bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 22
Luke 22
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 23 →
1
Ikawa karibu sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, inayoitwa Pasaka.
2
Nao watambikaji wakuu na waandishi wakatafuta, ndivyo wapate kumwangamiza. Maana walikuwa wakiwaogopa watu wa kwao.
3
Satani akamwingia Yuda anayeitwa Iskariota, naye alikuwa mwenzao wale kumi na wawili.
4
Akaenda zake, akasemezana nao watambikaji wakuu na wakubwa wa askari, ndivyo apate kumtia mikononi mwao.
5
Wakafurahi, wakapatana naye fedha za kumpa.
6
Ndipo, alipowaitikia waziwazi, akatafuta njia iliyofaa ya kumtoa, watu wasijue.
7
Ilipofika siku ya kula mikate isiyotiwa chachu, ndiyo siku iliyopasa kuchinja kondoo ya Pasaka,
8
akamtuma Petero na Yohana akisema: Nendeni, mtuandalie kondoo ya Pasaka, tupate kuila!
9
Nao wakamwambia: Unataka, tukuandalie wapi?
10
Akawaambia: Tazameni, mtakapoingia mjini mtakutana na mtu anayechukua mtungi wa maji, mfuateni mpaka nyumbani, atakamoingia!
11
Mwambieni mwenye nyumba: Mfunzi anakuuliza: Kiko wapi chumba cha kukaa, ndimo niile kondoo ya Pasaka pamoja na wanafunzi wangu?
12
Ndipo, atakapowaonyesha chumba kikubwa kilichotandikwa, humo tuandalieni!
13
Nao wakaenda, wakaona, kama alivyowaambia, wakaiandaa kondoo ya Pasaka.
14
*Saa ilipofika, akaja kukaa chakulani, nao mitume wakakaa pamoja naye.
15
Akawaambia: Nimetunukia sanasana kuila Pasaka hii pamoja nanyi, nikingali sijateswa bado.
16
Kwani nawaambiani: Sitaila tena, mpaka patakapotimia katika ufalme wa Mungu.
17
Kisha akatwaa kinyweo, akashukuru akisema: Mkitwae hiki, mgawiane wenyewe!
18
Kwani nawaambiani: Tangu sasa sitayanywa tena mazao ya mizabibu, mpaka ufalme wa Mungu utakapokuja.
19
Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema: Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyizeni hivyo, mnikumbuke!
20
Vivyo hivyo akakitwaa nacho kinyweo, walipokwisha kula, akisema: Kinyweo hiki ndicho Agano Jipya katika damu yangu inayomwagwa kwa ajili yenu.*
21
Lakini tazameni, mkono wa mwenye kunichongea upo hapa mezani pamoja nami!
22
Mwana wa mtu anakwenda njia yake, kama alivyotakiwa; lakini yule mtu, ambaye atachongewa naye, atapatwa na mambo.
23
Nao wakaanza kuulizana wao kwa wao: Kwetu sisi yuko nani atakayelifanya jambo hilo?
24
Kukawa mabishano kwao ya kwamba: Kati yetu ni nani aliye mkubwa?
25
Naye akawaambia: Wafalme wa mataifa huwatawala, nao wenye nguvu kwao huitwa mabwana wakubwa,
26
lakini ninyi msiwe hivyo! Ila aliye mkubwa kwenu na awe kama aliye mdogo, naye mwenye kuongoza na awe kama mwenye kutumika!
27
Kwani aliye mkubwa ni yupi? Anayekaa chakulani au anayetumika? Si yule anayekaa chakulani? Lakini mimi kati yenu niko kama mwenye kutumika.
28
Nanyi ndinyi mlioandamana nami katika kujaribiwa kwangu.
29
Kwa hiyo mimi nawawekea ninyi ufalme, kama Baba yangu alivyoniwekea mimi,
30
mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu, nanyi mtakaa katika viti vya kifalme, myahukumu hayo mashina kumi na mawili ya Isiraeli.
31
Simoni, Simoni, tazama, Satani amewataka ninyi, awapepete, kama wanavyopepeta ngano!
32
Lakini mimi nimekuombea, kunitegemea kwako kusikome. Nawe hapo, utakapogukia, uwatie ndugu zako nguvu!
33
Naye akamwambia: Bwana, nikiwa pamoja nawe niko tayari kwenda, ijapo iwe kifungoni, hata kufani.
34
Naye akasema: Nakuambia, Petero: Jogoo hatawika leo, usipokwisha kunikana mara tatu kwamba: Simjui.
35
Akawauliza: Nilipowatuma pasipo mfuko na mkoba na viatu, kulikuwako kitu, mlichokikosa? Wakasema: Hakuna hata kimoja.
36
Akawaambia: Lakini sasa mwenye mfuko na autwae, na mkoba vilevile, naye mwenye kuukosa na auze nguo yake, anunue upanga!
