bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 23
Luke 23
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 24 →
1
Kisha wakainuka wale watu wengi wote pia, wakampeleka kwa Pilato.
2
Wakaanza kumsuta wakisema: Huyu tulimwona, anavyowapindua watu wa taifa letu na kuwakataza, wasitoe kodi za Kaisari, akisema: Mimi Kristo ni mfalme.
3
Pilato alipomwuliza akisema: Wewe ndiwe mfalme wa Wayuda? akamjibu akisema: Wewe unavyosema, ndivyo.
4
Pilato akawaambia watambikaji wakuu na makundi ya watu kwake huyu mtu sioni neno la kumhukumu.
5
Lakini wale wakakaza sana kusema: Anawatukusa watu akifundisha katika Yudea yote; naye ameanza Galilea, akafika mpaka hapa.
6
Lakini Pilato alipoyasikia haya akauliza, kama ni mtu wa Galilea.
7
Naye alipotambua, ya kuwa alitoka katika ufalme wa Herode, akamtuma kwa Herode, kwani naye alikuwako Yerusalemu siku zile.
8
Herode alipomwona Yesu akafurahi sana; kwani tangu siku nyingi alikuwa akitaka kumwona, kwa sababu aliyasikia mambo yake, akangojea kuona kielekezo kinachofanyizwa naye.
9
Akamwuliza mengi, lakini yeye hakumjibu neno.
10
Lakini watambikaji wakuu na waandishi waliosimama hapo wakajihimiza kumsuta.
11
Herode pamoja na askari wake walipokwisha kumbeza na kumfyoza, akamvika nguo nyeupe imetukayo, akamrudisha kwa Pilato!
12
Siku ile Herode na Pilato walianza kuwa rafiki, maana siku zilizopita walikuwa wanachukiana.
13
Pilato akawaita watambikaji wakuu na wakubwa na watu wa kwao, wakutane,
14
akawaambia: Mmemleta kwangu mtu huyu, kwamba anawapindua watu; tazameni, mimi nimemwulizauliza mbele yenu, nisione kwake mtu huyu, ya kuwa ameyakosa, mnayomsuta.
15
Hata Herode vile vile hakuona, kwani amemrudisha kwetu. Tazameni, hakukosa neno limpasalo kuuawa.
16
Basi, nitampiga, kisha nitamfungua.
17
Maana ilikuwa imempasa kuwafungulia mmoja kwa desturi ya sikukuu.
18
Watu wote pia wakapiga kelele wakisema: Umwondoe huyu, afe, utufungulie Baraba!
19
Naye Baraba alikuwa ametiwa kifungoni kwa ajili ya kondo iliyokuwamo mjini na kwa ajili ya kuua watu.
20
Pilato akasema nao tena, kwani alitaka kumfungua Yesu.
21
Lakini wakabisha wakisema: Mwambe msalabani! Mwambe msalabani!
22
Ndipo, alipowauliza mara ya tatu: Ni kiovu gani, alichokifanya huyu? Sikuona neno kwake la kumhukumu, auawe; basi, nitampiga, kisha nitamfungua.
23
Lakini wale wakamchokesha kwa kupiga makelele sana wakitaka, awambwe msalabani; ndivyo, makelele yao nayo ya watambikaji wakuu yalivyoshinda.
24
Pilato akakata shauri na kuyaitikia, waliyoyataka:
25
akamfungua yule aliyetiwa kifungoni kwa ajili ya kondo na ya kuua watu, ndiye waliyemtaka; lakini Yesu akamtoa, wamfanyizie watakavyo.
26
Walipompeleka wakamshika Simoni wa Kirene aliyepita akitoka shambani, wakamtwika msalaba, amchukulie Yesu na kumfuata.
27
*Wakamfuata watu wengi mno, hata wanawake waliojipigapiga vifua na kumlilia.
28
Yesu akawageukia, akasema: Enyi wanawake wa Yerusalemu, msinililie mimi, ila mjililie wenyewe na watoto wenu!
