bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Luke 18
Luke 18
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 19 →
1
Akawaambia mfano wa kwamba: Imewapasa kuomba siku zote pasipo kuchoka,
2
akasema: Katika mji fulani mlikuwa na mwamuzi asiyemwogopa Mungu, wala hakumcha mtu ye yote.
3
Tena mle mjini mlikuwa na mwanamke mjane aliyemwendea mara kwa mara na kusema: Niamua na mpingani wangu!
4
Lakini siku nyingi hakutaka; kisha akasema moyoni mwake: Ijapo, nisimwogope Mungu, wala nisimche mtu ye yote,
5
Lakini kwa sababu ananisumbua, nitamwamulia mjane huyo, mwisho asije, akanipiga machoni.
6
Bwana akasema: Sikilizeni, mwamuzi mwenye upotovu anavyosema!
7
Naye Mungu asiwaamulie aliowachagua, wakimlilia mchana na usiku? Au atawakawilia?
8
Nawaambiani: Atawaamulia upesi. Mwasemaje? Mwana wa mtu atakapokuja ataona wanaomtegemea nchini?
9
*Kulikuwa na watu waliojiwazia wenyewe kuwa waongofu, wakawabeza wengine, akawaambia mfano huu:
10
Watu wawili walipanda kwenda Patakatifu kuomba. Wa kwanza alikuwa Fariseo, wa pili mtoza kodi.
11
Fariseo akasimama, akaomba na kusema hivi moyoni mwake: Mungu, nakushukuru, kwa sababu sifanani na watu wengine walio wanyang'anyi, wapotovu, wagoni, wala sifanani na huyu mtoza kodi.
12
Kila juma nafunga siku mbili, tena ninatoa fungu la kumi la vyote, ninavyovipata.
13
Lakini mtoza kodi akasimama mbali, asitake hata kuyainua macho mbinguni, ila akajipiga kifua akisema: Mungu, nionee huruma mimi niliye mkosaji!
14
Nawaambiani: Huyu alishuka kwenda nyumbani kwake mwenye wongofu kuliko yule. Kwani kila anayejikweza mwenyewe atanyenyekezwa; naye anayejinyenyekeza mwenyewe atakwezwa.*
15
Wakamletea hata vitoto, awaguse. Lakini wanafunzi walipowaona waliwatisha.
16
Ndipo, Yesu alipowaita, waje kwake, akisema: Waacheni vitoto, waje kwangu, msiwazuie! Kwani walio hivyo ufalme wa Mungu ni wao.
17
Kweli nawaambiani: Mtu asiyeupokea ufalme wa Mungu kama kitoto hatauingia kamwe.
18
Kulikuwa na mkubwa, akamwuliza akisema: Mfunzi mwema, nifanye nini, niurithi uzima wa kale na kale?
19
Yesu akamwambia: Unaniitaje mwema? Hakuna aliye mwema, asipokuwa Mungu peke yake tu.
20
Maagizo unayajua, ya kwamba: Usizini! Usiue! Usiibe! Usisingizie! Mheshimu baba yako na mama yako!
21
Naye akasema: Hayo yote nimeyashika, tangu nilipokuwa kijana.
22
Yesu alipoyasikia akamwambia: Umesaza kimoja bado: vyote pia, ulivyo navyo, viuze, uvigawie maskini! Hivyo utakuwa na kilimbiko mbinguni. Kisha uje, unifuate!
23
Lakini alipoyasikia haya, akasikitika sana, kwani alikuwa mwenye mali nyingi.
24
Yesu alipomwona hivyo, akasema: Vitazameni vigumu vinavyowazuia waegemeao mali kuingia katika ufalme wa Mungu!
25
Masumbuko ya ngamia ya kupenya tunduni mwa sindano ni madogo kuliko yake mwenye mali ya kuuingia ufalme wa Mungu.
26
Wao waliosikia wakasema: Ikiwa hivyo, yuko nani awezaye kuokoka?
27
Akasema: Mambo yasiyowezekana kwa watu huwezekana kwa Mungu.
28
Petero akasema: Tazama, sisi tumeviacha vyetu vyote, tukakufuata wewe.
29
Ndipo, alipowaambia: Kweli nawaambiani: Hakuna mtu aliyeacha nyumba au mkewe au ndugu au wazazi au wana kwa ajili ya ufalme wa Mungu,
30
asiporudishiwa na kuongezwa mara nyingi siku hizi za kuwapo nchini; tena siku zile zitakazokuja ataupata nao uzima wa kale na kale.
31
*Akawatwaa wale kumi na wawili, akawaambia: Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu. Huko Mwana wa mtu aliyoandikiwa na wafumbuaji yatatimizwa yote:
32
atatiwa mikononi mwa wamizimu, afyozwe nao pamoja na kutukanwa na kutemewa mate.
33
Tena watampiga viboko, kisha watamwua. Naye siku ya tatu atafufuka.
34
Lakini hao hawakuyasikia haya hata kidogo, neno hili likawa limefichika, wasilijue maana, wasiyatambue yaliyosemwa.
35
Ikawa, alipokaribia Yeriko, palikuwa na kipofu aliyekaa njiani kando akiomba sadaka.
36
Aliposikia, kundi la watu linapita, akauliza: Kuna nini?
37
Wakamsimulia, ya kuwa Yesu wa Nasareti anapita.
38
Ndipo, alipopaza sauti akisema: Yesu, mwana wa Dawidi, nihurumie!
39
Wao waliotangulia walipomkaripia, anyamaze, yeye akakaza sana kupaza sauti: Mwana wa Dawidi, nihurumie!
40
Ndipo, Yesu aliposimama, akaagiza, aletwe kwake. Alipomfikia, akamwuliza:
41
Wataka, nikufanyie nini? Naye akasema: Bwana, nataka, nipate kuona.
42
Yesu akamwambia: Ona! Kunitegemea kwako kumekuponya.
43
Papo hapo akapata kuona, akamfuata akimtukuza Mungu. Nao watu wote walioviona wakamsifu Mungu.
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 19 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24