bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 7
Luke 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 8 →
1
Alipokwisha kuyasema maneno yake yote, watu wakimsikiliza, akaenda, akaingia Kapernaumu.
2
Kukawako mkubwa wa askari mwenye mtumwa, ambaye alipendezwa sana naye; huyu alikuwa mgonjwa wa kufa.
3
Bwana wake aliposikia mambo ya Yesu akatuma kwake wazee wa Wayuda, wamwombe, aje, amponye mtumwa wake.
4
Walipomfikia Yesu wakakaza kumbembeleza wakisema: Amepaswa, umfanyie hivyo;
5
kwani anatupenda sisi taifa letu, hata nyumba ya kuombea ametujengea mwenyewe.
6
Yesu akaenda pamoja nao; alipokuwa mbali kidogo kuifikia ile nyumba, yule mkubwa wa askari akatuma rafiki zake kumwambia: Bwana, usijisumbue! Kwani hainipasi, uingie kijumbani mwangu.
7
Kwa hiyo nami sikujipa moyo wa kukujia mwenyewe. Ila sema neno tu! ndipo, mtoto wangu atakapopona!
8
Kwani nami ni mtu mwenye kuitii serikali, ninao askari chini yangu. Nami nikimwambia huyu: Nenda! basi, huenda; na mwingine: Njoo! huja; nikimwagiza mtumishi wangu: Vifanye hivi! huvifanya.
9
Yesu alipoyasikia hayo akamstaajabu, akaligeukia kundi la watu lililomfuata, akasema: Nawaambiani, hata kwa Waisiraeli sijaona bado mwenye kunitegemea kama huyu.
10
Wale waliotumwa waliporudi nyumbani, wakamkuta yule mtumwa, yuko amepona.
11
*Kisha punde kidogo akashika njia kwenda katika mji, jina lake Naini. Wakafuatana naye wanafunzi wake na kundi la watu wengi.
12
Alipolikaribia lango la mji, panatolewa mfu; huyu alikuwa mwana wa pekee wa mama yake, naye alikuwa mjane. Kwa hiyo watu wengi wa mji ule walikwenda pamoja naye.
13
Bwana alipomwona akamwonea uchungu, akamwambia: Usilie!
14
Alipofika karibu, alishike jeneza, wachukuzi wakasimama. Akasema: Kijana, nakuambia: Inuka!
15
Ndipo, yule mfu alipoinuka, akaanza kusema; kisha akampa mama yake.
16
Woga ukawashika wote, wakamtukuza Mungu wakisema: Mfumbuaji mkuu ametutokea, naye Mungu amewakagua wao wa ukoo wake.
17
Hili neno lake, alilolifanya, likaja kuenea Uyuda wote na nchi zote zilizoko pembenipembeni.*
18
Wanafunzi wake walipomsimulia Yohana hayo yote, akaita wanafunzi wake wawili,
19
akawatuma kwa Bwana, wamwulize: Wewe ndiwe mwenye kuja, au tungoje mwingine?
20
Waume hao walipofika kwake wakasema: Yohana Mbatizaji ametutuma kwako, tuulize: Wewe ndiwe mwenye kuja, au tungoje mwingine?
21
Saa ileile alikuwa akiponya wengi wenye magonjwa na maumivu na pepo wabaya; nao vipofu wengi akawapa kuona.
22
Akajibu akiwaambia: Rudini, mmsimulie Yohana, mliyoyaona nayo mliyoyasikia: vipofu wanaona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanapigiwa mbiu njema.
23
Tena mwenye shangwe ndiye asiyejikwaa kwangu.
24
Wajumbe wa Yohana walipokwisha kwenda zao, akaanza kusema na yale makundi ya watu mambo ya Yohana: Mlipotoka kwenda nyikani mlikwenda kutazama nini? Mlikwenda kutazama utete unaotikiswa na upepo?
25
Au mlitoka kutazama nini? Mlikwenda kutazama mtu aliyevaa mavazi mororo? Tazameni, wanaovaa mavazi yenye utukufu na kula vya mali wamo nyumbani mwa wafalme.
