bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 16
Acts 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 17 →
1
Akafika Derbe na Listira; huko kulikuwa na mwanafunzi, jina lake Timoteo, mwana wa mwanamke wa Kiyuda aliyemtegemea Bwana, lakini baba alikuwa Mgriki.
2
Kwa kuwa huyo alishuhudiwa vema na ndugu waliokuwamo mle Listira na Ikonio,
3
Paulo alimtaka, aondoke kwenda naye. Akamchukua, akamtahiri kwa ajili ya Wayuda waliokuwa katika miji ile, kwani wote walimjua, ya kuwa baba yake alikuwa Mgriki.
4
Walipozunguka katika miji ile wakawafundisha kuishika ile miiko iliyoagizwa nao mitume na wazee wa Yerusalemu.
5
Hivyo wateule wakapata nguvu za kumtegemea Bwana, wakawa wengi zaidi kwa kuongezwa kila siku.
6
Wakaikata nchi ya Furigia na ya Galatia wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasiliseme Neno lao katika Asia.
7
Walipofika Misia, wakajaribu kwenda Bitinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa.
8
Basi wakapita Misia, wakatelemka, wakafika Tiroa.
9
*Huko Paulo akatokewa na njozi usiku, akaona mtu wa Makedonia, amesimama na kumbembeleza kwamba: Vuka, uje Makedonia, utusaidie!
10
Alipokwisha kuiona njozi hiyo, papo hapo tukatafuta, jinsi tutakavyovuka, tuje Makedonia, maana sote tumejua kweli, ya kuwa ni Mungu aliyetuita, tuje, tuwapigie hiyo mbiu njema.
11
Tukaondoka Tiroa, tukaingia chomboni, tukaenda kwa tanga moja Samotirake; kesho yake tukafika Mji Mpya.
12
Toka huko tukafika Filipi, ni mji wa mbele wa upande huo wa Makedonia, tena ndimo, Waroma walimotua. Tulipokuwa tumekaa mjini mle siku kidogo
13
tukatoka langoni kwenda nje siku ya mapumziko, tukaenda kando ya mto, tulipowazia kuwa pao pa kuombea. Ndipo, tulipokaa, tukisema na wanawake waliokusanyika.
14
Palikuwapo mwanamke, jina lake Lidia; alitoka mji wa Tiatira, akawa mchuuzi wa nguo za kifalme. Kwa sababu alimcha Mungu, akasikiliza. Naye Bwana akamfunulia moyo, ayashike yaliyosemwa na Paulo.
15
Alipokwisha kubatizwa pamoja nao waliokuwamo mwake akatubembeleza na kusema: Kama mmeniona mimi kwamba: Ni mwenye kumtegemea Bwana, mwingie mwangu, mkae! Ndivyo, alivyotushurutisha.*
16
*Ikawa, sisi tulipokwenda kuomba, tukakutana na kijakazi mwenye pepo ya kuagua. Naye aliwachumia mabwana zake mali nyingi na uaguzi wake.
17
Pote, tulipokwenda, akatufuata, Paulo na sisi, akapaza sauti akisema: Watu hawa ndio watumwa wake Mungu alioko huko juu, nao huwatangazia njia ya wokovu.
18
Alipovifanya siku nyingi, vikamwumiza Paulo, akageuka, akamwambia yule pepo: Nakuagiza wewe kwa Jina la Yesu Kristo, umtoke! Naye akamtoka saa ileile.
19
Lakini mabwana zake walipoona, ya kuwa chumo lao la mali limewapotea, wakamshika Paulo na Sila, wakawaburura, wakaenda nao sokoni kwa wakubwa wa mji.
20
Wakawapeleka kwa mabwana wakubwa, wakasema: Watu hawa wanauchafua mji wetu; ni Wayuda,
21
hufundisha desturi zilizo mwiko kwetu kuzipokea au kuzifanya sisi tulio Waroma.
22
Watu wengi walipoinuka kuwaendea kwa nguvu, mabwana wakubwa wakawapokonya mavazi yao, wakaagiza, wapigwe.
23
Walipokwisha kuwapiga viboko vingi wakawatia kifungoni, wakamwagiza mlinda kifungo, awatie mahali pasipoingilikana.
24
Naye alipolipata agizo hili akawatia katika chumba cha ndani kabisa, tena miguu yao akaitia mikatale.
25
Lakini usiku wa manane Paulo na Sila wakamwomba Mungu na kumwimbia, wafungwa wenzao wakiwasikiliza.
26
Papo hapo nchi ikatetemeka sana, hata misingi ya kifungo ikatikisika; mara milango yote ikafunguka, hata minyororo yao wote ikakatika.
27
Mlinda kifungo akazinduka, akaona, milango ya kifungo iko wazi, akachomoa upanga, akataka kujiua, kwani alidhani, wafungwa wametoroka.
28
Lakini Paulo akamkemea na kupaza sauti akisema: Usijifanyie kiovu! Kwani sisi sote tupo hapa.
29
Akaagiza, taa ije, akarukia ndani na kutetemeka, akamwangukia Paulo na Sila.
30
Alipowapeleka nje na kuwauliza: Bwana zangu, inayonipasa kuyafanya, nipate kuokoka ndiyo nini?
31
wakasema: Mtegemee Bwana Yesu! Ndivyo, utakavyookoka wewe nao waliomo nyumbani mwako.
32
Wakamwambia Neno lake Mungu yeye nao wote waliokuwamo mwake.*
33
Akawakaribisha saa ileile ya usiku, akawaosha madonda ya mapigo yao, akabatizwa papo hapo yeye nao wote waliokuwa wake.
34
Kisha akawaingiza mwake, akawaandalia meza, akashangilia yeye nao wa nyumbani mwake wote, ya kuwa wamepata kumtegemea Mungu.
35
Kulipokucha, mabwana wakubwa wakawatuma wale askari waliowapiga, wamwambie: Wafungue watu wale!
36
Mlinda kifungo alipomwambia Paulo maneno haya kwamba: Mabwana wakubwa wametuma watu, mfunguliwe; sasa tokeni mwende na kutengemana!
37
Paulo akawaambia: Wametupiga mbele ya watu pasipo kutuhukumu sisi tulio Waroma na kututia kifungoni. Sasa je? Wanataka kutukimbiza na kufichaficha? Sivyo, sharti waje wenyewe, watutoe!
38
Askari waliowapiga walipowaambia mabwana wakubwa maneno haya, wakashikwa na woga kwa kusikia, ya kuwa ndio Waroma.
39
Wakaja, wakawabembeleza, wakawatoa, wakawaomba sana, watoke mjini mle.
40
Ndipo, walipotoka kifungoni, wakaingia nyumbani mwa Lidia; walipokwisha kuonana na ndugu na kuwatuliza mioyo wakaondoka.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28