bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 24
Luke 24
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
1
Siku ya kwanza ya juma wakaenda kaburini asubuhi na mapema wakichukua manukato, waliyoyatengeneza.
2
Wakaliona lile jiwe, limekwisha fingirishwa na kutoka kaburini.
3
Walipoingia, hawakuuona mwili wake Bwana Yesu.
4
Ikawa, walipopotelewa na jambo hili, mara wakawatokea watu wawili waliovaa nguo zimulikazo.
5
Kwa kuingiwa na woga, wakaziinamisha nyuso zao chini; ndipo, wale walipowaambia: Aliye hai mnamtafutiaje penye wafu?
6
Hayumo humu, ila amefufuliwa. Kumbukeni, alivyowaambia alipokuwa bado huko Galilea
7
akisema: Mwana wa mtu sharti atiwe mikononi mwa watu wakosaji, awambwe msalabani, kisha afufuke siku ya tatu!
8
Ndipo, walipoyakumbuka hayo maneno yake,
9
wakarudi toka kaburini, wakawasimulia wale kumi na mmoja na wengine wote haya yote.
10
Nao walikuwa Maria Magadalene na Yohana na Maria, mama yake Yakobo, na wengine waliokuwa pamoja nao; hao ndio waliowapasha mitume habari hizi.
11
Lakini wajapoyawazia maneno hayo kuwa upuzi tu, wasiwaitikie,
12
Petero akainuka, akapiga mbio kufika kaburini, akainama, akachungulia, akaiona sanda tu. Kisha akaenda zake na kulistaajabu moyoni mwake lililokuwapo.
13
*Siku ile wenzao wawili walikuwa wakienda, waje kijijini, jina lake Emao; mtu akitoka Yerusalemu, ni mwendo wa saa mbili.
14
Nao walikuwa wakiongeana hayo yote yaliyokuwapo.
15
Ikawa, wakiongea na kuulizana, Yesu mwenyewe akawakaribia, akaenda pamoja nao.
16
Lakini macho yao yalikuwa, kama yamefumbwa, wasipate kumtambua.
17
Alipowauliza: Ni maneno gani hayo, mnayoyaongea hapa njiani? wakasimama na kununa.
18
Mmoja wao, jina lake Kleofa, akajibu akimwambia: Wewe u mgeni peke yako Yerusalemu, usiyatambue yaliyokuwamo siku hizi?
19
Akawauliza: Yapi? Ndipo, walipomwambia: Mambo ya Yesu wa Nasareti! Alikuwa mfumbuaji mwenye nguvu ya kutenda na ya kusema mbele ya Mungu na mbele ya watu wote.
20
Huyo watambikaji wakuu na wakubwa wetu wamemtoa, ahukumiwe kuuawa, wakamwamba msalabani.
21
Lakini sisi twalimngojea, ya kuwa ndiye atakayewakomboa Waisiraeli. Yakiisha hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu hapo, yalipokuwapo.
22
Tena wako wanawake wa kwetu waliotushangaza; walikwenda kaburini asubuhi na mapema,
23
wasiuone mwili wake, wakaja, wakasema: Tumetokewa na malaika waliosema: Yeye yu hai.
24
Tena wako wenzetu waliokwenda kaburini, wakavikuta vivyo hivyo, kama wanawake walivyosema, lakini mwenyewe hawakumwona.
25
Ndipo, alipowaambia: Nyie msiotambua mambo, mnayo mioyo inayokawia kuyategemea yote, Wafumbuaji waliyoyasema.
26
Haikumpasa Kristo kuteswa hivyo, apate kuingia katika utukufu wake?
27
Akaanzia kwa Mose na kwa Wafumbuaji wote, akawaeleza, aliyoandikiwa katika Maandiko yote.
28
Walipokikaribia kijiji, walichokiendea, akajitendekeza, kama anataka kwenda mbele.
29
Lakini wakambembeleza sana wakisema: Fikia mwetu! kwani ni jioni, nalo jua limekwisha kuchwa. Basi, akaingia kufikia mwao.
30
Ikawa, alipokaa chakulani pamoja nao, akautwaa mkate, akauombea, akaumega, akawagawia.
31
Ndipo, macho yao yalipofumbuliwa, wakamtambua. Naye papo hapo alikuwa ametoweka machoni pao.
32
Kisha wakaambiana: Mioyo yetu humu ndani haikuwa ikiwaka moto, aliposema nasi njiani na kutueleza maana ya Maandiko?
33
Wakainuka saa ileile, wakarudi Yerusalemu, wakawakuta wale kumi na mmoja nao waliokuwa pamoja nao,
34
wamekusanyika na kusema: Bwana amefufuka kweli! Amemtokea Simoni!
35
Nao wakawasimulia, waliyoyaona njiani, na jinsi walivyomtambua, alipoumega mkate.*
36
Walipokuwa wakiongea hivyo, mwenyewe akaja kusimama katikati yao, akawaambia: Tengemaneni!
37
Wakastuka kwa kuingiwa na woga, wakawaza, wameona mzimu.
38
Akawaambia: Mbona mnahangaika hivyo? Tena kwa nini mawazo kama hayo yanawaingia mioyoni mwenu?
39
Yatazameni maganja yangu na miguu yangu, mjue: Ni mimi mwenyewe! Nipapaseni, mwone! Kwani mzimu hanayo nyama ya mwili wala mifupa, kama mnavyoniona mimi kuwa nayo.
40
Alipokwisha kuyasema haya akawaonyesha maganja na miguu.
41
Lakini walipokuwa hawajamtegemea bado kwa kufurahiwa na kwa kushangaa, akawauliza: Mnacho cha kula hapa?
42
Ndipo, walipompa kipande cha samaki kilichokaangwa.
43
Akakitwaa, akakila mbele yao.
44
Kisha akawaambia: Haya ndiyo maneno yangu, niliyowaambia nilipokuwapo bado kwenu, ya kwamba: Sharti yatimizwe yote, niliyoandikiwa katika Maonyo ya Mose na katika wafumbuaji na katika Mashangilio.
45
Ndipo, alipowafumbua akili, waelewe na Maandiko.
46
Akawaambia: Kwa hivyo vilivyoandikwa imempasa Kristo kuteswa na kufufuka katika wafu siku ya tatu;
47
kisha wao wa mataifa yote watatangaziwa kwa Jina lake, wajute, wapate kuondolewa makosa; hivi vianzie Yerusalemu!
48
Nanyi m mashahidi wa mambo haya.
49
Mtaniona mimi, nikituma kwenu kiagio cha Baba yangu! Lakini kaeni tu mjini, mpaka mtakapotiwa nguvu itokayo juu!
50
*Kisha akatoka nao, akawapeleka mpaka Betania; hapo akaiinua mikono yake, akawabariki.
51
Ikawa katika kuwabariki, akajitenga kwao akachukuliwa kwenda mbinguni.
52
Ndipo, walipomwangukia kifudifudi, kisha wakarudi Yerusalemu wenye furaha kuu.
53
Wakawapo hapo Patakatifu siku zote wakimtukuza Mungu.*
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24