26
Au mlitoka kutazama nini? Mlitaka kuona mfumbuaji? Kweli, nawaambiani: Ni mkuu kuliko mfumbuaji.
27
Huyo ndiye aliyeandikiwa: Utaniona, nikimtuma mjumbe wangu, akutangulie, aitengeneze njia yako mbele yako.
28
Nawaambiani: Miongoni mwao wote waliozaliwa na wanawake hakuna mkuu kuliko Yohana. Lakini aliye mdogo katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko yeye.
29
Watu wote waliomsikia, hata watoza kodi wakauitikia wongofu wake Mungu, wakabatizwa ubatizo wa Yohana.
30
Lakini Mafariseo na wajuzi wa Maonyo waliyatengua, Mungu aliyoyataka, wayafanye, wasibatizwe naye.
31
Basi, wao wa kizazi hiki niwafananishe na nini? Au wamefanana na mtu gani?
32
Wamefanana na watoto wanaokaa sokoni na kuitana wao kwa wao wakisema: Tumewapigia filimbi, nanyi hamkucheza; tena tumewaombolezea, nanyi hamkulia.
33
Kwani Yohana Mbatizaji alikuja, hakula mkate, wala hakunywa mvinyo, nanyi mkasema: Ana pepo.
34
Mwana wa mtu amekuja, akala, akanywa, nanyi mkasema: Tazameni mtu huyu mlaji na mnywaji wa mvinyo, mpenda watoza kodi na wakosaji!
35
Lakini werevu hutokezwa na watoto wake wote kuwa wa kweli.
36
*Fariseo mmoja alipomwalika, ale pamoja naye, akaingia nyumbani mwa yule Fariseo, akakaa chakulani.
37
Mjini mle mlikuwa na mwanamke mkosaji. Naye alipotambua, ya kuwa yumo mwa yule Fariseo, amekaa chakulani, akaja na kichupa cha manukato,
38
akamsimamia nyuma miguuni pake mwenye machozi, akaanza kuyadondosha miguuni pake, akayasugua kwa nywele za kichwani pake, akainonea miguu yake, kisha akaipaka manukato.
39
Yule Fariseo aliyemwalika alipoviona akasema moyoni mwake: Huyu kama angekuwa mfumbuaji, angemtambua mwanamke huyu anayemgusa, kama ni nani, kama ni wa namna gani, kwamba ni mkosaji.
40
Yesu akajibu akimwambia: Simoni, ninalo la kukuambia. Naye alipomwambia: Mfunzi, sema! akasema:
41
Mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili. Wa kwanza deni lake ni shilingi 500, mwenzake 50.
42
Walipokosa vya kulipa, akawaachilia wote wawili, wasilipe. Katika hao atakayempenda kumpita mwenziwe ni yupi?
43
Simoni akajibu akisema: Nadhani, ni yule aliyeachiliwa nyingi. Naye akamwambia: Ulivyolikata shauri hili, ndivyo kweli.
44
Kisha akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni: Unamtazama mwanamke huyu? Nilipoingia nyumbani mwako, hukunipa maji ya kunawa miguu; lakini huyu alinidondoshea machozi miguuni pangu, akayasugua kwa nywele za kichwani pake.
45
Hukuninonea, lakini huyu, tangu nilipoingia, hakuacha kuinonea miguu yangu.
46
Wewe hukunipaka mafuta kichwani, lakini huyu ameipaka miguu yangu manukato.
47
Kwa hiyo nakuambia: Ameondolewa makosa yake yaliyo mengi, kwani mapendo yake ni mengi. Lakini anayeondolewa machache tu, naye mapendo yake ni machache.
48
Kisha akamwambia yule mwanamke: Wewe umeondolewa makosa yako.
49
Ndipo, wale waliokaa chakulani pamoja naye walipoanza kusema mioyoni mwao: Huyu ni nani akiondoa hata makosa?
50
Naye akamwambia yule mwanamke: Kunitegemea kwako kumekuokoa; nenda na kutengemana!*
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24