bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 12
Luke 12
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 13 →
1
Makundi yalipokuwa yamekusanyika maelfu ya watu wakakanyagana kwa kuwa wengi; ndipo, alipoanza kuwaambia kwanza wanafunzi wake; Jilindeni kwa ajili ya chachu ya Mafariseo iliyo ujanja!
2
Hakuna lililofunikwa lisilofunuliwa halafu, wala hakuna lililofichwa lisilotambulikana halafu.
3
Maneno yote, mnayoyasema gizani, yatasikiwa mwangani; nalo mnalolinong'oneza masikioni nyumbani, litatangazwa barazani.
4
Lakini nawaambiani ninyi, wapenzi wangu: Msiwaogope wanaoweza kuiua miili tu, kisha hawana wanachoweza kuwafanyia tena!
5
Lakini nitawaonyeshani ninyi wa kumwogopa: Mwogopeni yule anayeweza kuwaua, kisha yuko na nguvu ya kuwatupa shimoni mwa moto! Kweli nawaambiani: Huyo mwogopeni!
6
Je? Videge vitano haviuzwi kwa senti mbili? Lakini hata mmoja wao hasahauliwi mbele ya Mungu.
7
Lakini kwenu ninyi hata nywele za vichwani penu zimehesabiwa zote. Kwa hiyo msiogope, ninyi mnapita videge vingi!
8
Lakini nawaambiani: Kila atakayeungama mbele ya watu, kwamba ni mtu wangu, naye Mwana wa mtu ataungama mbele ya malaika wa Mungu, kwamba ni mtu wangu.
9
Lakini atakayenikana mbele ya watu atakanwa mbele ya malaika wa Mungu.
10
Kila atakayesema neno la kumbisha Mwana wa mtu ataondolewa; lakini aliyembeza Roho Mtakatifu hataondolewa.
11
Lakini watakapowapeleka katika nyumba za kuombea na mabomani na pengine penye nguvu msihangaikie wala mizungu wala maneno ya kujikania wala ya kuwajibu!
12
Kwani Roho Mtakatifu atawafundisha saa ileile yapasayo kusema.
13
Kundini mwa watu alikuwamo aliyemwambia: Mfunzi, umwambie ndugu yangu, agawanye nami urithi, baba aliotuachia!
14
Naye akamwambia: Mwenzangu, yuko nani aliyeniweka, niwaamue na kuwagawanyia mali zenu?
15
*Akawaambia: Tazameni, mjilinde kwa ajili ya choyo cho chote! Kwani mali zikiwa nyingi sizo zinazomweka mtu, akizishika.
16
Akawaambia mfano akisema: Kulikuwa na mtu mwenye mali, ambaye shamba lake lilikuwa limezaa sana.
17
Ndipo, alipofikiri moyoni mwake akisema: Nifanyeje? Kwani sina pa kuyawekea mavuno yangu?
18
Kisha akasema: Nitafanya hivyo: nitayavunja mawekeo yangu, nijenge makubwa kuyapita hayo ndimo niziweke ngano zangu na mali zangu zote.
19
Ndipo, nitakapoiambia roho yangu: Roho yangu, unayo mema mengi yaliyowekwa ya miaka mingi. Basi, tulia, ule, unywe na kuchangamka!
20
Lakini Mungu akamwambia: Mpumbavu wee! Usiku huu watakutoza roho yako; nayo, uliyoyalimbika, yatakuwa ya nani?
21
Ndivyo, vinavyoendelea vya mwenye kukusanya mali nyingi, asipoziweka kwa Mungu.*
22
Akawaambia wanafunzi wake: Kwa hiyo nawaambiani: Msiyasumbukie maisha yenu mkisema: Tutakula nini? Wala msiisumbukie miili yenu mkisema: Tutavaa nini?
23
Kwani maisha hupita vyakula, nao mwili hupita mavazi.
24
Jifundisheni kwa makunguru! Hawapandi, wala hawavuni, wala hawana vichanja wala wekeo jingine. Naye Mungu anawalisha nao. Je? Ninyi hamwapiti ndege pakubwa?
25
Tena kwenu yuko nani anayeweza kwa kusumbuka kwake kujiongezea miaka yake kipande kama cha mkono tu?
26
Basi, msipokiweza hata kilicho kidogo sana, yale mengine mwayasumbukiaje?
27
Jifundisheni kwa maua ya uwago, kama yanavyokua! Hayafanyi kazi wala hayafumi nguo. Lakini nawaambiani: Hata Salomo katika utukufu wake wote hakuvikwa kama moja lao.
28
Basi, Mungu akiyavika hivyo majani ya porini yanayokaa leo tu, kesho yatupwe katika mabiwi, yateketee, je? Hatazidi kuwavika ninyi? Mbona mnamtegemea kidogo tu?
