bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 13
Luke 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 14 →
1
*Siku zilezile walikuwapo watu waliomsimulia ya Wagalilea, ambao Pilato alimwaga damu zao na kuzichanganya na damu za ng'ombe zao za tambiko.
2
Akajibu akiwaambia: Mwadhani, Wagalilea hao walikuwa wakosaji kuwapita Wagalilea wote, maana wameteswa hivyo?
3
Nawaambiani: Sivyo, ila msipojuta nyote mtaangamia vivyo hivyo.
4
Au wale kumi na wanane, uliowaangukia mnara kule Siloa na kuwaua, je? Mwadhani, wamekuwa wenye kulipizwa kuwapita wenyeji wote wa Yerusalemu?
5
Nawaambiani: Sivyo, ila msipojuta nyote mtaangamia vivyo hivyo.
6
Akausema mfano huu: Mtu alikuwa na mkuyu uliopandwa mizabibuni kwake. Alipokuja kutafuta matunda yake hakuyaona.
7
Kisha akamwambia mlimia mizabibu: Tazama, imepita miaka mitatu, tangu nilipoanza kuja kutafuta matunda ya mkuyu huu, lakini siyaoni. Basi, uukate! Hulizuiliani shamba?
8
Lakini huyo akajibu akimwambia: Bwana, uuache mwaka huu tu, niuchimbie pembenipembeni, nikautilie mbolea!
9
Labda utazaa matunda siku zitakazokuja. Lakini usipozaa, basi, utaukata.*
10
Akawa akifundisha siku ya mapumziko katika nyumba moja ya kuombea.
11
Mle nyumbani mkawa na mwanamke mwenye pepo aliyemwuguza miaka 18; kwa hiyo alikuwa amepindana, asiweze kunyoka kamwe.
12
Yesu alipomwona akamwita, akamwambia: Mama, umefunguliwa huu unyonge wako;
13
Kisha akambandikia mikono yake. Papo hapo akanyoka, akamtukuza Mungu.
14
Lakini mkuu wa nyumba ya kuombea akamkasirikia Yesu, kwa sababu amemponya siku ya mapumziko, akawaambia watu waliokuwamo: Ziko siku sita za kufanya kazi; basi, mje siku hizo, mpate kuponywa, lakini msiponywe siku ya mapumziko!
15
Bwana akajibu akisema: Enyi wajanja, ninyi nyote hamwafungui ng'ombe au punda wenu zizini siku ya mapumziko na kuwapeleka, wanywe?
16
Lakini huyu aliye mwana wa Aburahamu haikumpasa kufunguliwa siku ya mapumziko kifungo hiki, Satani alichomfunga miaka 18?
17
Aliposema hayo, wabishi wake wakapatwa na soni wote, lakini wale watu wengi wote wakayafurahia mambo matukufu yote, aliyoyafanya.
18
Kisha akasema: Ufalme wa Mungu umefanana na nini? Niufananishe na nini?
19
Umefanana na kipunje cha haradali, alichokitwaa mtu na kukitupia shambani kwake. Nacho hukua na kupata kuwa mti, hata ndege wa angani hutua katika matawi yake.
20
Tena akasema: Ufalme wa Mungu niufananishe na nini?
21
Umefanana na chachu, mwanamke akiitwaa, akaichanganya na pishi tatu za unga, mpaka ukachachwa wote.
22
Naye alipofanya mwendo wa kwenda Yerusalemu akapita mijini na vijijini akiwafundisha.
23
Mtu alipomwuliza: Bwana, watu watakaookoka ni wachache tu? akamwambia:
24
Gombeeni, mpate kuuingia mlango ulio mfinyu! Nawaambiani: Wengi watataka kuuingia, lakini hawataweza.
25
Tangu hapo, mwenye nyumba atakapoinuka na kuufunga mlango, ndipo, mtakapoanza kusimama nje na kuugonga mlango mkisema: Bwana, Bwana, tufungulie! Naye atajibu akiwaambia: Siwajui ninyi, mtokako.
26
Ndipo, mtakapoanza kusema: Tumekula, tumekunywa machoni pako, nawe umetufundisha viwanjani petu.
27
Ndipo, atakapowaambia ninyi: Siwajui, mtokako, ondokeni kwangu nyote mfanyao mapotovu!
28
Ndiko, kitakakokuwa kilio na kukereza meno, mtakapowaona akina Aburahamu na Isaka na Yakobo na wafumbuaji wote, wamo katika ufalme wa Mungu, lakini ninyi wenyewe mtajiona, mmetupwa nje.
29
Wako watakaotoka maawioni na machweoni kwa jua na upande wa kaskazini na wa kusini, nao watakaa chakulani katika ufalme wa Mungu.
30
Tazameni, wako wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, tena wako wa kwanza watakaokuwa wa mwisho.
31
Saa ileile wakawako Mafariseo waliomjia, wakamwambia: Toka hapa, ujiendee! kwani Herode anataka kukuua.
32
Akawaambia: Nendeni, mkamwambie mbweha huyo: Tazama, leo na kesho nafukuza pepo na kuponya wagonjwa, nayo siku ya tatu mambo yangu yatamalizika.
33
Lakini leo na kesho na kesho kutwa sharti niende, kwani haiwezekani, mfumbuaji auawe, isipokuwa Yerusalemu.
34
Yerusalemu, Yerusalemu, unawaua wafumbuaji, ukawapiga mawe waliotumwa kwako! Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako, kama kuku anavyovikusanya vifaranga vyake mabawani! Lakini hamkutaka!
35
Mtaona, Nyumba yenu ikiachwa, iwe peke yake! Nawaambiani: Hamtaniona tena mpaka siku ile, mtakaposema: Na atukuzwe ajaye kwa Jina la Bwana!
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24