bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 18
Acts 18
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 19 →
1
Kisha Paulo akatoka Atene, akafika Korinto.
2
Akaona Myuda mmoja, jina lake Akila, aliyezaliwa Ponto; naye alikuwa amekuja juzijuzi toka Italia pamoja na mkewe Puriskila, kwa sababu Kaisari Klaudio aliagiza, Wayuda wote watoke Roma. Akafikia kwao,
3
kwa sababu kazi yao ya ufundi ilikuwa moja, akakaa kwao, wakafanya kazi; maana walikuwa mafundi wa kushona mahema.
4
Lakini kila siku ya mapumziko akabishana nao Wayuda na Wagriki nyumbani mwa kuombea, akawafundisha na kuwashinda.
5
Lakini Sila na Timoteo walipofika toka nchi ya Makedonia, Paulo akafuliza kulitangaza Neno akiwashudia Wayuda, ya kuwa Yesu ndiye Kristo.
6
Lakini walipopingamana naye na kumtukana, akawakung'utia mavumbi ya nguo zake, akawaambia: Damu zetu zitavijia vichwa vyenu! Mimi simo, ila nimetakata nikienda tangu sasa kwao wamizimu.
7
Akaondoka mle, akaingia nyumbani mwa mtu mwenye kumcha Mungu, jina lake Tiro Yusto, ambaye nyumba yake ilikuwa imepakana na nyumba ya kuombea.
8
Lakini Krispo aliyekuwa mkubwa wa nyumba ya kuombea alimtegemea Bwana pamoja na waliokuwamo nyumbani mwake wote. Hata wenyeji wa Korinto wengi walipovisikia wakamtegemea, wakabatizwa.
9
Bwana akamwambia Paulo kwa njozi usiku: Usiogope, tangaza tu, usinyamaze!
10
Kwani mimi niko pamoja nawe, hakuna atakayekushika, akufanyie maovu. Kwani humu mjini ninao watu wengi.
11
Akakaa huko mwaka na miezi sita akifundisha kwao Neno la Mungu.
12
Lakini Galioni alipokuwa bwana mkubwa wa nchi ya Akea, Wayuda wakapatana kumwunukia Paulo, wakampeleka bomani,
13
wakasema: Huyu anawahimiza watu kumcha Mungu na kuyabeza Maonyo yake.
14
Naye Paulo alipotaka kukifumbua kinywa chake, Galioni akawaambia Wayuda: Nyie Wayuda, mtu huyu kama amekosa kwa kufanya kibaya cho chote, ingalifaa kuwasikiliza vema.
15
Lakini kama ni mabishano tu kwa ajili ya maneno na majina na maonyo ya kwenu, myatazame wenyewe! Mambo kama haya mimi sitaki kuyaamua.
16
Akawafukuza bomani.
17
Ndipo, wote walipomkamata Sostene, mkubwa wa nyumba ya kuombea, wakampiga mbele ya boma; lakini nayo hayo Galioni hakuyatazama.
18
Paulo alipokwisha kukaa huko tena siku nyingi akaagana na ndugu, akatweka kwenda Ushami, Puriskila na Akila wakiwa pamoja naye; kwanza akanyoa kichwa kule Kenkerea, kwani alikuwa amejitia mwiko.
19
Walipofika Efeso, akawaacha huko; naye mwenyewe akaingia nyumbani mwa kuombea, akaongea na Wayuda.
20
Lakini walipombembeleza, akae kwao kitambo, hakuwaitikia,
21
ila akaagana nao akisema: Sikukuu itakayokuja sharti niimalizie Yerusalemu, lakini Mungu akitaka, nitarudi kwenu tena. Alipoondoka Efeso,
22
akatweka, akafika Kesaria, akapanda kuamkiana na wateule; kisha akatelemka kwenda Antiokia.
23
Alipokwisha kukaa huko siku kidogo akaondoka tena, akakata nchi ya Galatia na ya Furigia na kuingia mji kwa mji akiwashupaza wanafunzi wote.
24
Kulikuwa na Myuda, jina lake Apolo, aliyezaliwa Alekisandria; alikuwa na nguvu ya kusema, tena nguvu yake ilitoka katika utambuzi wa Maandiko; naye akafika Efeso.
25
Huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana, akashurutishwa na Roho kusema na kuyafundisha mambo ya Yesu, yalivyo kweli, lakini aliujua ubatizo wa Yohana tu.
26
Huyo alipoanza kutangaza nyumbani mwa kuombea waziwazi, Puriskila na Akila wakamsikia nao, wakampokea, wakamfunulia vema njia ya Mungu, aijue kabisa.
27
Naye alipotaka kuvuka kwenda Akea, ndugu wakamtia moyo, wakawaandikia wanafunzi, wampokee. Alipofika huko akawasaidia sana waliogawiwa kumtegemea Bwana.
28
Kwani aliwashinda sana Wayuda mbele za watu wote akionyesha na kuyaeleza Maandiko, ya kuwa Yesu ni Kristo.
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 19 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28