bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 9
Acts 9
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 10 →
1
Naye Sauli alikuwa akingali bado akiwatolea wanafunzi wa Bwana ukorofi kwa kuwatisha na kwa kuwaua. Akamwendea mtambikaji mkuu,
2
akataka kwake barua za kwenda Damasko, aende nazo kwenye nyumba za kuombea za Wayuda, kwa maana alitaka kuwafunga na kuwapeleka Yerusalemu wo wote, atakaowaona wa njia hiyo, wakiwa waume au wake.
3
Lakini alipokuwa akienda na kufika karibu ya Damasko, mara akamulikiwa na mwanga uliotoka mbinguni,
4
akaanguka chini, akasikia sauti iliyomwambia: Sauli, Sauli, unanifukuzaje?
5
Alipouliza: Ndiwe nani, Bwana? akajibu: Mimi ni Yesu, ambaye unanifukuza wewe.
6
Utashindwa na kupiga mateke penye machomeo. Lakini inuka, uingie mjini! Ndimo, utakamoambiwa yakupasayo, uyafanye.
7
Lakini wenziwe waliokuwa pamoja naye njiani walikuwa wamesimama, wasiweze kusema, kwa sababu waliusikia uvumi, wasione mtu.
8
Sauli alipoinuka chini, macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; kwa hiyo wakamshika mkono, wakampeleka Damasko.
9
Siku tatu akawapo, asione kitu, wala asile, wala asinywe.
10
Mlikuwa na mwanafunzi mle Damasko, jina lake Anania. Huyo Bwana akamwambia katika njozi: Anania! Aliposema: Tazama, nipo hapa Bwana!
11
Bwana akamwambia: Inuka, uende kufika penye barabara inayoitwa Nyofu, uulize nyumbani mwa Yuda, kama yumo mtu wa Tarso, jina lake Sauli. Kwani tazama, yumo katika kuomba.
12
Naye ameona mtu, jina lake Anania, anavyoingia humo, alimo, ambandikie mikono, apate kuona tena.
13
Anania akajibu: Bwana, nimesikia kwa watu wengi maovu yote, mtu huyo aliyowafanyia watakatifu wako walioko Yerusalemu.
14
Tena amepata ruhusa kwa watambikaji wakuu kuwafunga hapa wote pia wanaolitambikia Jina lako.
15
Lakini Bwana akamwambia: Nenda tu! Kwani mtu huyu ataniwia chombo kiteule cha kulipeleka Jina langu mbele yao wamizimu na wafalme na wana wa Isiraeli.
16
Nami nitamwonyesha mateso yote, atakayoteswa kwa ajili ya Jina langu.
17
Kisha Anania akaondoka, akaenda, akaingia nyumbani mle, akambandikia mikono akisema: Ndugu yangu Sauli, Bwana Yesu aliyekuotokea njiani, alipokuja, amenituma, upate kuona tena na kujazwa Roho takatifu.
18
Papo hapo pakawa kama magamba yaliyoanguka toka machoni pake, akaona, tena akainuka, akabatizwa.
19
Naye alipokwisha kula chakula akapata nguvu tena. Akakaa siku kidogo, pamoja na wanafunzi waliokuwamo Damasko,
20
hakukawia kuipiga mbiu ya Yesu katika nyumba za kuombea akisema: Huyo ndiye Mwana wa Mungu.
21
Wote waliomsikia wakahangaika mioyoni, wakasema: Je? Huyu siye aliyekuwa akiwateka Yerusalemu waliolitambikia Jina hili? Huku nako hakuyajia yayo hayo kuwafunga na kuwapeleka kwa watambikaji wakuu?
22
Lakini Sauli akakaza kutenda nguvu, akawatatanisha Wayuda waliokaa Damasko akiwashinda kwa kusema: Huyu ndiye Kristo.
23
Siku zilipokwisha pita nyingi, Wayuda wakala njama ya kumwangamiza,
24
lakini Sauli alipata kuitambua njama yao. Walipomwotea malangoni pa mji mchana na usiku, wapate kumwangamiza,
25
ndipo, wanafuanzi walipomchukua usiku, wakamtia kapuni, wakamshusha ukutani.
26
Alipofika Yerusalemu akajaribu kugandamiana na wanafunzi, wote wakiwa wakingali na woga wa kumwogopa, wasiitikie, ya kuwa ni mwanafunzi;
27
ndipo, Barnaba alipomchukua, akampeleka kwa mitume, akawasimulia, alivyomwona Bwana njiani, navyo alivyosema naye, tena alivyolitangaza Jina la Yesu huko Damasko waziwazi.
28
Kisha akafuatana nao akiingia, tena akitoka nao Yerusalemu, akalitangaza Jina la Bwana waziwazi.
29
Hata Wayuda waliotoka Ugriki akasema nao na kubishana nao. Ndipo, walipotafuta njia ya kumwangamiza.
30
Lakini ndugu walipoyatambua wakamsindikiza mpaka Kesaria, wakamtuma kwenda zake Tarso.
31
Hivyo wateule walitengamana pote katika Yudea na Galilea na Samaria, wakajijenga, wakaendeleana kwa kumcha Bwana, tena wakawa wengi wakitulizwa na Roho Mtakatifu.
32
Ikawa, Petero alipopita pote akashuka na kuwafikia hata watakatifu waliokaa Lida.
33
Huko akaona mtu, jina lake Enea, alikuwa amepooza na kulala kitandani miaka minane.
34
Petero akamwambia: Enea, Yesu Kristo anakuponya; inuka, ujitandikie mwenyewe! Papo hapo akainuka.
35
Walipomwona wao wote waliokaa Lida na Saroni, wakageuka, wamfuate Bwana.
36
Yope mlikuwamo mwanafunzi mwanamke, jina lake Tabea, maana yake ni Paa. Huyu alikuwa na matendo mema mengi ya kugawia wengi.
37
Ikawa, siku zile akaugua, akafa; kisha wakamwosha, wakamlaza katika chumba cha juu.
38
Kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu ya Yope, wanafunzi walisikia, ya kuwa Petero yuko huko; kwa hiyo wakatuma kwake watu wawili, wamwombe, asikawie kuja kwao.
39
Petero akainuka, akaenda nao. Alipofika, wakapanda naye kwenda katika chumba cha juu. Humo wanawake wajane wote wakamjia, wakasimama wakilia na kumwonyesha kanzu na nguo zote, alizowashonea yule Paa alipokuwa pamoja nao.
40
Petero akawatoa wote, waje nje, akapiga magoti, akamwomba Mungu na kuugeukia ule mwili wake, akasema: Tabea, inuka! Ndipo, alipoyafumbua macho yake; alipomwona Petero akajiketisha.
41
Naye akamshika mkono, akamwinua, akawaita wale watakatifu na wale wajane, akamsimamisha mbele yao, akiwa yu hai.
42
Vikaja kutambulikana Yope mjini mote; kwa hiyo wengi wakamtegemea Bwana.
43
Akakaa siku nyingi huko Yope kwa fundi wa kutengeneza ngozi, jina lake Simoni.
← Chapter 8
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 10 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28