bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 1
Acts 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 2 →
1
*Mwenzangu Teofilo, katika kitabu cha kwanza nalikuandikia yote, Yesu aliyoanza kuyafanya na kuyafundisha
2
mpaka siku ile, alipopazwa mbinguni. Hapo alikuwa amekwisha kuwaagizia mitume, aliowachagua, mambo ya Roho takatifu.
3
Tena wale ndio, aliowatokea na kuwaonyesha mara kwa mara, ya kuwa anaishi, alipokuwa amekwisha kuteswa; zile siku za kuwaonekea na kusema nao mambo ya ufalme wa Mungu zilikuwa 40.
4
Alipokwisha kuwakusanya akawaagiza, wasitoke Yerusalemu, ila wakingoje kiagio cha Baba, mlichokisikia kwangu;
5
kwani Yohana alibatiza kwa maji, lakini ninyi mtabatizwa katika Roho takatifu, tena siku hizo zinazosalia ni chache tu.
6
Waliokusanyika walipomwuliza: Bwana, siku hizo ndipo, utakapowasimamishia Waisiraeli ufalme wao tena?
7
akawaambia: Si nyie waliopaswa na kutambua siku au saa, Baba alizoziweka kwa nguvu yake yeye;
8
ila mtapewa nguvu, Roho Mtakatifu atakapowashukia ninyi, kisha mtakuwa mashahidi wangu hapa Yerusalemu na katika nchi yote ya Yudea na ya Samaria, mfike hata mapeoni kwa nchi.
9
Naye alipokwisha kuyasema haya akainuliwa juu, wakitazama, wingu lilivyomchukua machoni pao.
10
Walipokuwa wakitumbuliza macho mbinguni, alikokwenda, mara waume wawili wenye nguo nyeupe wakasimama huko kwao,
11
nao wakasema: Nyie waume wa Galilea, mmesimamaje mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kwenu na kupazwa mbinguni atarudi vivyo hivyo, mlivyomwona, akienda zake mbinguni.*
12
Ndipo, walipoondoka penye huo mlima unaoitwa Wa Michekele, ulioko karibu ya Yerusalemu, ni mwendo usio na mwiko wa siku ya mapumziko; wakarudi Yerusalemu.
13
Walipokwisha ingia wakapanda kipaani mle walimokaa, ni Petero na Yohana na Yakobo na Anderea, Filipo na Toma, Bartolomeo na Mateo, Yakobo wa Alfeo na Simon Zelote na Yuda wa Yakobo.
14
Hao wote walishikamana na kutenda moyo mmoja wa kumwomba Mungu, wakawa pamoja na wale wanawake na Maria, mamake Yesu, na pamoja na ndugu zake.
15
Siku zile Petero aliinuka katikati ya ndugu waliokuwa wamekutana pamoja, wapata 120, akasema:
16
Waume ndugu zangu, ilipasa andiko litimie, Roho Mtakatifu alilolisema kale kinywani mwa Dawidi kwa ajili ya Yuda aliyekuwa kiongozi wao waliomkamata Yasu.
17
Kwani alikuwa amehesabiwa pamoja nasi, tena huu utumishi wetu ulikuwa bia moja naye.
18
Huyo amepata konde kwa mshahara wa upotovu, akaanguka kifudifudi, akatumbuka katikati, nayo matumbo yake yote yakatoka.
19
Vikatambulikana kwa wenyeji wote wa Yerusalemu, wakaliita konde lile kwa msemo wao Hakeldama, ni kwamba: Konde la Damu.
20
Kwani imeandikwa katika kitabu cha Mashangilio: Kao lake liwe hame tu, asioneke atakayetua mlemle. Tena: Mtu mwingine na autwae ukaguzi wake.
21
Basi, wako wenzetu waliokuwa pamoja nasi siku zote, Bwana Yesu alipoingia kwetu,
22
mpaka alipotoka tena, tangu hapo, Yohana alipobatiza, mpaka siku ile, alipopazwa na kutolewa kwetu; inapasa, mmoja wao awe shahidi wa ufufuko wake pamoja nasi.
23
Wakasimamisha wawili: Yosefu aliyeitwa Barsaba, aliyekuwa na jina jingine la Yusto, na Matia.
24
Kisha wakamwomba Mungu wakisema: Wewe Bwana, uitambuaye mioyo yao wote, tuonyeshe mmoja, uliyemchagua katika hawa wawili,
25
aupokee huu utumishi na utume, apashike mahali, Yuda alipotoka, aende zake mahali pake yeye.
26
Walipowapigia kura, kura ikamguia Matia; kwa hiyo akahesabiwa pamoja na wale mitume kumi na mmoja.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28