bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 10
Luke 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 11 →
1
Kisha Bwana akachagua wengine 70, akawatanguliza mbele yake wawiliwawili, waingie kila mji na kila mahali, alipotaka kwenda mwenyewe.
2
Naye akawaambia: Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Mwombeni mwenye mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake!
3
Nendeni! Tazameni, nawatuma ninyi, mwe kama wana kondoo walio katikati ya mbwa wa mwitu!
4
Msitwae mfuko wala mkoba wala viatu! Tena msiamkiane na mtu njiani!
5
Lakini nyumbani mo mote, mtakamoingia, kwanza semine: Nyumba hii itengemane!
6
Itakapokuwa, yumo mwenye kutengemana, utengemano wenu utamkalia. Lakini kama hatakuwamo, utawarudia ninyi.
7
Namo nyumbani mlemle mkaeni mkila, mkinywa mnavyopewa! Kwani mtenda kazi hupaswa na kupewa mshahara wake. Msizunguke nyumba kwa nyumba!
8
Namo mjini mo mote, mtakamoingia, nao wakiwapokea, vileni, mnavyoandaliwa!
9
Waponyeni wagonjwa waliomo nakuwaambia: Ufalme wa Mungu umewakaribia!
10
Lakini mjini mo mote, mtakamoingia, wasipowapokea, tokeni Lakini mjini mo mote, mtakamoingia, wasipowapokea, tokeni mwao, mwende uwanjani mkisema:
11
Hata mavumbi ya mji wenu yaliyotushika miguuni twawakung'utia ninyi; lakini haya yatambueni: Ufalme wa Mungu umekaribia!
12
Nawaambiani: Siku ile mji wa Sodomu utapata mepesi kuliko mji ule.
13
Yatakupata, wewe Korasini! Yatakupata, wewe Beti-Saida! Kwani ya nguvu yaliyofanyika kwenu kama yangalifanyika Tiro na Sidoni, wangalijuta kale na kujivika magunia na kujikalisha majivuni.
14
Lakini penye hukumu miji ya Tiro na Sidoni itapata machungu yaliyoi madogo kuliko yenu.
15
Nawe Kapernaumu, hukupazwa mpaka mbinguni? Utatumbukia mpaka kuzimuni.
16
Anayewasikia ninyi hunisikia mimi. Naye anayewatengua ninyi hunitengua mimi. Naye anayenitengua mimi humtengua naye aliyenituma.
17
*Wale 70 wakarudi wenye furaha, wakasema: Bwana, hata pepo hututii kwa Jina lako.
18
Ndipo, alipowaambia: Nalimwona Satani, akianguka kama umeme toka mbinguni.
19
Tazameni, nimewapa nguvu za kukanyaga nyoka na nge, mshinde uwezo wote wa yule mchukivu, tena hakuna kitu kitakachowapotoa.
20
Lakini msiyafurahie hayo, ya kuwa pepo huwatii, ila yafurahieni, ya kuwa mmeandikwa majina yenu mbinguni!*
21
Saa ileile Roho Mtakatifu akamshangiliza, naye akasema: Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwani hayo umewaficha werevu na watambuzi, ukawafunulia wachanga. Ndio, Baba, kwani hivyo ndivyo, ulivyopendezwa navyo.
22
Vyote nimepewa na Baba yangu. Hakuna anayemtumbua Mwana, kama ni nani, pasipo Baba; wala hakuna anayemtambua Baba, kama ni nani, pasipo Mwana, na kila, Mwana atakayemfunulia.
23
*Akawapindukia wanafunzi, akawaambia, walipokuwa peke dyao: Yenye shangwe ni macho yanayoyaona, mnayoyaona ninyi.
24
Kwani nawaambiani: Wengi waliokuwa wafumbuaji na wafalme walitaka kuyaona, mnayoyaona ninyi, lakini hawakuyaona; walitaka kuyasikia, mnayoyasikia ninyi, lakini hawakuyasikia.
25
Pakawapo mjuzi wa Maonyo, akainuka, akamtega akisema: Mfunzi, nifanye nini, nipate kuurithi uzima wa kale na kale?
26
Naye akamwambia: Katika Maonyo imeandikwa nini? Unasomaje?
27
Akajibu akisema: Umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa nguvu yako yote na kwa mawazo yako yote! Naye mwenzio umpende, kama unavyojipenda mwenyewe!
28
Akamwambia: Umejibu kweli; yafanye hayo! Ndipo, utakapopata kuishi.
29
Lakini kwa sababu alitaka kujijulisha kuwa ni mwongofu, akamwambia Yesu: Mwenzangu ni nani?
30
Yesu akalishika neno hili akisema: Kulikuwa na mtu, alitoka Yerusalemu, akatelemka kwenda Yeriko, akaguiwa na wanyang'anyi. Hao walipokwisha kumvua nguo zake, na kumpiga vigongo, wakaenda zao na kumwacha, akitaka kufa.
31
Ikatukia, mtambikaji akiitelemkia njia ile; alipomwona akaepuka, akapita.
32
Vilevile hata Mlawi akafika mahali pale; lakini alipomwona akaepuka, akapita.
33
Kisha Msamaria aliyeifuata njia ile akaja huko, alikokuwa; alipomwona akamwonea uchungu,
34
akamjia, akamfunga madonda yake akiyamwagia mafuta na mvinyo, akampandisha juu ya punda wake yeye mwenyewe, akampeleka kifikioni, akamwuguza.
35
Siku ya kesho akatoa shilingi mbili, akampa mwenye fikio, akasema: Mwuguze huyu! Kama unatumia kuzipita hizi, nitakulipa zote nitakaporudi.
36
Waonaje? Katika hao watatu aliyejifanya kuwa mwenzake yule aliyeguiwa na wanyang'anyi ni yupi?
37
Naye akasema: Ndiye aliyemwonea huruma. Ndipo, Yesu alipomwambia: Nenda nawe, ufanye vivyo hivyo!*
38
*Walipokwenda zao, akaingia kijijini. Mlikuwa na mwanamke, jina lake Marta, akamfikiza nyumbani mwake.
39
Naye alikuwa na ndugu yake aliyeitwa Maria; huyu akajiketisha miguuni pa Bwana, akamsikiliza maneno yake.
40
Lakini Marta akabururwa huko na huko kwa utumikizi mwingi. Kisha akaja kusimama hapo, alipokuwa, akasema: Bwana, huvitazami, huyu ndugu yangu akiniacha, nitumike peke yangu? Umwambie, anisaidie!
41
Lakini Bwana akajibu akimwambia: Marta, Marta, unahangaika kwa kusumbukia mambo mengi.
42
Lakini vinavyopasa ni vichache au kimoja tu. Maria amelichagua fungu lililo jema, naye hatapokwa.*
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24