bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 14
Acts 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 15 →
1
Ikawa, walipokusanyika huko Ikonio nyumbani mwa kuombea mwa Wayuda, wakawaambia maneno yayo hayo, hata Wayuda na Wagriki wengi mno wakaja kuyategemea.
2
Lakini Wayuda waliokataa kutii wakaichokoza mioyo ya wamizimu na kuwawazisha maovu, wachukizwe na hao ndugu.
3
Wakakaa huko siku nyingi wakitangaza waziwazi, walivyoshikamana na Bwana, naye akayashuhudia hayo maneno, waliyoyasema ya magawio yake akitokeza vielekezo na vioja vilivyofanyizwa na mikono yao.
4
Watu waliokuwamo mle mjini wakakosana, wengine walikuwa upande wa Wayuda, wengine upande wa mitume.
5
Lakini wamizimu na Wayuda pamoja na wakubwa wao walitaka kuwashambulia, wawakorofishe na kuwapiga mawe.
6
Walipoyatambua wakakimbilia miji ya Likaonia na Listira na Derbe na mingine iliyoko kandokando.
7
Wakakaa huko wakiipiga hiyo mbiu njema.
8
Listira kulikuwa na mtu aliyekaa hawezi miguu; ni kiwete tangu hapo, alipotoka tumboni mwa mama yake, hakuweza kwenda kamwe.
9
Huyu alimsikiliza Paulo, alipokuwa akisema. Naye alipomkazia macho, akamwona, ya kuwa anatazamia kuponywa,
10
akamwambia kwa sauti kuu: Inuka, usimame kwa miguu yako, inyoke! Ndipo, alipoinuka na kuruka na kuzungukazunguka.
11
Makundi ya watu walipoona, Paulo alilolifanya, wakapaza sauti wakisema kwa Kilikaonia: Miungu imegeuka kufanana na sisi watu, ikatushukia.
12
Wakampa Barnaba jina lake Zeu na Paulo jina lake Herme, kwa sababu ndiye aliyekuwa mnenaji.
13
Kisha mtambikaji wa nyumba ya Zeu iliyokuwa nje ya mji akaleta ng'ombe na vilemba vya maua malangoni, yeye na makundi ya watu wakataka kuwachinjia ng'ombe za tambiko.
14
Lakini mitume Barnaba na Paulo walipoyasikia wakayararua mavazi yao, wakayarukia hayo makundi, wakapaza sauti
15
wakisema: Waume, haya mnayafanyia nini? Hata sisi tu watu wenye kufa kama ninyi. Tunawapigia mbiu njema, mwiache miungu hii ya bure, mmgeukie Mungu Mwenye uzima aliyeziumba mbingu na nchi na bahari navyo vyote vilivyomo.
16
Siku zilizopita aliwaacha wamizimu wote, wazishike njia zao;
17
lakini hakujitowesha kwenu, maana alifanya mema akiwapa mvua toka mbinguni na miaka ya mavuno mazuri, hivyo aliishibisha mioyo yenu vyakula na mashangilio.
18
Wakisema hivyo, ilisalia kidogo tu, wasiweze kuwazuia hao watu wengi, wasiwachinjie ng'ombe za tambiko.
19
Kisha Wayuda wakaja huko toka Antiokia na Ikonio, wakachokoza makundi ya watu, wakampiga Paulo mawe, wakamtoa mjini na kumburura wakidhani, amekwisha kufa.
20
Lakini wanafunzi walipomsimamia kwa kumzungukia, akainuka, akaingia mjini. Kesho yake akatoka pamoja na Barnaba kwenda Derbe.
21
Ule mji nao wakaupigia hiyo mbiu njema, wakapata wanafunzi wengi; kisha wakarudi kwenda Listira na Ikonio na Antiokia.
22
Wakaishupaza mioyo ya wanafunzi, wakawahimiza, wafulize kumtegemea Bwana, wakawaambia: Inatupasa kupatwa na maumivu mengi, tukiingia katika ufalme wa Mungu.
23
Kila mahali penye wateule wakawawekea wazee, wakawapeleka kwa Bwana, ambaye walianza kumtegemea, wakiwaombea pamoja na kufunga.
24
Wakaikata nchi ya Pisidia, wakafika Pamfilia,
25
wakalitangaza lile Neno mle Perge, wakatelemka kwenda Atalia.
26
Huko wakajipakia chomboni kwenda Antiokia; ndiko, walikotoka kwa kutumwa, wenzao wakiwaombea, Mungu awaongoze kwa upole katika kazi ile, waliyokwisha kuitimiza.
27
Walipofika wakawakusanya wateule, wakawasimulia yote, Mungu aliyoyafanya kwa kuwa nao, hata alivyowafungulia wamizimu mlango, nao wapate kumtegemea.
28
Siku, walizokaa huko pamoja na wanafunzi, si chache.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28