bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 15
Luke 15
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 16 →
1
*Watoza kodi na wakosaji wo wote walipokuwa wanamjia, wamsikilize,
2
Mafariseo na waandishi wakanung'unika wakisema: Huyu huwapokea wakosaji, ale pamoja nao.
3
Ndipo, alipowatolea mfano huu akisema:
4
Kwenu yuko mtu mwenye kondoo mia akipoteza mmoja wao, asiyewaacha wale tisini na tisa porini, aende kumtafuta yule aliyepotea, mpaka atakapomwona?
5
Naye akimwona anamweka mabegani kwa kufurahi.
6
Tena akifika kwao anawaita rafiki zake na majirani zake na kuwaambia: Furahini pamoja nami! Kwani nimemwona kondoo wangu aliyepotea.
7
Nawaambiani: Vivyo hivyo mkosaji mmoja anapojuta, kutakuwako huko mbinguni furaha inayoipita ile iliyoko kwa ajili ya waongofu tisini na tisa wasiopaswa na kujuta.
8
Au yuko mwanamke mwenye shilingi kumi akipoteza moja, asiyewasha taa na kufagia nyumbani na kuitafuta kwa uangalifu, mpaka atakapoiona?
9
Naye akiiona anawaita shoga zake na majirani zake na kusema: Furahini pamoja nami! Kwani nimeiona shilingi yangu, niliyoipoteza.
10
Nawaambieni: Vivyo hivyo mkosaji mmoja anapojuta, itakuwako furaha mbele ya malaika za Mungu.*
11
*Kisha akasema: Kulikuwa na mtu mwenye wana wawili.
12
Aliye mdogo wao akamwambia baba yake: Baba, nipe fungu la mali litakalokuwa langu! Ndipo, alipowagawanyia mali.
13
Siku chache zilipopita, mwana mdogo akavikusanya vyote, akajiendea kufika katika nchi ya mbali. Huko akazitapanya mali zake kwa kuzitumia ovyoovyo tu.
14
Alipoziishia zote pia, njaa kubwa ikaiguia nchi ile, naye akaanza kuumia kwa njaa.
15
Ndipo, alipokwenda kugandamiana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye akamtuma shambani, achunge nguruwe.
16
Akataka sana kulijaza tumbo lake maganda tu, nguruwe waliyokula, lakini hakuna aliyempa.
17
Ndipo, alipojirudia mwenyewe akisema: Vibarua wangapi wako kwa baba yangu wanaoshiba chakula na kusaza, nami hapa ninakufa njaa!
18
Nitainuka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia: Baba, nimemkosea Mungu na wewe;
19
hainipasi tena kuitwa mwana wako, unitumikishe kuwa kama kibarua wako!
20
Kisha akaondoka, akaenda kwa baba yake. Akingali mbali bado, baba yake akamwona, akamwonea uchungu, akapiga mbio, akamkumbatia shingoni, akamnonea.
21
Mwanawe akamwambia: Baba, nimemkosea Mungu na wewe; hainipasi tena kuitwa mwana wako.
22
Lakini baba yake akawaambia watumwa wake: Leteni upesi nguo iliyo nzuri kuliko zote, mmvike! Mtieni hata pete kidoleni na viatu miguuni!
23
Kisha mleteni yule ndama aliyenona, mmchinje, tupate kula na kushangilia!
24
Kwani huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana tena. Wakaanza kushangilia.
25
Lakini mwana wake mkubwa alikuwa shambani; alipokuja na kufika karibu ya mjini akasikia nyimbo na michezo.
26
Akaita mtumwa mmoja, akamwuliza: Mambo hayo ya nini?
27
Naye akamwambia: Ndugu yako amekuja; ndipo, baba yako alipomchinjia yule ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yuko mzima.
28
Akakasirika sana, hakutaka kuingia. Lakini baba yake alipotoka na kumbembeleza,
29
akamjibu baba yake akimwambia: Tazama, miaka hii yote ninakutumikia; tena hakuna agizo lako, nisilolifanya. Nawe hujanipa hata kibuzi, nipate kushangilia na rafiki zangu.
30
Lakini alipokuja huyu mwana wako aliyekula mali zako pamoja na wagoni, umemchinjia yule ndama aliyenona.
31
Naye akamwambia: Mwanangu, wewe siku zote uko pamoja nami, nayo yote, niliyo nayo, ni yako.
32
Lakini imetupasa kushangilia na kufurahi, kwani huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka. Alikuwa amepotea, naye ameonekana tena.*
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24