bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 3
Luke 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 4 →
1
Mwaka wa 15 wa kutawala kwake Kaisari Tiberio Pontio Pilato alikuwa mtawala nchi ya Yudea, naye Herode alikuwa mfalme wa Galilea, naye Filipo, ndugu yake, alikuwa mfalme wa Iturea na wa nchi ya Tarakoniti, naye Lisania alikuwa mfalme wa Abilene,
2
tena Ana na Kayafa walikuwa watambikaji wakuu. Hapo ndipo, neno la Mungu lilipomjia Yohana, mwana wa Zakaria, huko nyikani.
3
Akaenda katika nchi zote za kando ya Yordani, akatangaza ubatizo wa kujutisha, wapate kuondolewa makosa.
4
Ikawa, kama ilivyoandikwa kitabuni mwa maneno ya mfumbuaji Yesaya: Iko sauti ya mtu apigaye mbiu nyikani: Itengenezeni njia ya Bwana! Yanyosheni mapito yake!
5
Vibonde vyote vifukiwe, navyo vilima vyote na vichuguu vyote vichimbuliwe! Napo palipopotoka panyoshwe, napo penye mashimo pawe njia za sawasawa,
6
wote wenye miili wauone wokovu wake Mungu.
7
Akawaambia makundi ya watu waliotokea, wabatizwe naye: Ninyi wana wa nyoka, nani aliwaambia ninyi, ya kuwa mtayakimbia makali yatakayokuja?
8
Tendeni mazao yaliyo ya kujuta kweli! Msianze kusema mioyoni mwenu: Tunaye baba yetu, ndiye Aburahamu! Kwani nawaambiani: Katika mawe haya ndimo, Mungu awezamo kumwinulia Aburahamu wana.
9
Miti imekwisha wekewa mashoka mashinani, kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa, utupwe motoni.
10
Yale makundi ya watu wakamwuliza wakisema: Basi, tufanye nini?
11
Akajibu akiwaambia: Mwenye nguo mbili amgawie mwenziwe asiye nayo, naye mwenye vyakula na afanye vilevile!
12
Watoza kodi nao walipokuja, wabatizwe, wakamwuliza: Mfunzi, tufanye nini?
13
Naye akawaambia: Msitoze kuvipita hivyo, mlivyoagizwa!
14
Walipomwuliza nao askari wakisema: Nasi tufanye nini? akawaambia: Msimwendee mtu kwa nguvu wala kwa ukorofi, tena mtoshewe na mishahara yenu!
15
Watu walipokuwa wakingoja, vya Yohana vitakapotokea wazi, wote waliwaza mioyoni mwao kwamba: Yeye labda ni Kristo; ndipo, Yohana
16
aliposema akiwaambia wote: Mimi nawabatiza kwa maji; lakini anakuja aliye na nguvu kunipita mimi, nami sifai kumfungulia kanda za viatu vyake. Yeye atawabatiza katika Roho takatifu na katika moto.
17
Ungo wa kupepetea umo mkononi mwake, apafagie pake pa kupuria ngano; ngano atazikusanya, aziweke chanjani mwake, lakini makapi atayachoma kwa moto usiozimika.
18
Hivyo aliwapigia watu mbiu njema na kuwaonya hata mengine mengi.
19
Lakini mfalme Herode alipoumbuliwa naye kwa ajili ya Herodia, mke wa nduguye, na kwa ajili ya mabaya yote, Herode aliyoyatenda,
20
akayaongeza mabaya yake na kumfunga Yohanba kifungoni.
21
Lakini watu wote walipokuwa wakibatizwa, Yesu anaye alipobatizwa, ikawa, alipokuwa katika kuomba, ndipo, mbingu zilipofunuka,
22
Roho Mtakatifu akamshukia mwenye mwili kama wa njiwa, sauti ikatoka mbinguni: Wewe ndiwe mwanangu mpendwa, nimependewa na wewe.
23
Yesu alipoianza kazi yake alikuwa wa miaka kama 30. Akadhaniwa kuwa mwana wa Yosefu, wa Eli,
24
wa Matati, wa Lawi, wa Melki, wa Yanai, wa Yosefu,
25
wa matatia, wa Amosi, wa Nahumu, wa Esili, wa Nagai,
26
wa Mahati, wa Matatia, wa Simei, wa Yoseki, wa Yoda,
27
wa Yohana, wa Resa, wa Zerubabeli, wa Saltieli, wa Neri,
28
wa Melki, wa Adi, wa Kosamu, wa Elmadamu, wa Heri,
29
wa Yesu, wa Eliezeri, wa Yorimu, wa Matati, wa Lawi,
30
wa Simeoni, wa Yuda, wa Yosefu, wa Yonamu, wa Eliakimu,
31
wa Melea, wa Mena, wa Matata, wa Natani, wa Dawidi,
32
wa Isai, wa Obedi, wa Boazi, wa Salmoni, wa Nasoni,
33
wa Aminadabu, wa Ramu, wa Hesiromu, wa Peresi, wa Yuda,
34
wa Yakobo, wa Isaka, wa Aburahamu, wa Tera, wa Nahori,
35
wa Serugi, wa Ragau, wa Pelegi, wa Eberi, wa Sala,
36
wa Kenani, wa Arpakisadi, wa Semu, wa Noa, wa Lameki,
37
wa Metusela, wa Henoki, wa Yaredi, wa Mahalaleli, wa Kenani,
38
wa Enosi, wa Seti, wa Adamu wa Mungu.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24