37
Kwani nawaambiani: Lile lililoandikwa sharti litimie kwangu mimi la kwamba: Akahesabiwa kuwa mwenzao wapotovu; kwani naliyoandikiwa hutimia.
38
Nao wakasema: Bwana, tazama, hapa ziko panga mbili! Naye akawaambia: Basi.
39
*Kisha akatoka, akaenda mlimani pa michekele, kama alivyozoea, nao wanafunzi wake wakamfuata.
40
Alipofika pale akawaambia: Mwombe, msije kuingia majaribuni!
41
Akaepukana nao na kuja mbali kidogo kama hapo, mtu anapotupa jiwe, akapiga magoti, akaomba akisema:
42
Baba, ukitaka kipitishe kinyweo hiki, nisikinywe! Lakini yasifanyike, niyatakayo mimi, ila yafanyike uyatakayo wewe!
43
Ndipo, malaika alipomtokea toka mbinguni, akamtia nguvu.
44
Kisha akawa akigombana na kifo, kwa hiyo akajihimiza kuomba, nalo jasho lake likawa kama matone ya damu yaliyodondoka chini.
45
Alipoinuka katika kuomba, akawajia wanafunzi, akawakuta, wamelala usingizi kwa sikitiko,
46
akawaambia: Mbona mmelala usingizi? Inukeni, mwombe, msije kuingia majaribuni!*
47
Angali akisema, mara wakaja kundi la watu, mmoja wao wale kumi na wawili, jina lake Yuda, akiwatangulia, akamkaribia Yesu kumnonea.
48
Yesu akamwambia: Yuda, unamchongea Mwana wa mtu kwa kumnonea?
49
Nao waliokuwa pamoja naye walipoyaona yatakayokuwapo, wakasema: Bwana, tuwapige kwa upanga?
50
Mwenzao mmoja akampiga mtumwa wa mtambikaji mkuu, akamkata sikio la kuume.
51
Lakini Yesu akajibu akisema: Waacheni, wamalize! Akamgusa sikio, akamponya.
52
Kisha Yesu akawaambia waliomjia, wale watambikaji wakuu na wakuu wa Patakatifu na wazee: Mmetoka wenye panga na rungu, kama watu wanavyomwendea mnyang'anyi.
53
Kila siku nilikuwa nanyi hapo Patakatifu, lakini hamkunyosha mikono, mnikamate. Lakini hii ndiyo saa yenu, ndipo, giza linaposhikia nguvu.
54
*Walipokwisha kumkamata, wakampeleka, wamwingize nyumbani mwa mtambikaji mkuu. Lakini Petero akafuata mbalimbali.
55
Walipowasha moto katikati ya ua na kukaa pamoja, naye Petero akaja kukaa katikati yao.
56
Kijakazi alipomwona, akikaa penye mwangaza wa moto, akamkazia macho, akasema: Hata huyu alikuwa pamoja naye.
57
Akakana akisema: Simjui, mama.
58
Punde kidogo mwingine akamwona, akasema: Wewe nawe u mwenzao. Lakini Petero akasema: Mwenzangu, siye mimi.
59
Saa moja ilipopita, mwingine akakaza kusema: Kweli hata huyu alikuwa pamoja naye, kwani ni Mgalilea.
60
Lakini Petero akasema: Mwenzangu, sijui, unavyosema. Angali akisema, papo hapo jogoo akawika.
61
Ndipo, Bwana alipomgeukia Petero, amtazame; hapo Petero akalikumbuka lile neno la Bwana, kama alivyomwambia: Jogoo atakapokuwa hajawika leo, utakuwa umenikana mara tatu.
62
Akatoka nje, akalia sana kwa uchungu.*
63
*Wale waume waliomshika Yesu wakamfyoza na kumpiga,
64
wakamfunika uso, wakamwuliza wakisema: Fumbua! Ni nani aliyekupiga?
65
Hata masimango mengine mengi wakasema na kumtukana.
66
Kulipokucha, wakakusanyika wazee wa kwao na watambikaji wakuu na waandishi, wakampeleka barazani kwa wakuu wao wote.
67
Wakasema: Tuambie, kama wewe ndiwe Kristo! Akawaambia: Nikiwaambia, hamtanitegemea;
68
lakini nikiwauliza, hamtanijibu, wala hamtanifungua.
69
Lakini tangu sasa Mwana wa mtu atakuwa amekaa kuumeni kwa nguvu ya Mungu.
70
Ndipo, waliposema wote: Je? Ndiwe mwana wa Mungu? Naye akawaambia: Ninyi mnasema, kwani nimi ndiye.
71
Nao wakasema: Ushuhuda tunautakia nini tena? Kwani wenyewe tumevisikia, anavyosema.*
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 23 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24