bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 2
Luke 2
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 3 →
1
*Ikawa siku zile, amri ikitoka kwa Kaisari Augusto, walimwengu wote waandikiwe kodi;
2
huko kuandikwa kulikuwa kwa kwanza, kukawa siku zile, Kirenio alipotawala Ushami.
3
Ndipo, watu wote waliposhika njia za kwenda kuandikiwa kodi, kila mtu akaenda mjini kwao.
4
Yosefu naye akaondoka Galilea katika mji wa Nasareti kwenda Yudea katika mji wa Dawidi unaoitwa Beti-Lehemu, kwa kuwa yeye alikuwa wa mlango na wa udugu wa Dawidi.
5
Akaenda pamoja na mkewe Maria aliyeposwa naye, waandikiwe kodi; naye alikuwa ana mimba.
6
Ikawa, walipokaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia.
7
Akamzaa mwana wake wa kwanza, ni wa kiume, akamvika nguo za kitoto, akamlaza waliamo ng'ombe, kwani hawakupata pengine nyumbani mwa wageni.
8
Kulikuwa na wachungaji katika nchi ileile, walilala malishoni na kulilinda kundi lao kwa zamu ya usiku.
9
Ndiko, malaika wa Bwana alikowatokea, nao utukufu wa Bwana ukawamulikia po pote, wakashikwa na woga mwingi.
10
Lakini malaika akawaambia: Msiogope! kwani tazameni, ninawapigia mbiu njema yenye furaha kuu itakayowajia watu wote.
11
Kwani mmezaliwa leo mwokozi wenu katika mji wa Dawidi, ndiye Bwana Kristo.
12
Nacho kielekezo chenu ni hiki: mtaona kitoto kichanga, kimevikwa nguo za kitoto, kimelazwa waliamo ng'ombe.
13
Mara wakawa pamoja na yule malaika wingi wa vikosi vya mbinguni, wakamsifu Mungu wakiimba:
14
Utukufu ni wa Mungu mbinguni juu, nchini uko utengemani kwa watu wampendezao.
15
*Ikawa, malaika walipoondoka kwao kwenda mbinguni, wachungaji wakasemezana wao kwa wao: Haya! Twende, tufike hata Beti-Lehemu, tulitazame jambo hilo lililokuwapo, Bwana alilotutambulisha!
16
Wakaenda mbio, wakawakuta, akina Maria na Yosefu na kitoto kichanga, kimelazwa waliamo ng'ombe.
17
Walipokwisha kumwona wakalitambulisha lile neno, waliloambiwa na kitoto hiki.
18
Ndipo, wote walioyasikia walipoyastaajabu, waliyoambiwa na wachungaji.
19
Lakini Maria akayashika maneno hayo yote, akayaweka moyoni mwake na kuyawaza.
20
Kisha wachungaji wakarudi wakimtukuza Mungu na kumsifu kwa yote, waliyoyasikia, kwani waliona, ni vivyo, kama walivyoambiwa.*
21
*Siku nane za kumtahiri zilipotimia, akaitwa jina lake YESU, lililotajwa na malaika, mama yake alipokuwa hajapata mimba yake.*
22
*Siku zao zilipotimia za weuo, aliouagiza Mose, wakampeleka Yerusalemu, wamtokeze kwake Bwana.
23
Ndivyo, ilivyoandikwa katika Maonyo ya Bwana: Kila mtoto mume atakayezaliwa wa kwanza na mama yake aitwe mtakatifu wa Bwana!
24
Wakatoa vipaji vya kumkomboa, kama ilivyoagizwa katika Maonyo ya Bwana, hua wawili au makinda mawili ya njiwa manga.
25
*Huko Yerusalemu kulikuwa na mtu, jina lake Simeoni. Mtu huyo alikuwa mwongofu mwenye kumcha Mungu, akaungoja utulivu wa Isiraeli; nayo Roho takatifu ilikuwa naye.
26
Huyo alikuwa amefumbuliwa na Roho Mtakatifu kwamba: Hutaona kufa usipomwona kwanza Kristo wa Bwana.
27
Basi, akaja Patakatifu kwa kuongozwa na Roho. Wazazi walipoingia na mtoto Yesu, wamfanyie, kama walivyozoezwa na Maonyo,
28
mwenyewe akampokea mikononi pake, akamtukuza Mungu akisema:
29
Bwana, sasa unampa mtumwa wako ruhusa, aende zake na kutulia, kama ulivyosema.
30
Kwani macho yangu yameuona wokovu wako,
31
ulioutengeneza machoni pa makabila yote:
32
ni mwanga wa kuwamulikia wamizimu, ukoo wako wa Isiraeli utukuzwe.*
33
Baba yake na mama yake walipokuwa wakiyastaajabu aliyosemewa,
34
Simeoni akawabariki, akamwambia Maria, mama yake: Tazama, huyu ndiye aliyewekewa, wengi walio Waisiraeli waangushwe naye, nao wengine wengi wainuliwe naye; tena amewekewa kuwa kielekezo kinachobishiwa.
35
Nawe wewe upanga utakuchoma moyoni, kusudi mawazo yao wengi yaliyomo mioyoni mwao yafunuke.
36
Kukawa na mfumbuaji wa kike, jina lake Ana, binti Fanueli, wa shina la Aseri. Huyo miaka yake ilikuwa mingi sana; alikuwa amekaa pamoja na mumewe miaka saba baada ya kuwa manamwali.
37
Tena siku hizo alikuwa mjane mwenye miaka 84, lakini hakuondoka Patakatifu akimtumikia Mungu usiku na mchana kwa kufunga na kuombea watu.
38
Naye akawajia saa ileile, akamshukuru Mungu waziwazi, akawaambia mambo ya huyo mtoto wote walioungoja ukombozi wa Yerusalemu.
39
Walipokwisha kuyamaliza yote yaliyoagizwa na Maonyo ya Bwana wakarudi Galilea mjini kwao Nasareti.
40
Lakini yule mtoto akakua, akapata nguvu ya Roho na werevu wote wa kweli, naye Mungu akamgawia mema yake.*
41
*Wazazi wake huenda Yerusalemu kila mwaka kula sikukuu ya Pasaka.
42
Naye alipopata miaka 12, wakakwea naye, kama walivyozoea kwenye hiyo sikukuu.
43
Zile siku zilipomalizika, wakarudi, lakini mtoto wao Yesu akasalia Yerusalemu, wazazi wake wasijue.
44
Wakadhani, yumo katika wenzake wa njiani. Wakaenda mwendo wa siku moja, kisha wakamtafuta kwa ndugu zao na kwa wenzi wao.
45
Wasipomwona wakarudi Yerusalemu wakimtafuta.
46
Siku tatu zilipopita, wakamwona Patakatifu, amekaa katikati ya wafunzi akiwasikiliza na kuulizana nao,
47
nao wote waliomsikia wakaustukia sana ujuzi wake wa kujibu.
48
Walipomwona wakashangaa, mama yake akamwmbia: Mwanangu, mbona umetufanyia hivyo? Tazama, baba yako na mimi tumekutafuta kwa uchungu.
49
Akawaambia: Mwanitafutiani? Hamkujua, ya kuwa imenipasa kuwa mwake Baba yangu?
50
Wao hawakulijua maana neno hili, alilowaambia.
51
Kisha akatelemka pamoja nao, akafika Nasareti, akakaa na kuwatii. Naye mama yake akayashika maneno hayo yote moyoni mwake.
52
Yesu akakua na kuongezeka werevu wa kweli, mpaka akiwa mtu mzima, tena akawa akimpendeza Mungu na watu.*
← Chapter 1
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 3 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24