bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 6
Luke 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 7 →
1
Akawa akipita katika mashamba siku ya mapumziko; l nao wanafunzi wake wakakonyoa masuke, wakayafikicha kwa mikono, wakala.
2
Lakini walikuwako Mafariseo waliosema: Mbona mnafanya yaliyo mwiko siku ya mapumziko?
3
Yesu akawajibu akisema: Hamkuvisoma hata hivyo, Dawidi alivyovifanya, walipoona njaa yeye nao wenziwe waliokuwa pamoja naye?
4
Hapo aliingia Nyumbani mwa Mungu, akaitwaa mikate aliyowekewa Bwana, akaila, akawapa nao wenziwe. Nayo kuila ni mwiko, huliwa na watambikaji peke yao.
5
Akawaambia: Mwana wa mtu ni bwana wa siku ya mapumziko.
6
Ikawa siku nyingine ya mapumziko, akaingia nyumbani mwa kuombea, akafundisha. Mle mlikuwa na mtu, ambaye mkono wake wa kuume ulikuwa umekaukiana.
7
Waandishi na Mafariseo wakamtunduia, kama atamponya siku ya mapumziko, waone neno la kumsuta.
8
Naye akayajua mawazo yao, akamwambia yule mwenye mkono uliokaukiana: Inuka, usimame hapa katikati! Akainuka, akasimama hapo.
9
Kisha Yesu akawaambia: Nawauliza ninyi: Iko ruhusa siku ya mapumziko kufanya mema au kufanya maovu? kuponya roho ya mtu au kuiangamiza?
10
Akawatazama wote waliokuwako, akamwambia: Unyoshe mkono wako! Alipovifanya, huo mkono wake ukageuka kuwa mzima.
11
Wale wakawa kama wenye wazimu, wasijue kitu, wakasemezana wao kwa wao, watakayomtendea Yesu.
12
Ikawa siku zile, akatoka kwenda mlimani kuomba; akakesha kucha katika kumwomba Mungu.
13
Kulipokucha, akawaita wanafunzi wake, akachagua miongoni mwao kumi na wawili; ndio aliowapa jina la Mitume.
14
Ni Simoni, aliyempa jina la Petero, na Anderea nduguye, na Yakobo na Yohana na Filipo na Bartolomeo
15
na Mateo na Toma na Yakobo wa Alfeo na Simoni aliyeitwa Zelote
16
na Yuda wa Yakobo na Yuda Iskariota, ndiye aliyekuwa mchongezi.
17
Akashuka pamoja nao, akasimama mahali penye uwanda; hapo palikuwa na kundi zima la wanafunzi wake wengi na watu wengine wengi sana waliotoka Yudea po pote na Yerusalemu na pwani pa Tiro na Sidoni;
18
ndio waliokuja, wamsikilize yeye, waponywe magonjwa yao. Nao waliosumbuliwa na pepo wachafu wakaponywa.
19
Wale watu wote wakatafuta kumgusa tu, kwani nguvu zilizotoka kwake ziliwaponya wote.
20
Kisha akainua macho, akawatazama wanafunzi wake, akasema: Wenye shangwe ni ninyi mlio maskini, maana ufalme wa Mungu ni wenu.
21
Wenye shangwe ni ninyi mnaoona njaa sasa, maana mtashibishwa.
22
Wenye shangwe ni ninyi, watu watakapowachukia na kuwatenga kwao na kuwatukana na kuyakataa majina yenu kwa kuwa mabaya kwa ajili ya Mwana wa mtu.
23
Furahini siku ile na kurukaruka! Kwani tazameni, mshahara wenu ni mwingi mbinguni! Kwani hivyo ndivyo, baba zao walivyowafanyia wafumbuaji.
24
Lakini yatawapata ninyi wenye mali, kwani mmekwisha upata utulivu wenu.
25
Yatawapata nanyi mnaoshiba sasa, kwani mtaona njaa. Yatawapata ninyi mnaocheka sasa, kwani mtasikitika na kulia.
26
Yatawapata ninyi, watu wote wanapowaendea kwa maneno mazuri, kwani hivyo ndivyo, baba zao walivyowafanyia wafumbuaji wa uwongo.
