bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 21
Luke 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 22 →
1
Alipoinua macho akaona, wenye mali walivyotia sadaka zao katika sanduku ya vipaji.
2
Akaona hata mwanamke mjane aliyekuwa mkiwa, alivyotia mle visenti viwili.
3
Ndipo, aliposema: Kweli nawaambiani: Huyu mjane mkiwa ametia mengi kuliko wote.
4
Kwani hao wote walitoa mali katika mali zao nyingi, wakazitia penye sadaka, lakini huyu kwa ukiwa wake amevitoa vyote, alivyokuwa navyo, ndivyo vilivyomlisha.
5
Wengine waliposema, Patakatifu palivyokuwa pamepambwa na mawe mazuri na mapambo mengine, ndipo, aliposema:
6
Je? Mwayatazama haya? Siku zitakuja, ambapo halitaachwa hata jiwe moja juu ya jiwe lenziwe lisiloporomoshwa chini.
7
Wakamwuliza wakisema: Mfunzi, hayo yatakuwapo lini? Tena kielekezo ni nini, hayo yatakapotimia?
8
Naye akasema: Angalieni, msipotezwe! Kwani wengi watakuja kwa Jina langu na kusema: Mimi ndiye, nazo siku zimekwisha kufika. Msiwafuate hao!
9
Nanyi mtakaposikia vita na mainukiano, msitukutike! Kwani hayo sharti yawepo kwanza; lakini mwisho hauji upesi.
10
Ndipo alipowaambia: Watainukiana taifa na taifa, tena wafalme na wenzao wafalme.
11
Mahali penginepengine patakuwa na matetemeko makuu, pengine na kipindupindu, pengine na njaa. Hata vielekezo vikubwa vitatokea mbinguni vya kuogofya.
12
Lakini hayo yote yatakapokuwa hayajatimia bado, watawanyoshea mikono, wawakamate na kuwakimbiza, wawapeleke nyumbani mwa kuombea namo mabomani, wawaweke mbele yao wafalme na mabwana wakubwa kwa ajili ya Jina langu.
13
Hayo yatawapata ninyi, mje kunishuhudia kwao.
14
Jueni, nguvu imo mioyoni mwenu, msianze kuyahangaikia maneno ya kujikania!
15
Kwani mimi nitawapa vinywani maneno yenye werevu wa kweli; nao wabishi wenu wote hawataweza kuyabisha wala kuyakana.
16
Nanyi mtatolewa na wazazi na ndugu na wenzenu wa ukoo na rafiki; wengine wenu watawaua,
17
nanyi mtakuwa mmechukiwa na watu wote kwa ajili ya Jina langu.
18
Lakini hata unywele mmoja hautawapotelea vichwani,
19
ila kwa kuvumilia mtazikomboa roho zenu.
20
Lakini hapo mtakapoona, mji wa Yerusalemu ukizungukwa na vikosi, ndipo mjue, ya kuwa kuangamizwa kwake kumetimia.
21
Siku zile watakaokuwako Yudea na wakimbilie milimani! Nao watakaokuwamo mle mjini watoke! Nao watakaokuwako shambani wasiuingie tena!
22
Kwani siku hizo zitakuwa za malipizo, yote yaliyoandikwa yapate kutimizwa.
23
Lakini watakaoona vibaya zaidi ndio wenye mimba na wenye kunyonyesha siku zile. Kwani itakuwa kondo kubwa katika nchi, makali yatakapowatokea watu wa kabila hili:
24
wengine wataanguka kwa ukali wa panga, wengine watatekwa na kutawanyishwa kwenye mataifa yote. Namo Yerusalemu mtakanyagwa na wamizimu, mpaka siku za wamizimu zitakapotimizwa.
25
*Kutakuwa na vielekezo vya jua na vya mwezi na vya nyota. Huku nchini watu wa mataifa yote watapotelewa na mioyo wasipojua maana, mawimbi ya bahari yatakapokaza kuvuma na kutukutika.
26
Ndipo, watu watakapozimia kwa woga na kwa kuyangoja mambo yatakayopajia pote, wanapokaa, kwani hata nguvu za mbingu zitatukutishwa.
27
Hapo ndipo, watakapomwona Mwana wa mtu, anavyokuja katika wingi mwenye nguvu na utukufu mwingi.
28
Lakini hayo yatakapoanza kuwapo, myaelekeze macho yenu mbinguni na kuviinua vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu utakuwa uko karibu!
29
Kisha akawaambia mfano: Utazameni mkuyu na miti yote!
30
Mnapoiona, ikichipua, mnatambua wenyewe, ya kuwa siku za vuli zimekwisha kuwa karibu.
31
Vivyo hivyo nanyi mtakapoyaona hayo, yakiwapo, tambueni, ya kuwa ufalme wa Mungu umewafikia karibu!
32
Kweli nawaambiani: Kizazi hiki hakitakoma, mpaka yatakapokuwapo yote.
33
Mbingu na nchi zitakoma, lakini maneno yangu hayatakoma.
34
Lakini jilindeni, ulafi na ulevi na masumbuko ya nchini yasiwalemee mioyoni, siku ile isiwajie, msipoingoja!
35
Kwani kama mtego unavyonasa, itawajia wote po pote, wanapokaa nchini.
36
Kesheni siku zote na kuomba, mpate nguvu za kuyakimbia hayo yote, yatakayokuwapo, msimamishwe mbele ya Mwana wa mtu!*
37
Akawa kila siku akifundisha Patakatifu, lakini usiku hutoka na kulala kwenye mlima unaoitwa Wa Michekele.
38
Nao watu wote walikuwa wakimwendea asubuhi pale Patakatifu, wamsikilize.
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24