bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 17
Luke 17
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 18 →
1
Kisha akawaambia wanafunzi wake: Makwazo hayana budi kuja, lakini anayeyaleta atapatwa na mambo.
2
Akitundikwa shingoni pake jiwe kubwa la kusagia, kisha atumbukizwe baharini, inamfaa kuliko kukwaza mmoja tu aliye mwenzao hawa wadogo.
3
Jiangalieni! Ndugu yako akikukosea, umtishe! Naye akijuta, umwondolee!
4
Ijapo, akukosee mara saba siku moja na kukurudia mara saba na kusema: Nimejuta, sharti umwondolee!
5
Mitume wakamwambia Bwana: Tuongezee nguvu za kumtegemea Mungu!
6
Bwana akasema: Cheo chenu cha kumtegemea Mungu kikiwa kidogo kama kipunje cha mbegu, mtauambia mkuyu huu: Ng'oka hapo, ulipo, ujipande baharini! nao utawatii.
7
Kwenu yuko mwenye mtumwa wa kulima au wa kuchunga atakayemwambia huyo, akirudi toka shamba: Sasa hivi njoo, ukae chakulani?
8
Hatamwambia: Andalia chakula, nitakachokila, ujifunge nguo, unitumikie, mpaka nitakapokwisha kula na kunywa! Kisha nawe ule, unywe?
9
Je? Atamwambia mtumwa asante, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa?
10
Vivyo nanyi matakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa semeni: Sisi tu watumwa wasiofaa, tumefanya tu yaliyotupasa kuyafanya!
11
*Ikawa, alipokwenda Yerusalemu, akashika njia ya kupita katikati ya Samaria na Galilea.
12
Alipoingia kijijini akakutana na waume kumi wenye ukoma waliokuwa wamesimama mbali,
13
wakapaza sauti wakisema: Bwana Yesu, tuhurumie!
14
Alipowaona akawaambia: Nendeni kujionyesha kwa watambikaji! Ikawa, walipokwenda wakatakaswa.
15
Lakini mmoja wao alipoona, ya kuwa amepona, akarudi akimtukuza Mungu kwa sauti kuu.
16
Akamwangukia kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.
17
Yesu akajibu akisema: Sio kumi waliotakaswa? Wale tisa wako wapi?
18
Hawakuonekana wengine waliorudi, wamtukuze Mungu, pasipo huyu mgeni?
19
Akamwambia: Inuka, uende zako! Kunitegemea kwako kumekuponya.*
20
*Alipoulizwa na Mafariseo: Ufalme wa Mungu unakuja lini? akawajibu akisema: Ufalme wa Mungu unapokuja, watu hawatauona kwa macho,
21
wala hawatasema: Tazama, up hapa! au: Uko huko! Kwani ufalme wa Mungu umo ndani yenu.
22
Kisha akawaambia wanafunzi: Siku zitakuja, mtakapotunukia kuiona siku moja tu ya siku za Mwana wa mtu, msiione.
23
Nanyi watu watakapowaambia: Tazameni huko! Tazameni hapa! msiende huko, wala msiwafuate!
24
Kwani kama umeme unavyomulika mbinguni toka pembe hii mpaka pembe ile na kuviangaza vilivyoko chini ya mbingu, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa mtu, siku yake itakapofika.
25
Lakini kwanza imempasa kuteswa mengi na kukataliwa nao wa kizazi hiki.
26
Navyo vilivyokuwa siku za Noa, ndivyo vitakavyokuwa hata siku zile za Mwana wa mtu.
27
Walikuwa wakila, hata wakinywa, walikuwa wakioa, hata wakiozwa mpaka siku, Noa alipoingia katika chombo kikubwa, yakaja mafuriko makubwa ya maji, yakawaangamiza wote.
28
Ndivyo, vilivyokuwa hata siku za Loti: walikuwa wakila, hata wakinywa, wakinunua, hata wakiuza, wakipanda, hata wakijenga.
29
Lakini siku, Loti alipotoka Sodomu, ndipo, moto uliochanganyika na mawe ya kiberitiberiti ulipotoka mbinguni kama mvua, ukawaangamiza wote.
30
Vivyo hivyo vitakuwa siku ile, Mwana wa mtu atakapofunuliwa.*
31
Siku ile mtu atakayekuwapo nyumbani juu, vitu vyake vikiwa nyumbani, asiingie kuvichukua! Vivyo hivyo naye atakayekuwako shambani asivirudie vilivyoko nyuma!
32
Mkumbukeni mkewe Loti!
33
Atakayetafuta kuiponya roho yake ataiangamiza; naye atakayeiangamiza ataiponya, iwepo.
34
Nawaambiani: Usiku ule watu wawili watakaolalia kitanda kimoja, mmoja atapokewa, mwenzake ataachwa.
35
Wake wawili watakaokuwa wakisaga pamoja, mmoja atapokewa, mwenzake ataachwa.
36
Wawili watakaokuwako shambani, mmoja atapokewa, mwenzake ataachwa.
37
Walipojibu na kumwuliza: Wapi, Bwana? akawaambia: Penye nyamafu ndipo, nao tai watakapokusanyikia.
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24