarudi akitoka huko Yordani, akapelekwa na Roho nyikani,
2
akajaribiwa siku 40 na Msengenyaji. Siku zile hakula cho chote; zilipokwisha pita, akaona njaa.
3
Msengenyaji akamwambia: Kama ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili, liwe chakula!
4
Yesu akamjibu akisema: Imeandikwa: Mtu hataishi kwa chakula tu, ila kwa kila neno la Mungu.
5
Kisha akampandisha mlimani, akamwonyesha kwa kitambo kidogo ufalme wote pia wa ulimwengu.
6
Kisha Msengenyaji akamwambia: Nguvu hii yote na utukufu wake nitakupa wewe; kwani mimi nimepewa, nami humpa ye yote, nimtakaye.
7
Basi, wewe ukiniangukia hapa machoni pangu, yote yatakuwa yako.
8
Yesu akajibu akimwambia: Ondoka nyuma yangu, Satani! Imeandikwa: Umwangukie Bwana Mungu wako na kumtumikia peke yake!
9
Kisha akampeleka Yerusalemu, akamsimamisha juu pembeni hapo Patakatifu, akamwambia: Kama ndiwe Mwana wa Mungu, ruka hapa, ujitupe chini!
10
Kwani imeandikwa: Atakuagizia malaika zake, wakulinde,
11
nao watakuchukua mikononi mwao, usije kujikwaa mguu wako katika jiwe.
12
Yesu akajibu akimwambia: Liko neno la kwamba: Usimjaribu Bwana Mungu wako!
13
Msengenyaji alipokwisha kumjaribu yote akaondoka, akamwacha kwanza.
14
Yesu akarudi Galilea mwenye nguvu ya Roho, akavumika katika nchi zote zilizoko pembenipembeni.
15
Naye alipofundisha katika nyumba zao za kuombea akatukuzwa nao wote.
16
*Alipofika Nasareti, - ndio mji, alimolelewa, - akaingia siku ya mapumziko nyumbani mwa kuombea, kama alivyozoea. Alipoinuka kuwasomea
17
akapewa kitabu cha mfumbuaji Yesaya; alipokifunua hicho kitabu akaona mahali palipolandikwa:
18
Roho ya Bwana inanikalia, kwa hiyo ameanipaka mafuta, niwapigie maskini mbiu njema. Amenituma, niwatangazie mateka, ya kuwa watakombolewa, nao vipofu, ya kuwa wataona, niwape ruhusa walioumizwa, wajiendee,
19
niutangaze mwaka wa Bwana upendezao.
20
Kisha akakifunga kitabu, akamrudishia mtumishi, akaketi. Ndipo, wote waliokuwamo humo nyumbani mwa kuombea walipomkazia macho,
21
akaanza kuwaambia: Leo hivi yaliyoandikwa hapa yametimia masikioni penu.*
22
Nao wote wakamshuihudia ya kuwa ndivyo, wakastaajabu maneno ya upole yaliyotoka kinywani mwake, wakasema: Huyu si mwana wa Yosefu?
23
Akawaambia: Kweli mtaniambia fumbo hili: Mganga, jiponye mwenyewe! Hata huku kwako, ulikokulia, yafanye, tuliyoyasikia, ya kuwa yamefanyika Kapernaumu!
24
Lakini akasema: Kweli nawaambiani: Hakuna mfumbuaji anayepokelewa kwao, alikokulia.
25
Nawaambiani ya kweli: Siku za Elia kulikuwa na wajane wengi katika Waisiraeli; ni hapo, mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita, ikawa njaa kubwa katika nchi zote.
26
Lakini hao Elia hakutumwa kwa mwenzao mmoja, ila alitumwa Sareputa wa Sidoni kwa mwanamke mjane wa kule.
27
Tena siku za mfumbuaji Elisa kulikuwa na wenye ukoma wengi katika Waisiraeli, lakini kwao hao hakuna aliyetakaswa ila Namani wa Ushami.
28
Wote waliokuwamo humo nyumbani mwa kuombea walipoyasikia haya, mioyo yao ikajaa makali,
29
wakainuka, wakamfukuza mjini, wakampeleka ukingoni pa mlima, ambao mji wao ulikuwa umejengwa juu yake, wapate kumsukuma chini.
30
Lakini yeye akapita katikati yao, akaenda zake.
31
Akashuka kwenda Kapernaumu, mji wa Galilea, akawa akiwafundisha siku ya mapumziko.
32
Nao wakashangazwa na mafundisho yake, kwani maneno yake yalikuwa yenye nguvu.
33
Humo nyumbani mwa kuombea mkawa na mtu mwenye pepo mchafu, akapaza sauti na kupiga kelele:
34
Acha! Tuko na jambo gani sisi na wewe, Yesu wa Nasareti? Umekuja kutuangamiza. Nakujua, kama u nani; ndiwe Mtakatifu wa Mungu.
35
Yesu alipomkaripia akisema: Nyamaza, umtoke! ndipo, yule pepo alipomkumba, aanguke katikati, kisha akamtoka pasipo kumwumiza.
36
Wote wakaingiwa na kituko, wakasemezana wao kwa wao wakiuliza: Neno gani hilo? Anawaagiza pepo wachafu kwa nguvu ya kifalme, nao hutoka!
37
Huo uvumi wake ukatoka, ukafika po pote penye nchi zilizoko pembenipembeni.
38
Alipoondoka nyumbani mwa kuombea akaingia nyumbani mwa Simoni. Naye mama ya mkewe Simoni alikuwa ameshikwa na homa kali, wakamwombea kwake.
39
Akaja, akasimama kichwani pake, akaikaripia homa; ndipo, ilipomwacha. Papo hapo akainuka kitandani, akawatumikia.
40
Jua lilipokuchwa, wakaja wote waliokuwa na wanyonge wa magonjwa menginemengine, wakiwaleta kwake; akawaponya kwa kuwabandikia mikono kila mmoja.
41
Hata pepo wakatoka wengi wakipiga kelele na kusema: Wewe ndiwe Mwana wa Mungu. Lakini akawakaripia, akawakataza kusema, ya kuwa walimjua kuwa yeye ni Kristo.
42
Lakini kulipokucha, akatoka, akaenda mahali palipokuwa pasipo watu. Ndipo, makundi ya watu walipomtafuta, wakaja kwake, wakamzuia, asiondoke kwao.
43
Lakini akawaambia: Inanipasa kuipigia hata miji mingine mbiu njema ya ufalme wa Mungu, kwani hiyo ndiyo, niliyotumiwa.
44
Kisha akawa akiipiga hiyo mbiu katika nyumba za kuombea zilizoko Galilea.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24