bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 20
Luke 20
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 21 →
1
Ikawa siku moja, alipofundisha watu hapo Patakatifu na kuipiga hiyo mbiu njema, wakamwinukia watambikaji wakuu na waandishi na wazee,
2
wakamwambia wakisema: Utuambie: Hayo unayafanya kwa nguvu gani? au ni nani aliyekupa nguvu hii?
3
Akajibu akiwaambia: Hata mimi nitawauliza neno moja, mnijibu:
4
Ubatizo wake Yohana ulitoka mbinguni au kwa watu?
5
Wakafikiri mioyoni mwao kwamba: Tukisema: Ulitoka mbinguni, atatuuliza: Mbona hamkumtegemea?
6
Lakini tukisema: Ulitoka kwa watu, watu wote watatupiga mawe. Kwani walikuwa wametambua kweli kwamba: Yohana ni mfumbuaji.
7
Kwa hiyo wakajibu: Hatujui, ulikotoka.
8
Ndipo, Yesu alipowaambia: Basi, hata mimi siwaambii nguvu inayonifanyisha hayo.
9
Akaanza kuwatolea watu mfano huu: Mtu alipanda mizabibu, akaipangisha wakulima, kisha akaenda katika nchi nyingine kukaa siku nyingi.
10
Siku zilipotimia, akatuma mtumwa kwa wale wakulima, wampe matunda ya mizabibu. Lakini wakulima wakampiga, wakamrudisha mikono mitupu.
11
Akaongeza kutuma mtumwa mwingine. Naye wale wakampiga na kumtukana, wakamrudisha mikono mitupu.
12
Akaongeza kumtuma wa tatu. Naye wale wakamtia vidonda na kumfukuza.
13
Ndipo, mwenye mizabibu aliposema: Nifanyeje? Nitamtuma mwanangu mpendwa, labla huyo watamcha.
14
Lakini wakulima walipomwona wakafikiri na kusemezana wao kwa wao: Huyu ndiye kibwana; na tumwue, urithi wake uwe wetu!
15
Kwa hiyo wakamsukumasukuma mpaka nje ya mizabibu, wakamwua. Basi, mwenye mizabibu atawafanyia nini?
16
Atakuja na kuwangamiza wakulima hao nayo mizabibu atawapa wengine. Wao waliosikia wakasema: Yasiwe hayo!
17
Naye akawatazama, akasema: Basi, maana ya neno lililoandikwa ni nini? Hilo la kwamba: Jiwe, walilolikataa waashi, hilihili limekuwa jiwe la pembeni?
18
Kila atakayeanguka juu ya jiwe lile atapondeka; naye litakayemwangukia, litambana tikitiki.
19
Saa ileile waandishi na watambikaji wakuu wakatafuta kumkamata, lakini waliliogopa lile kundi la watu; kwani walitambua, ya kuwa amewasemea wao wenyewe mfano lhuo.
20
Wakamtunduia, wakatuma wapelelezi, wafanye ujanja wa kuwa kama waongofu, maana wamnase kwa maneno yake, wapate kumpeleka bomani kwenye nguvu ya mtawala nchi.
21
Nao wakamwuliza wakisema: Mfunzi, tumekujua, ya kuwa unasema ya kweli na kuyafundisha, hutazami nyuso za watu, nayo njia ya Mungu unaifundisha, ilivyo kweli.
22
Sisi tuko na ruhusa ya kumtolea Kaisari kodi, au haiko?
23
Kwa kuujua werevu wao mbaya, akawaambia:
24
Nionyesheni shilingi! Ina chapa na maandiko ya nani? Nao wakasema: Yake Kaisari.
25
Ndipo, alipowaambia: Basi, yaliyo yake Kaisari mtoleeni Kaisari, naye Mungu yaliyo yake Mungu!
26
Hivyo hawakuweza kumnasa kwa maneno yake mbele za watu, wakamstaajabu, alivyojibu, wakanyamaza.
27
Kulikuwa na Masadukeo wanaobisha kwamba: Hakuna ufufuko; wakamjia, wakamwuliza wakisema:
28
Mfunzi, Mose alitundikia: Mtu akifiwa na mkubwa wake aliyekuwa na mkewe pasipo kuwa na mwana, nduguye amchukue huyo mke, amzalie mkubwa wake mwana.
29
Kulikuwa na waume saba walio ndugu.
30
Wa kwanza akaoa mke, akafa pasipo kuwa na mwana.
31
Naye wa pili, kisha wa tatu akamchukua yule mwanamke; vivi hivi hata wale saba, hawakuacha wana walipokufa.
32
Mwisho akafa naye mwanamke.
33
Basi, katika ufuko huyo mwanamke atakuwa mke wa yupi wa hao? Kwani wote saba walikuwa naye yule mwanamke.
34
Yesu akawaambia: Wana wa dunia hii huoa, tena huolewa.
35
Lakini wale watakaopewa kuifikia dunia ile na kufufuliwa katika wafu hawataoa, wala hawataolewa.
36
Kwani hawataweza kufa tena, maana watafanana na malaika, watakuwa wana wa Mungu kwa hivyo, walivyofufuka.
37
Lakini kwa ajili ya wafu, kwamba wafufuliwa, hata Mose alivifumbua kidogo hapo kichakani alipomwita Bwana: Mungu wa Aburahamu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.
38
Lakini Mungu siye wa wafu, la wao walio hai; kwani kwake wote huishi.
39
Kulikuwa na waandishi waliojibu wakisema: Mfunzi, umesema vema.
40
Kwani hawakujipa moyo tena kumwuliza neno.
41
Kisha akawaambia: Husemaje, ya kuwa Kristo ni mwana wa Dawidi?
42
Kwani Dawidi mwenyewe asema katika kitabu cha Mashangilio: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti kuumeni kwangu,
43
mpaka niwaweke adui zako chini miguuni pako!
44
Basi, Dawidi akimwita Bwana, anakuwaje tena mwana wake?
45
Akawaambia wanafunzi, watu wote waliposikia:
46
Jilindeni kwa ajili ya waandishi wanaotaka kutembea wenye kanzu ndefu, tena hupenda kuamkiwa na watu sokoni! Namo nyumbani mwa kuombea hupenda viti vya mbele, hata wakialikwa chakulani hupenda kukaa penye wakuu.
47
Huzila nyumba za wajane, wakijitendekeza, kama wanakaza kuwaombea. Walio hivyo mapatilizo yao yatakuwa kuliko ya wengine.
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 21 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24