bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 5
Luke 5
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 6 →
1
*Ikawa, kundi la watu lilipomsonga na kulisikia Neno la Mungu, alikuwa amesimama ufukoni pa ziwa la Genesareti,
2
akaona vyombo viwili, vimekaa ufukoni, nao wavuvi walikuwa wameshuka wakiziosha nyavu zao.
3
Ndipo, alipoingia katika chombo kimoja kilichokuwa cha Simoni, akamwomba, akisogeze mbali kidogo hapo ufukoni. Akakaa katika chombo akiwafundisha makundi ya watu.
4
Alipokwisha kusema nao akamwambia Simoni: Peleka chombo kilindini, mzishushe nyavu zetu mvue samaki!
5
Simoni akajibu akisema: Bwana, usiku kucha tumesumbuka kwa kazi, tusipate kitu; lakini kwa agizo lako wewe nitazishusha nyavu.
6
Walipovifanya hivyo wakakamata samaki wengi sana, nyavu zao zikakatikakatika.
7
Ndipo, walipowapungia wenzi wao waliokuwa katika chombo kingine, waje kuwasaidia, nao wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, vikafikia kuzama.
8
Simoni Petero alipoyaona hayo akampigia Yesu magoti, akasema: Ondoka kwangu, Bwana! kwani mimi ni mtu mkosaji.
9
Kwani kituko kilikuwa kimemshika yeye nao wote waliokuwa pamoja naye, kwa hivyo, walivyokamata samaki wengi;
10
akina Yakobo na Yohana, wana wa Zebedeo, ndio waliokuwa wenzake Simoni. Yesu akamwambia Simoni: Usiogope! Toka sasa utakuwa ukivua watu.
11
Walipokwisha kuvipeleka vyombo uvukoni, wakayaacha yote wakamfuata yeye*
12
Ikawa, alipokuwa kule kwenye miji ile, mara kulikuwako mtu aliyeenezwa mwili wote na ukoma. Naye alipomwona Yesu akamwangukia kifudifudi, akamwomba akisema: Bwana, ukitaka waweza kunitakasa.
13
Ndipo, aliponyosha mkono, akamgusa akisema: Nataka, utakaswe. Mara ukoma ukamwondoka.
14
Kisha akamkataza, asimwambie mtu neno, akasema: Uende zako, ujionyeshe kwa mtambikaji, utoe kipaji kwa ajili ya kutakaswa kwako, kama Mose alivyoagiza, kije kinishuhudie kwao!
15
Lakini uvumi wake ukafuliza kuendelea, wakakusanyika makundi ya watu wengi, wamsikilize wakiponywa magonjwa yao.
16
Lakini yeye akajiepua, akaenda mahali palipokuwa pasipo watu, akawapo akiomba.
17
Ikawa siku moja, alipokuwa akifundisha, wakakaa naye Mafariseo na wafunzi wa Maonyo waliokuwa wametoka kila mji wa Galilea na Yudea na Yerusalemu. Nayo nguvu ya Mungu ilikuwa naye ya kuponya wagonjwa.
18
Papo hapo wakaja watu wakileta mtu aliyelala kitandani mwenye ugonjwa wa kupooza. Wakajaribu kumwingiza nyumbani na kumweka mbele yake.
19
Wasipoona pa kumwingizia kwa ajili ya watu wengi wakapanda katika paa la nyumba, wakafumua vigae, wakamshusha hapo pamoja na kitanda chake, wakamweka katikati mbele ya Yesu.
20
Alipoona, walivyomtegemea, akasema: Mwenzangu, umeondolewa makosa yako.
21
Ndipo, waandishi na Mafariseo walipoanza kuwaza wakisema: Nani huyu anayesema maneno ya kumbeza Mungu? Yuko nani awezaye kuondoa makosa? Siye Mungu peke yake tu?
22
Kwa kuyatambua hayo mawazo yao Yesu akajibu akiwaambia: Mnawaza nini mioyoni mwenu?
23
Kilicho chepesi ni kipi? kusema: Umeondolewa makosa yako! au kusema: Inuka, uende?
24
Lakini kusudi mpate kujua, ya kuwa Mwana wa mtu ana nguvu ya kuondoa makosa nchini, akamwambia mwenye kupooza: Nakuambia: Inuka, jitwishe kitanda chako, uende nyumbani kwako!
25
Papo hapo akainuka machoni pao, akajitwisha kitanda, alichokilalia, akaenda nyumbani kwake akimtukuza Mungu.
26
Ndipo, wote walipostuka sana, wakamtukuza Mungu, wakashikwa na woga mwingi wakisema: Utukufu, tuliouona leo, sio wa kuujua.
27
Kisha alipotoka kwenda zake akaona mtoza kodi, amekaa forodhani, jina lake Lawi. Akamwambia: Nifuata!
28
Naye akayaacha yote, akainuka, akamfuata.
29
Kisha Lawi akamfanyia karamu kubwa nyumbani mwake, mkawamo na kundi jingi la watoza kodi na wengine, wakakaa chakulani pamoja nao.
30
Mafariseo na waandishi wao wakanung'unika, wakawaambia wanafunzi wake: Kwa nini mnakula, tena mnakunywa pamoja na watoza kodi na wakosaji?
31
Yesu akajibu akiwaambia: Walio wazima hawapaswi na mganga, ila walio wagonjwa.
32
Sikujia kuwaita waongofu, ila wakosaji, wajute.
33
Kisha wakamwambia: Wanafunzi wa Yohana hukaza kufunga na kuomba, vilevile nao wanafunzi wa Mafariseo, lakini wanafunzi wako hula, hunywa.
34
Yesu akawaambia: Hamwezi kuwafungisha walioalikwa arusini, bwana arusi akingali pamoja nao.
35
Lakini siku zitakuja, watakapoondolewa bwana arusi; siku zile ndipo, watakapofunga.
36
Kisha akawaambia mfano, ya kuwa hakuna mtu akataye kiraka cha nguo mpya na kukitia katika kanzu chakavu. Kama anafanya hivyo, anaikata ile mpya, nacho kiraka cha nguo mpya hakipatani na ile chakavu.
37
Wala hakuna mtu anayetia mvinyo mpya katika viriba vichakavu; kwani akiitia mle, mvinyo mpya itavipasua viriba, nayo yenyewe itamwagika, navyo viriba vitaangamia.
38
Ila mvinyo mpya hutiwa katika viriba vipya.
39
Wala hakuna aliyekunywa mvinyo ya kale, akitaka mpya, kwani husema: ile ya kale ndiyo nzuri.
← Chapter 4
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 6 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24