29
Basi, ninyi msiulize: Tutakula nini? au: Tutakunywa nini? Wala msijikweze!
30
Kwani wamizimu waliomo ulimwenguni ndio wanaoyatafuta hayo yote; lakini Baba yenu amewajua, ya kuwa mnapaswa nayo.
31
Lakini utafuteni ufalme wake! Ndivyo mtakavyopewa hayo.
32
Msiogope, mlio kikundi kidogo! Kwani baba yenu imempendeza kuwapa ninyi huo ufalme.
33
Uzeni vitu vyenu, mpate ya kuwagawia maskini! Jishoneeni mifuko isiyochakaa ya kuwekea mbinguni limbiko lisilopungua! Tena ndiko, kusikofika mwizi, wala kusikoharibiwa na mende.
34
Kwani limbiko lenu liliko, ndiko, nayo mioyo yenu itakakokuwa.
35
*Mwe mmejifunga viuno vyenu, nazo taa zenu ziwe zinawaka!
36
Nanyi mfanane na watu wanomngoja bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, kusudi wamfungulie mlango papo hapo, atakaporudi na kupiga hodi.
37
Wenye shangwe ni watumwa wale, ambao bwana atakapokuja atawakuta, wakikesha. Kweli nawaambiani: Atajifunga na kuwaketisha chakulani, naye atakuja kuwatumikia.
38
Wenye shangwe ndio, atakaowakuta hivyo, hata akija zamu ya pili au ya tatu ya kulinda usiku.
39
Lakini litambueni neno hili: kama mwenye nyumba angaliijua saa, mwizi atakayojia, hangaliacha, nyumba yake ibomeolewe.
40
Nanyi mwe tayari! Kwani Mwana wa mtu atajia saa, msiyomwazia.
41
Petero akasema: Bwana, mfano huu unatuambia sisi tu au watu wote?
42
Bwana akasema: Basi, yuko nani aliye mtunzaji mwelekevu na mwerevu, bwana wake atakayempa kuwatunza watumwa wake, awape posho, saa yao itakapofika?
43
Mwenye shangwe ni mtumwa yule, bwana wake atakayemkuta, akifanya hivyo, atakapokuja.*
44
Kweli nawaambiani: Atampa kuzitunza mali zake zote.
45
Lakini yule mtumwa akisema moyoni mwake: Bwana wangu anakawia, akaanza kuwapiga watumwa na vijakazi, hata kula na kunywa na kulewa,
46
bwana wake mtumwa yule atamjia siku, asiyomngojea, na saa, asiyoitambua, kisha atamchangua kuwa vipande viwili, nalo fungu lake atampa pamoja nao wasiomtegemea Mungu.
47
Maana yule mtumwa aliyeyatambua, bwana wake ayatakayo, asijitengeneze, wala asiyafanye hayo, aliyoyataka, huyo atapigwa fimbo nyingi.
48
Lakini yule asiyeyatambua alipofanya yapasayo kupigwa atapigwa fimbo chache. Kwani kila aliyepewa mengi, kwake yatatafutwa mengi, naye waliyemwagizia mengi watazidi kumwuliza mengi.
49
Nalijia kutupa moto nchini, tena hakuna ninachokitaka, ila uwake.
50
Lakini ninao ubatizo, ndio nibatizwe; nami ninasongeka sana, mpaka umalizike.
51
Mwaniwazia, kwamba nimejia kuiletea nchi utengemano? Nawaambiani: Sivyo, ila naleta matengano.
52
Kwani tokea sasa watu watano waliomo katika nyumba moja watatengana, watatu wagombanishe wawili, nao wawili wagombanishe watatu.
53
Watagombana baba na mwana wake, tena mwana na baba yake, tena mama na mwana wake wa kike, tena mwana wa kike na mama yake, vilevile mkwe na mkwewe.
54
Akayaambia makundi ya watu: Mnapoona wingu linalotoka machweoni, papo hapo mnasema: Mvua inakuja; nayo inakuja kweli.
55
Tena mnaposikia upepo unaovuma kusini mnasema: Litakuwa jua kali; nalo linakuwapo.
56
Enyi wajanja, mnayoyaona ya nchini na ya mbinguni mnajua kuyapambanua, mbona hamzipambanui siku hizi za sasa?
57
Tena ninyi wenyewe, mbona hamfuati uamuzi wenye wongofu?
58
Kwani mnapokwenda bomani, wewe na mshitaki wako, umkaze njiani, mpatane, maana asikukokote kwa mwenye hukumu, naye mwenye hukumu asikutie mkononi mwa mpiga fimbo, naye mpiga fimbo asikutie kifungoni.
59
Nakuambia: Hutatoka humo kabisa, mpaka utakapomaliza kulipa, isisalie hata senti moja.
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24