bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 11
Luke 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 12 →
1
Ikawa alipokuwa mahali akiomba, akiisha, mwanafunzi wake mmoja akamwambia: Bwana, tufundishe hata sisi kuomba, kama naye Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake!
2
Akawaambia: Mnapoomba semeni: Baba yetu ulioko mbinguni, Jina lako litakaswe! Ufalme wako uje! Uyatakayo yatimizwe nchini, kama yanavyotimizwa mbinguni!
3
Tupe kila siku chakula chetu cha kututunza!
4
Tuondolee makosa yetu! Kwani nasi wenyewe humwondolea kila aliyetukosea. Usituingize majaribuni! Ila tuokoe maovuni!
5
*Akawaambia: Kulikuwa na mtu mwenye rafiki; huyu akamwendea usiku wa manane na kumwambia: Rafiki yangu, unikopeshe mikate mitatu!
6
Kwani rafiki yangu aliyechwelewa njiani amenifikia, nami sina cha kumwandalia.
7
Basi, kwenu yule wa ndani atamjibu nini? Atamwambia: Usinisumbue! Kwani mlango umekwisha fungwa, nao watoto wangu wako kitandani pamoja nami; siwezi kuinuka, nikupe?
8
Nawaambiani: Ijapo, asiinuke, ampe, kwa sababu ni rafiki yake, lakini atainuka, ampe yote yampasayo ya mgeni, kwa sababu hana soni ya kuomba.
9
Nami nawaambiani: Ombeni! ndipo, mtakapopewa. Tafuteni! ndipo, mtakapoona. Pigeni hodi! ndipo, mtakapofunguliwa mlango.
10
Kwani kila anayeomba hupewa, naye anayetafuta huona, naye anayepiga hodi hufunguliwa mlango.
11
Tena kwenu yuko baba, mwanawe anapomwomba samaki, ampe nyoka, asimpe samaki?
12
Au anapomwomba yai, ampe nge?
13
Basi, ninyi mlio wabaya mkijua kuwapa watoto wenu vipaji vyema, Baba alioko mbinguni asizidi kuwapa Roho Mtakatifu wanaomwomba?*
14
*Akawa akifukuza pepo aliyekuwa bubu; naye pepo alipotoka, bubu akaanza kusema. Ndipo, makundi ya watu walipostaajabu.
15
Lakini walikuwako waliosema: Nguvu ya Belzebuli, mkuu wa pepo, ndiyo, anayofukuzia pepo.
16
Wengine wakamjaribu wakitaka, afanye kielekezo kitokacho mbinguni.
17
Kwa kuyajua hayo mawazo yao, akawaambia: Kila ufalme unapogombana wao kwa wao huwa mahame tu, nazo nyumba huangukiana.
18
Naye Satani anapojigombanisha mwenyewe, ufalme wake utasimamikaje? Kwani mnasema: Nafukuza pepo kwa nguvu ya Belzebuli.
19
Nami nikiwafukuza pepo kwa nguvu ya Belzebuli, Je? Wana wenu huwafukuza kwa nguvu ya nani? Kwa hiyo hao ndio watakaowaumbua.
20
Lakini mimi nikiwafukuza pepo kwa nguvu ya kidole cha Mungu, ufalme wa Mungu umekwisha kuwafikia ninyi.
21
Mwenye nguvu akililinda boma lake na kushika mata, basi, yaliyo yake yatakaa na kutengemana.
22
Lakini mwenye nguvu kuliko yeye atakapomjia na kumshinda atamnyang'anya mata yake yote yaliyomshikiza, kisha atayagawanya mateka.
23
Asiye wa upande wangu hunikataa; naye asiyekusanya pamoja nami hutapanya.,
24
Pepo mchafu anapomtoka mtu hupita mahali pasipo na maji akitafuta kituo. Asipokiona husema: Nitarudi nyumbani mwangu, nilimotoka.
25
Anapokuja huiona, imefagiwa na kupambwa.
26
Ndipo, anapokwenda kuchukua pepo saba wengine walio wabaya kuliko yeye; nao huingia, wakae humo: hivyo ya mwisho ya mtu yule yatakuwa mabaya kuliko ya kwanza.
27
Ikawa, alipoyasema haya, mwanamke aliyekuwako katika kundi la watu akapaza sauti akimwambia: Lenye shangwe ni tumbo lililokuzaa na maziwa, uliyoyanyonya.
