bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Acts 13
Acts 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 14 →
1
Katika wateule waliokuwamo Antiokia walikuwa wafumbuaji na wafunzi, akina Barnaba na Simeoni aliyeitwa Nigeri na Lukio wa Kirene na Manaeni aliyelelewa pamoja na mfalme Herode, tena Sauli.
2
Hao walipokuwa wakimtumikia Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema: Nitengeeni Barnaba na Sauli, waifanye kazi, niliyowaitia!
3
Ndipo, walipofunga na kuomba, wakawabandikia mikono, kisha wakawasindikiza.
4
Kwa hivyo, walivyotumwa na Roho Mtakatifu, wakatelemka kwenda Seleukia; huko wakaingia chomboni kwenda Kipuro.
5
Walipofika Salami wakalitangaza Neno la Mungu katika nyumba za kuombea za Wayuda. Naye Yohana alikuwa pamoja nao akiwatumikia.
6
Wakakikata kisiwa chote wakienda kwa miguu mpaka Pafo, hapo wakaona mtu wa Kiyuda aliyekuwa mganga na mwaguaji wa uwongo, jina lake Baryesu.
7
Huyo alikaa kwa mtawala nchi Sergio Paulo aliyekuwa mtu mwelekevu. Alipomwita Barnaba na Sauli kwa kutaka kulisikia Neno la Mungu,
8
yule mganga Elima (kwani hii ndiyo maana ya jina lake) akawabishia mno akitaka kumpinga mtawala nchi, asije kumtegemea Mungu.
9
Lakini Sauli anayeitwa Paulo akajaa Roho takatifu, akamkazia macho,
10
akasema: Wewe mwana wa Msengenyaji, uliyejaa udanganyi na uovu wote, unachukizwa na wongofu wote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?
11
Sasa utaona, mkono wa Bwana ukikukamata! Utakuwa kipofu, usilione jua siku hizi! Papo hapo akaguiwa na kiwi cha macho na giza, akapapasapapasa akitafuta watu wa kumshika mkono.
12
Mtawala nchi alipoyaona yaliyofanyika, akaustaajabu huo ufundisho wa Bwana, akamtegemea.
13
Kisha Paulo na wenziwe wakajipakia chomboni, wakaondoka Pafo kwenda Perge katika Pamfilia; lakini Yohana akawaacha, akarudi Yerusalemu.
14
Walipoondoka Perge, wakakata nchi, wakafika Antiokia wa Pisidia; siku ya mapumziko wakaingia nyumbani mwa kuombea, wakakaa.
15
Mafungu ya Maonyo na ya Wafumbuaji yalipokwisha kusomwa, wakubwa wa nyumba ya kuombea wakatuma kwao kwamba: Ndugu zetu, mkiwa na neno la kuituliza mioyo ya watu lisemeni!
16
Ndipo, Paulo alipoinuka, akawapungia mkono, akasema: Waume wa Isiraeli, nanyi mnaomcha Mungu, sikilizeni!
17
Mungu wa watu hawa wa kwetu Waisiraeli aliwachagua baba zetu, akawakuza kuwa makundi makubwa, walipokaa ugenini katika nchi ya Misri. Kisha akaunyosha mkono wake, akawaongoza na kuwatoa kule,
18
akawavumilia jangwani miaka kama 40.
19
Alipokwisha poteza mataifa saba katika nchi ya Kanaani, akawapa nchi yao, waitwae.
20
Kisha akawapa waamuzi miaka kama 450, mpaka siku za mfumbuaji Samueli.
21
Walipotaka mfalme, Mungu akawapa Sauli, mwana wa Kisi, mtu wa shina la Benyamini, miaka 40.
22
Tena alipokwisha kumwondoa huyo akamwinua Dawidi, awe mfalme wao; mwenyewe akamshuhudia kwamba: Nimemwona Dawidi, mwana wa Isai, kuwa mtu anayeupendeza moyo wangu; ndiye atakayeyafanyiza yote, niyatakayo.
23
Katika uzao wake huyo Mungu akawaletea Waisiraeli mwokozi Yesu, kama alivyoagana nao.
24
Alipokuwa hajawatokea bado, Yohana alikwisha kuwatangazia watu wote wa Isiraeli ubatizo wa kujutisha.
25
Lakini Yohana alipoumaliza mwenendo wake akasema: Yeye, mnayeniwazia kuwa, mimi siye; lakini tazameni, anakuja nyuma yangu, ambaye hainipasi kumfungulia viatu vya miguu yake.