27
Lakini nawaambia ninyi mnaonisikia: Wapendeni adui zenu! Wafanyieni mazuri wanaowachukia!
28
Wabarikini wanaowaapiza! Waombeeni wanaowabeza!
29
Mtu akikupiga kofi shavu moja, umgeuzie la pili, alipige nalo! Mtu anayekunyang'anya kanzu yako, usimkataze kuichukua hata shuka!
30
Kila anayekuomba umpe, naye akunyang'anyaye mali zako, usizitake tena kwake!
31
Kama mnavyotaka, watu wawafanyie ninyi, nanyi mwafanyie vivyo hivyo!
32
Maana mkiwapenda wanaowapendani mnawagawia nini? Kwani nao wakosaji huwapenda wawapendao.
33
Nanyi mnapowafanyia mema wanaowafanyia mema ninyi mnawagawia nini? Nao wakosaji hufanya hivyo hivyo.
34
Nanyi mnapokopesha watu, mnaowangojea kurudishiwa nao, mnawagawia nini? Nao wakosaji huwakopesha wakosaji wenzao, warudishiwe yaleyale.
35
Lakini wapendeni wachukivu wenu! Wafanyieni mema na kuwakopesha, msiowangojea kurudishiwa cho chote! Hivyo mshahara wenu utakuwa mwingi, nanyi mtakuwa wana wake Alioko huko juu. Kwani yeye huwagawia nao wenye majivuno nao wenye ubaya.
36
*Mgeuke kuwa wenye huruma, kama Baba yenu alivyo mwenye huruma!
37
Msiumbue watu, nanyi msije mkaumbuliwa! Msionee watu, nanyi msije mkaonewa! Wafungueni watu, nanyi mje mkafunguliwa!
38
Wapeni watu, nanyi mje mkapewa! Kipimo kizuri kilichoshindiliwa na kutingishwa na kumwagika mtapewa, mfutikie katika nguo zenu. Kwani kipimo, mnachokipimia wengine, ndicho, mtakachopimiwa nanyi tena.
39
Akawaambia mfano: Je? Kipofu aweza kumwongoza kipofu mwenziwe? Hawatatumbukia wote wawili shimoni?
40
Mwanafunzi hampiti mfunzi wake, lakini kila aliyekwisha fundishwa atakuwa, kama mfunzi wake alivyo.
41
Nawe unakitazamiani kibanzi kilichomo jichoni mwa ndugu yako, lakini gogo lililomo jichoni mwako wewe mwenyewe hulioni?
42
Unawezaje kumwambia ndugu yako: Ngoja, ndugu yangu, nikitoe kibanzi kilichomo jichoni mwako? Nalo gogo lililomo jichoni mwako mwenyewe hulioni? Mjanja, kwanza litoe gogo katika jicho lako! Kisha utazame vema, ndivyo upate kukitoa kibanzi kilichomo jichoni mwa ndugu yako!*
43
Kwani hakuna mti mzuri unaozaa matunda maovu; tena hakuna mti mwovu unaozaa matunda mazuri.
44
Kwani kila mti hutambulikana kwa matunda yake mwenyewe. Kwani hawachumi kuyu miibani, wala hawachumi zabibu katika mikunju.
45
Mtu mwema hutoa mema katika kilimbiko chake chema cha moyo, lakini naye mbaya hutoa mabaya katika mabaya yake. Kwani moyo unayoyajaa ndiyo, kinywa cha mtu kinayoyasema.
46
Tena mnaniitiani: Bwana! Bwana! msipoyafanya, ninayoyasema?
47
Kila anayekuja kwangu na kuyasikia maneno yangu na kuyafanyiza, nitawaonyesha, anavyofanana navyo.
48
Amefanana na mtu aliyejenga nyumba, akiichimbia chini vizuri na kuweka msingi mwambani. Maji yalipojaa yakatoka mto, ukapasua penye ile nyumba, lakini haukuweza kuitingisha, kwa kuwa ilikuwa imejengwa vizuri.
49
Lakini anayeyasikia asipoyafanyiza amefanana na mtu aliyejenga nyumba mchangani pasipo msingi. Basi, mto ulipotokea na kupasua hapo, ilianguka papo hapo, kupasuka kwake ile nyumba kukawa kukubwa.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24