28
Naye akasema: Kweli wenye shangwe ndio wanaolisikia Neno la Mungu na kulishika.*
29
Makundi ya watu walipomkusanyikia, akaanza kusema: Ukoo huu ni ukoo mbaya; wanatafuta kielekezo, lakini hawatapata kielekezo, ila kielekezo cha Yona.
30
Kwani kama Yona alivyowawia watu wa Niniwe kielekezo, ndivyo naye Mwana wa mtu atakavyowawia wao wa ukoo huu kielekezo.
31
Yule mfalme wa kike aliyetoka kusini atawainukia waume wa ukoo huu siku ya hukumu, awaumbue. Kwani yeye alitoka mapeoni kwa nchi, aje kuusikia werevu wa Salomo uliokuwa wa kweli. Tena tazameni, hapa yupo anayempita Salomo!
32
Siku ya hukumu waume wa Niniwe watauinukia ukoo huu, wauumbue; kwani walijuta kwa tangazo la Yona. Tena tazameni, hapa yupo anayempita Yona!
33
Hakuna mwenye kuwasha taa anayeiweka panapofichika au chini ya kapu, ila huiweka juu ya mwango, maana wanaoingia waone mwanga.
34
Taa ya mwili ni jicho lako. Basi, jicho lako liking'aa, nao mwili wako wote unao mwanga. Lakini likiwa bovu, nao mwili wako unayo giza.
35
Kwa hiyo angalia, mwanga uliomo ndani yako usiwe giza!
36
Mwili wako unapokuwa wote unao mwanga, pasiwe upande wenye giza, ndipo, utakapokuwa na mwanga pia, utakuwa kama taa inayokumulikia mwanga wa umeme.
37
Alipokuwa katika kusema, Fariseo akamwalika chakulani. Naye akaingia, akakaa mezani.
38
Fariseo huyo alipoviona akastaajabu, ya kuwa hakunawa kwanza kabla ya kula.
39
Bwana akamwambia: Ninyi Mafariseo, vinyweo na vyano mnaviosha nje, lakini ndani ninyi mmejaa mapokonyo na mabaya.
40
M wajinga, aliyevifanya vya nje hakuvifanya vya ndani navyo?
41
Basi, vile vilivyomo ndani vigawieni watu! Mara vyenu vyote huwa safi.
42
Yatawapata, ninyi Mafariseo, kwani fungu la kumi mnalitolea hata mchicha na nyanya na mboga zo zote. Lakini penye hukumu napo penye upendo wa Mungu mnapapita. Haya yawapasa kuyashika pasipo kuyaacha yale.
43
Yatawapata, ninyi Mafariseo, kwani nyumbani mwa kuombea mnapenda viti vya mbele, tena hupenda kuamkiwa na watu sokoni.
44
Yatawapata, ninyi waandishi na Mafariseo, kwani mmefanana na makaburi yasiyoonekana, ambayo watu hukanyaga juu yao, wasiyajue.
45
Ndipo, mjuzi wa Maonyo alipojibu akimwambia: Mfunzi, ukisema hayo unatutukana hata sisi.
46
Naye akasema: Nanyi wajuzi wa Maonyo yatawapata, kwani mnatwika watu mizigo isiyochukulika, nanyi wenyewe hamwigusi mizigo hiyo hata kwa kidole chenu kimoja tu.
47
Yatawapata ninyi, kwani mnayajenga makaburi ya wafumbuaji, nao baba zenu ndio waliowaua.
48
Hivyo mnayashuhudia matendo ya baba zenu, ya kuwa yanawapendeza; kwani wale waliwaua, nanyi mnawajengea.
49
Kwa sababu hii ujuzi wa Mungu ulisema: Nitatuma kwao wafumbuaji na mitume, wengine wao watawaua, wengine watawafukuza,
50
wao wa kizazi hiki walipishwe damu za wafuambji wote zilizomwagwa tangu hapo, ulimwengu ulipoumbwa,
51
kuanzia damu ya Abeli mpaka kuifikia damu ya Zakaria aliyeuawa katikati ya meza ya Bwana na Nyumba ya Mungu. Kweli nawaambiani: Wao wa kizazi hiki watazilipa.
52
Yatawapata, ninyi wajuzi wa Maonyo, kwani mliutwaa ufunguo wa utambuzi; wenyewe hamkuingia, mkawazuia wao waliotaka kuingia.
53
Alipotoka mle, waandishi na Mafariseo wakaanza kumtunduia sana na kumwuliza maneno mengi
54
na kumnyatia wakiwinda maneno, anayoyasema, kama wataona la kumsuta.
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24