26
Waume ndugu zangu, wana wa uzao wa Aburahamu, nanyi mnaomcha Mungu, Neno la wokovu huu lilitumwa kufika kwetu sisi;
27
lakini wale wanaokaa Yerusalemu na wakubwa wao hawakumtambua huyo, wakamhukumu; ndivyo, walivyoyatimiza maneno ya Wafumbuaji yanayosomwa kila siku ya mapumziko.
28
Ijapokuwa hawakuona neno lolote la kumwua, wakamhimiza Pilato, aangamizwe.
29
Nao walipokwisha kuyatimiza yote, aliyoandikiwa, wakamwambua mtini, wakamzika kaburini;
30
lakini Mungu akamfufua katika wafu.
31
Kisha siku nyingi akaonekana kwao waliotoka pamoja naye Galilea kwenda kupanda Yerusalemu. Hao sasa ndio mashahidi wake kwenye watu wa kwetu.
32
Nasi tunawapigia mbiu njema ya kile kiagio, baba zetu walichokipata kwamba:
33
Mungu amekitimizia wana wetu alipomfufua Yesu. ndivyo, alivyoandikwa hata katika shangilio la pili: Wewe ndiwe Mwanangu, siku hii ya leo mimi nimekuzaa.
34
Lakini ya kuwa amemfufua katika wafu, asirudie tena kuoza, ndivyo, alivyosema kwamba: Nitawapa ninyi magawio matakatifu ya Dawidi yanayotegemeka.
35
Kwa hiyo anasema hata pengine: Hutamtoa akuchaye, apate kuoza.
36
Lakini Dawidi alipokwisha kuwatumikia waliokuwako siku zile kwa mapenzi yake Mungu, alipata kulala, akawekwa mahali pa baba zake, akapata kuoza.
37
Lakini yule Mungu aliyemfufua, hakupa kuoza.
38
Kwa hiyo waume ndugu, litambulkane kwenu, ya kuwa ni kwa ajili yake yeye, mkipigiwa mbiu ya kwamba: Makosa yameondolea!
39
Na tena: Yote yasiyowezekana kuondolewa kwa nguvu ya Maonyo ya Mose, kila mwenye kumtegemea Bwana anaondolewa nayo kwa nguvu yake yeye, awe mwongofu.
40
Kwa hiyo angalieni, ninyi yasiwajie yaliyosemwa na Wafumbuaji ya kuwa:
41
Ninyi wenye kubeza, angalieni na kustaajabu, mzizimke! Kwani mimi siku hizi nitatenda tendo, kama mtu angewasimulia tendo hilo, msingeliitikia.
42
Walipotoka hapo, wamizimu wakawaomba, nao waambiwe maneno hayo siku ya pili ya mapumziko.
43
Waliokuwamo nyumbani mwa kuombea walipotawanyika, Wayuda na wafuasi wengi waliomcha Mungu wakamfuata Paulo na Barnaba. Waliposema nao wakawahimiza, washikamane na magawio yake Mungu.
44
Siku ya mapumziko iliyofuata walikusanyika wao wa mji wote, walisikie Neno la Mungu.
45
Lakini Wayuda walipoyaona hayo makundi ya watu wakajazwa wivu, wakayabisha yaliyosemwa na Paulo na kumtukana.
46
Ndipo, Paulo na Barnaba waliposema waziwazi pasipo woga: Ilikuwa imepasa, ninyi mwambiwe wa kwanza Neno la Mungu. Lakini mnapolitupa na kujiwazia kwamba: Uzima wa kale na kale hauwafalii, basi, twawageukia wamizimu.
47
Kwani tumeagizwa hivyo na Bwana: Nimekuweka kuwa mwanga wa wamizimu, uwe wokovu wao hata mapeoni kwa nchi.
48
Wamizimu walipoyasikia haya wakafurahi, wakalitukuza Neno la Bwana, wakalitegemea wote waliokuwa wamewekewa kupata uzima wa kale na kale.
49
Ndivyo, Neno la Bwana lilivyoenea katika nchi ile yote.
50
Lakini Wayuda waliwachokoza wanawake wakuu walioyashika matambiko yao, hata wakubwa wa mji, wakawachukua, wawashambulie akina Paulo na Barnaba, wakawafukuza, watoke mipakani kwao.
51
Ndipo, walipowakung'utia mavumbi ya miguuni, wakaenda, wakaja Ikonio.
52
Lakini wanafunzi wakajazwa furaha na Roho takatifu.
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28