29
Kwani tazameni, siku zitakuja, watakaposema: Wenye shangwe ndio wagumba na matumbo yasiyozaa na maziwa yasiyonyonyesha!
30
Ndipo, watakapoanza kuiambia milima: Tuangukieni! na kuyaambia machuguu: Tufunikeni!
31
Kwani mti mbichi wakiufanyizia hivyo huo mkavu utakuwaje?
32
Wakapelekwa nao wengine wawili waliofanya maovu, wauawe pamoja naye.
33
Walipofika mahali panapoitwa Fuvu la Kichwa, wakamwamba msalabani pale yeye na wale wafanya maovu, mmoja kuumeni, mmoja kushotoni.
34
Kisha Yesu akasema: Baba, waondolee! Kwani hawajui wafanyayo.* Hata nguo zake wakazipigia kura, wazigawanyiane.
35
Nao watu walikuwa wamesimama wakitazama; lakini wakuu wakamfyoza wakisema: Wengine aliwaokoa, na ajiokoe mwenyewe, kama ndiye Kristo aliyechaguliwa na Mungu!
36
Nao askari wakamfyoza wakimkaribia na kumpelekea siki
37
wakisema: Kama ndiwe mfalme wa Wayuda, jiokoe!
38
Tena juu yake palikuwa pameandikwa Kigriki na Kiroma na Kiebureo: HUYU NDIYE MFALME WA WAYUDA.
39
*Mwenzao mmoja wale wafanya maovu waliotundikwa akambeza: Wewe siwe Kristo? Jiokoe mwenyewe na sisi!
40
Lakini mwenzake akajibu akimkaripia na kusema: Humwogopi Mungu wewe nawe, uliomo katika mapatilizo yaya haya?
41
Na sisi tumehukumiwa kweli, kwani tunalipizwa yaliyoyapasa matendo yetu; lakini huyu hakuna kipotovu, alichokifanya.
42
Kisha akasema: Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako!
43
Yesu akamwambia: Kweli nakuambia: Leo utakuwa pamoja nami katika Paradiso.
44
Ikawa, ilipofika kama saa sita, pakawa na giza katika nchi yote nzima mpaka saa tisa,
45
kwa kuwa jua liliacha kuwaka; ndipo, pazia la Jumbani mwa Mungu lilipopasuka katikati.
46
Yesu akapaza sauti kuu akisema: Baba, roho yangu naiweka mikononi mwako. Alipokwisha kuyasema haya, pumzi ikamtoka.*
47
Lakini bwana askari alipoliona lililokuwapo akamtukuza Mungu akisema: Kweli mtu huyu alikuwa mwongofu.
48
Nayo makundi yote ya watu waliokuwako kuyatazama hayo, walipoyaona yaliyokuwapo wakarudi kwao na kujipiga vifua.
49
Nao wote waliojuana naye walikuwa wamesimama mbali, hata wanawake waliofuatana naye toka Galilea walikuwako wakiyatazama hayo.
50
Ndipo, palipotokea mtu aliyekuwa mkuu, jina lake Yosefu wa Arimatia, ndio mji wa Wayuda. Huyo alikuwa mtu mwema na mwongofu;
51
kwa hiyo hakujitia katika mashauri na matendo yao; naye alikuwa akiungoja ufalme wa Mungu.
52
Huyo akaenda kwa Pilato, akataka kupewa mwili wa Yesu.
53
Akaushusha msalabani, akaufunga kwa sanda, akauweka katika kaburi lililochongwa mwambani, ambalo hajazikwa mtu bado ndani yake.
54
Nayo siku ile ilikuwa ya andalio; ndipo, sikukuu ilipoanzia.
55
Lakini wanawake waliokuja pamoja naye toka Galilea wakafuata, wakalitazama kaburi, tena jinsi mwili wake ulivyowekwa.
56
Kisha wakarudi, wakatengeneza viungo na manukato; lakini siku ya mapumziko wakakaa kimya, kama walivyoagizwa.
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 24 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24